Msikilizeni Zitto Star TV

Msikilizeni Zitto Star TV

akiongea startv asubuhi amesema wataanza kusambaza uzalendo wiki ijayo kwa kufanya ziara kupita mikoa 14.

Zitto Z Kabwe
Ndg Mwanachama na rafiki wa ACT Wazalendo,
tunaanza awamu ya pili ya ziara ya
kutambulisha chama chetu na kuhamasisha
wananchi kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la kupiga kura. Ili kufanikisha ziara hii
tunahitaji fedha kununua mafuta, kukodisha
magari na kujikimu. Tunaomba mchango wako
wa tshs 10,000 tu. Tuma mchango wako
kwenye namba 0763463740 (ACT POLITICAL)
au 0715784670 (ACT TANZANIA) au NMB A/C
NO. 22610004083 ACT-TANZANIA.[/QUOTE kazi nzuri tutaichangia

ukisha changia utujulishe!!!
 
Zitto anajidai kumuenzi Nyerere wakati Siasa zake zote na wapambe wake zimebase kwenye Ukanda,Udini na Ukabila na kuhonga vyombo vya habari vitu ambavyo ni kinyume kabisa na Nyerere,JF lazima isikilize members wake wake sio kupiga Ban watu wanaomkosoa Zitto.
 
Nimemsikiliza vizuri, hakuna la maana aliloongea ambalo naweza lilipoti hapa!! Acha kuwa msukule wa Zitto, jitambue utoke kuwa mfuasi wa mtu uwe mfuasi wa itikadi!! CDM ina majibu yote kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi pamoja na matatizo yanayotukabiri wanyonge!! Sio hizo porojo za umimi za Msaliti Zitto!!

Mbona mpo kimya basi! haya mwambieni Lema au Sungu watudadavulie chanzo cha tattizo na ufumbuzi wake. Subutuu!!!
 
akiongea startv asubuhi amesema wataanza kusambaza uzalendo wiki ijayo kwa kufanya ziara kupita mikoa 14.

Zitto Z Kabwe
Ndg Mwanachama na rafiki wa ACT Wazalendo,
tunaanza awamu ya pili ya ziara ya
kutambulisha chama chetu na kuhamasisha
wananchi kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la kupiga kura. Ili kufanikisha ziara hii
tunahitaji fedha kununua mafuta, kukodisha
magari na kujikimu. Tunaomba mchango wako
wa tshs 10,000 tu. Tuma mchango wako
kwenye namba 0763463740 (ACT POLITICAL)
au 0715784670 (ACT TANZANIA) au NMB A/C
NO. 22610004083 ACT-TANZANIA.[/QUOTE kazi nzuri tutaichangia

hell nooooh! Biblia inasema usitupe chakula cha watoto kwa mbwa
 
Mbona mpo kimya basi! haya mwambieni Lema au Sungu watudadavulie chanzo cha tattizo na ufumbuzi wake. Subutuu!!!

unafikiri hao ndiyo CHADEMA pekee kwenye mamilioni ya wafuasi? Ayaatoolahh Zitto kawaharibu akili kweli kweli
 
unafikiri hao ndiyo CHADEMA pekee kwenye mamilioni ya wafuasi? Ayaatoolahh Zitto kawaharibu akili kweli kweli

Haya basi Taifa linaangamia! Mtowoni huyo Mwenye uwezo huo aongee tumsikie basi. Inakuwaje Mamilioni yanatetemeka na jeshi la mtu mmoja.
 
Zzk ni mchumi?au ni kifupi cha mchumia tumbo?

Mpaka mjadala wenyewe unapoteza mwelekeo, kuna watu humu hata Mungu wanaweza kumwita shetani kama maslahi ya bwana zao yameguswa..
 
Mi sitaki kuamini kama kweli wewe ni Chadema! Unamtukana mama yake? We sio wa Chadema. Siamini kabisa! Inaonekana huna elimu hata ya chekechea! Elimu ndogo ni tatizo! Lasivyo yawezekana ulimchungulia mzazi wako jinsia ya KE sehemu nyeti ukapata laana! Sio bure! manaake huwaheshim akina mama!

Hiyo laana uloachiwa itaendelea kukutafuna milele daima! Ungama dhambi zako hujachelewa. Mheshim mama ako na akina mama wote ili upate baraka.

Siasa sio ugomvi na matusi dhidi ya wazazi wetu tena wasiohusika. Washabiki wa MAGAMBA waache washabikie au waelimishe, wafuasi wa ACT nao vivyohivyo.

Nikweli CCM imetuchosha, ila harakati za kuitoa CCM madarakani haziwezi kufanikiwa kwa matusi na vitu vingine vinavyofanana na hivyo. Jenga hoja Watanzania wakuelewe.

Kuna watu wamezivua akili zao, wanatukanag kila aina ya tusi, na imekuwa kama sera maalumu ya Chama chao, matusi
 
zzk kaenda kuzungumzia kushuka kwa sh.we unatukana mbn we ukwenda ila cdm imetuharbia vijana co siri uwez kuskiliza point ya mtu km unamchukia uo ni ujinga ulopitiliza mashabiki wa cdm badliken jaman
 
bado hajui kwamba tsh imeshuka dhidi ya currencies nyingine...
kama kawa jisukule la mbowe at work. jianaume zima linafanya kazi ya kulamba miguu ya mwanaume mwengine. mwanaume hatakiwi kuwa laini kiasi hicho.
 
"funguwa website, www.zittokabwefoundationvicoba.wapka.mobi"


je huyu jamaa ndiyo mwenye hii vicoba akishirikiana na vicky kamata na je kweli watu wananufaika au utapeli?
 
Tatizo ni kuhama chama!!! Tatizo ni kuwa ACT wazalendo!!! Tatizo ni kiongozi wa chama!!.! Tatizo ni Zito!!!?
 
Nataka kurudi Chadema mara baada ya .....

Nitayaamini maneno yanayotolewa na wanachadema siku siku haya maswali yakipatiwa majawabu

Natamani sana kuwa Kamanda lakini haya yananitatanisha,naombeni majibu ili nifanye maamuzi magumu.

1.Walituambia kuwa chama cha wananchi CUF ni tawi la ccm,wakaenda mbali kwa kuwaita kuwa ni chama cha Mashoga ghafla wakasahau matusi yao na wakaanza mashirikiano Mapya,Je ile tuhuma iliishia wapi?

2.Chadema walituaminisha kuwa Chama cha NCCR mageuzi kimejaa Usalama wa Taifa,wakaenda mbali wakamkejeli Mbatia, tena ndani ya Bunge kuwa,yupo Upinzani huku akiitumikia ccm,ghafla tu Mbatia ni Mshirika namba Mbili wa Ukawa bila watanzania kuelezwa kama zile tuhuma zilikuwa za kweli au za kutunga kwa nia ya kuwalaghai watu.

3.Chadema kwenye Ilani yake 2010 walituambia kuwa tukiwachagua hawatachukua posho kama hatua mojawapo ya kuonyesha kwa vitendo kuchukizwa na matumizi mabaya ya serikali.Je Kwanini wamekiuka Ilani yao?

4.Chadema Mwaka 2011 walikataa kushirikiana na vyama vya Upinzani ili kuunda kambi ya Upinzani yenye sauti na nguvu,wakatuambia kuwa Vyama vyote ni mawakala wa ccm isipokuwa Chadema,hivyo kushirikiana nao ni kurudisha nyuma harakati za ukombozi,ghafla tu baraza kivuli la mawaziri likavunjwa na wale vibaraka wa ccm wakaingizwa kwenye kambi ya upinzani bila sisi wafuasi kuambiwa ni lini ukibaraka wao umeisha mpaka wakaaminiwa.

5.Tuliambiwa kuwa David Kafulila ni mtu hatari kwa ustawi wa Upinzani hasa Chadema,tukaambiwa ni Sisimizi ambae hana umuhimu wowote ndani ya Chadema ,ghafla tu Sisimizi kageuka tembo,Mtu hatari kageuka Shujaa na sasa ananadiwa na viongozi wa Chadema kuwa ukawa imepata tuzo,Je ni lini kafulila alianza kuaminiwa ?

6.Tuliambiwa tena kuwa ,Serikali kutumia mashangingi huku Zahanati hazina dawa ni kiwango cha juu cha Ubinafsi,Mbowe akalikataa Shangingi la Kiongozi wa Upinzani....ghafla nimemuona Bukoba akiwa na Shangingi lenye maandishi KUB. Je ndio lilelile alilolikataa hadharani au ni lingine?

7.Mbowe alituahidi kwenda mahakamani,na kudai kuwa wanasheria wake wanaandaa mashtaka dhidi ya Zitto Kabwe baada ya Zitto kumtuhumu kuwa alipokea fedha toka kwa makada wa ccm na kuwa alicheza dili ns Kinana kuhusu deni analodaiwa na NSSF.Je taratibu za ufunguaji kesi ziliishia wapi ?

8. Chadema Mwaka 2011 ilitangazia Umma kutomtambua Rais Kikwete kwakuwa alishindwa na Slaa,ghafla wanatangaza kuomba mashauriano na Rais waliemkataa,wakafika Ikulu kujadiliana juu ya maswala mbalimbali ya Kitaifa,wakanywa Juice na kupiga picha,Je ni lini Chadema ilianza kumtambua Rais na kwanini sisi wananchi hatukuelezwa kuwa kuanzia sasa Kikwete ni Rais?
Sina nia ya kuibua Marumbano yasiyotujenga bali nataka mtu mwenye uelewa mkubwa kuliko mimi anaondoe Uvulivuli ili nami nijitambue.


Naomba nijibiwe hayo ili nami niwe Kamanda nitakaeitetea Chadema popote.

Hayo Majawabu yakipatikana,ndio utakuwa mwisho wa Chama cha ACT-Wazalendo maana umma utaiamini Chadema na hivyo kuiunga mkono.

Kama Maswali yakikosa Majibu basi Chadema itakosa uhalali wa kutuhumu ACT-Wazalendo na viongozi wake na hivyo wananchi wataendelea kujiunga na ACT-Wazalendo kwa kuamini kuwa maneno yoyote yanayotolewa na Chadema ni Ulaghai.

Karibuni kwa majibu Makamanda ili nasi tupate chakuwaambia wananchi ili waipuuze ACT-Wazalendo.

Mhh!!.
Kama ndivyo walivyo. Nina akili timamu. Nachanganya hizo na zangu!
 
zzk kaenda kuzungumzia kushuka kwa sh.we unatukana mbn we ukwenda ila cdm imetuharbia vijana co siri uwez kuskiliza point ya mtu km unamchukia uo ni ujinga ulopitiliza mashabiki wa cdm badliken jaman

Ni kichekesho kwa kuwa gavana na kamati imezungumzia na waziri Mwigulu kazungumzia , Kafulila alikuwapo sasa naenda kuzungumza nini wakati wenye dhamana wamezungumza vizuri sana. Proffessor Ndulu si ----- kama mnavotaka kufikiri ,ni kichwa kizuri kanifundisha finance huyo kiongozi anajua nni cha ziada zaidi ya wenye data,
 
Kusema kweli ule waraka Mwigamba aliomwandikia Zitto umenifanya nimfahamu Zitto vizuri. Kumbe tuhuma zoote anazohusishwa nazo ni za kweli. Kwa sababu SABABU alichosema Mwigamba kuhusu Zitto kilitoka kwenye unbiased perspective kwa wakati ule. Zitto ana matatizo ya msingi. Na hili tatizo la ubinafsi 'one man show" personal glory ambayo Pasco ameyazumgumzia sana kuhsu Zitto ndiyo yatakayomwangusha. Zitto haamini katika taasisi! Ukimsikliza mara nyingi kwenye mazungumzo yake neno, "nimefanya, nilishauri niltoa hoja, nili, mimi, nime, nime...He only believes in himself. He is myopic! Hili tatiz sijui linatokana na makuzi au ni udhaifu wa kawaida! Lakini km Mwigamba alivyomwambia, Zitto amekuwa katika special mission tangu 2008 kuimaliza Chadema. Mambo mengine nilikuwa nayatilia shaka laini waraka wa mwigamba kwa zitto umenifanya niamini kwamba asilimia kubwa ya tuhuma dhidi ya Zitto ni za kweli!

Huyu kitaalamu tunamwita "Resource innovator". Ni aina ya watu wanaozusha fikra na kusimamia kile wanachokiamini. Na Mara zote hufanikiwa. Wazo lolote linalokuja nje ya gikra huchukuliwa kwa tahadhari kubwa.

Ni watu nadra sana katika jamii.
 
We acha tu, kasababisha nichelewe kunywa chai, uchumi wa nchi anaujua vizuri, juzi nilimsikiliza Mbatia yaani alikuwa anaongea pumba hadi roho ikaniuma eti waziri kivuli wa fedha hovyo kabisa. Zitto amekomaa kiuchumi, kuna mambo amenifungua macho, kuwa sasa uchumi wetu unategemea watalii mgodi wa Geita na mauzo ya viti vya plastic, ndo kilimo kifuate, hii ni habari mbaya kabisa kusikia.

Kushuka kwa kilimo cha pamba kwa 40% hii ni habari ya kushitua sana, wakati mjerumani alisema pamba ni white gold sie imegeuka laana. Japo mvua zinanyesha mashamba yote hayajalimwa, yale majembe ya kukokotwa na ng'ombe hayapo tena.

Pia amegusia kuwa upumbavu wa hawa jamaa kusema nchi hatatawalika kunaleta hofu kwa watu wenye mitaji yao.

Huyo Zitto anakwepa mambo ya msingi hasa yanayoigusa CCM ndio maana hoja zake zinapinda , anawaweza nyie ambao hamkusoma , sie wengine tuna elimu kubwa ya finance na economics hana jeuri ya kunihadaa huyo, na sio mimi tu wapo watu wengi huyu bwana hawezi kuwahadaa nyie form four ndio mnamuona mchumi wa taifa yaani Napata kicheko sana. Mwambie aende UDBS akawaone wachumi kibao.Waziri ametaja vizuri hizo sababu za kuporomoka shilingi, ametoa specific na genuine reasons so far as finance is concerned Zitto analeta theory na kujenalise kukwepa kutaja uozo wa CCM wakati gavana kasema bila chenga
 
Kumbe ww unaonekana ni mfuata watu, we are much concerned with party's Policies sio utoto wenu wa kuigiza cdm mchana usiku mko na ccm kupanga hujuma
Kama na wewe ni mmoja wa inner circle ya CHADEMA basi wamekula hasara. Kichwa box kabisa, kinachojadiliwa kingine na wewe unakuja na jambo lingine tofauti kabisa.Usomege uelewe kwanza,sio unakurupuka tu kushambulia watu na kuwatupia tuhuma juu ya mambo yasiyokuwepo.Nyambafu!
 
Back
Top Bottom