Msikilizeni Zitto Star TV

Msikilizeni Zitto Star TV

Watanzania wamekuwa werevu mno miaka hii. Tapeli anajulikana mapema kabla jua halijachomoza.
Zitto na utapeli wake hataweza kutapeli watanzania

hayupo mtu wa kudanganya tena, acheni atumie fedha kama bajeti ya CCM inavyoelekeza watu wapate mishiko then tusubiri kura za wananchi kwa UKAWA PEKEE

Huyu dogo apigwe sahiv anatuhujumu wananchi

mmeamka wote hata kusali hamwendi kisa zzk atawatoa kamasi
 
Nataka kurudi Chadema mara baada ya .....

Nitayaamini maneno yanayotolewa na wanachadema siku siku haya maswali yakipatiwa majawabu

Natamani sana kuwa Kamanda lakini haya yananitatanisha,naombeni majibu ili nifanye maamuzi magumu.

1.Walituambia kuwa chama cha wananchi CUF ni tawi la ccm,wakaenda mbali kwa kuwaita kuwa ni chama cha Mashoga ghafla wakasahau matusi yao na wakaanza mashirikiano Mapya,Je ile tuhuma iliishia wapi?

2.Chadema walituaminisha kuwa Chama cha NCCR mageuzi kimejaa Usalama wa Taifa,wakaenda mbali wakamkejeli Mbatia, tena ndani ya Bunge kuwa,yupo Upinzani huku akiitumikia ccm,ghafla tu Mbatia ni Mshirika namba Mbili wa Ukawa bila watanzania kuelezwa kama zile tuhuma zilikuwa za kweli au za kutunga kwa nia ya kuwalaghai watu.

3.Chadema kwenye Ilani yake 2010 walituambia kuwa tukiwachagua hawatachukua posho kama hatua mojawapo ya kuonyesha kwa vitendo kuchukizwa na matumizi mabaya ya serikali.Je Kwanini wamekiuka Ilani yao?

4.Chadema Mwaka 2011 walikataa kushirikiana na vyama vya Upinzani ili kuunda kambi ya Upinzani yenye sauti na nguvu,wakatuambia kuwa Vyama vyote ni mawakala wa ccm isipokuwa Chadema,hivyo kushirikiana nao ni kurudisha nyuma harakati za ukombozi,ghafla tu baraza kivuli la mawaziri likavunjwa na wale vibaraka wa ccm wakaingizwa kwenye kambi ya upinzani bila sisi wafuasi kuambiwa ni lini ukibaraka wao umeisha mpaka wakaaminiwa.

5.Tuliambiwa kuwa David Kafulila ni mtu hatari kwa ustawi wa Upinzani hasa Chadema,tukaambiwa ni Sisimizi ambae hana umuhimu wowote ndani ya Chadema ,ghafla tu Sisimizi kageuka tembo,Mtu hatari kageuka Shujaa na sasa ananadiwa na viongozi wa Chadema kuwa ukawa imepata tuzo,Je ni lini kafulila alianza kuaminiwa ?

6.Tuliambiwa tena kuwa ,Serikali kutumia mashangingi huku Zahanati hazina dawa ni kiwango cha juu cha Ubinafsi,Mbowe akalikataa Shangingi la Kiongozi wa Upinzani....ghafla nimemuona Bukoba akiwa na Shangingi lenye maandishi KUB. Je ndio lilelile alilolikataa hadharani au ni lingine?

7.Mbowe alituahidi kwenda mahakamani,na kudai kuwa wanasheria wake wanaandaa mashtaka dhidi ya Zitto Kabwe baada ya Zitto kumtuhumu kuwa alipokea fedha toka kwa makada wa ccm na kuwa alicheza dili ns Kinana kuhusu deni analodaiwa na NSSF.Je taratibu za ufunguaji kesi ziliishia wapi ?

8. Chadema Mwaka 2011 ilitangazia Umma kutomtambua Rais Kikwete kwakuwa alishindwa na Slaa,ghafla wanatangaza kuomba mashauriano na Rais waliemkataa,wakafika Ikulu kujadiliana juu ya maswala mbalimbali ya Kitaifa,wakanywa Juice na kupiga picha,Je ni lini Chadema ilianza kumtambua Rais na kwanini sisi wananchi hatukuelezwa kuwa kuanzia sasa Kikwete ni Rais?
Sina nia ya kuibua Marumbano yasiyotujenga bali nataka mtu mwenye uelewa mkubwa kuliko mimi anaondoe Uvulivuli ili nami nijitambue.


Naomba nijibiwe hayo ili nami niwe Kamanda nitakaeitetea Chadema popote.

Hayo Majawabu yakipatikana,ndio utakuwa mwisho wa Chama cha ACT-Wazalendo maana umma utaiamini Chadema na hivyo kuiunga mkono.

Kama Maswali yakikosa Majibu basi Chadema itakosa uhalali wa kutuhumu ACT-Wazalendo na viongozi wake na hivyo wananchi wataendelea kujiunga na ACT-Wazalendo kwa kuamini kuwa maneno yoyote yanayotolewa na Chadema ni Ulaghai.

Karibuni kwa majibu Makamanda ili nasi tupate chakuwaambia wananchi ili waipuuze ACT-Wazalendo.

Huna nafasi hapa cdm kwani hakuna nafasi za watu wanamna yako,ndumila kuwili baki huko huko wafu na mizoga mzikane.
 
Team ccm please tuendelee kumpa support ya kutosha kijana wetu zzk
 
tatizo hamtapata akina shibuda, watakaokatwa ccm wataenda act na sio cdm kwani wameshaona wenzao kilichowapata huko. Kuna sura hata ukizipeleka appt au chausta zitashinda tu na ndo hizo zitaibeba act. Ila kama mnaamini hana madhara basi wacheni kumfuata kila anakopita muone cha mtemakuni.

ok mkuu. Vipi zitto amepata zile milion 700 toka kwa mamvi na ccm?
 
Tajiri amerudi toka Ujerumani??

Anaendeleaje? Maana nahisi amesimamisha mchakato ndani ya ccm mpaka arudi.
 
akiongea startv asubuhi amesema wataanza kusambaza uzalendo wiki ijayo kwa kufanya ziara kupita mikoa 14. stay tuned
mikoa au Miji? Mkoa wa Ruvuma una wilaya na majimbo kadhaa ya uchaguzi sasa ayatullah anazuru songea mjini anasema amezuru mkoa wa Ruvuma!
 
Hili ndiyo tatizo la pro CDM kulazimisha kila mtu afikiri kama wao, kwamba wao wasipomsikiliza ZZK watanzania wengine nao wabadilishe channel.

Tanzania inayokadiriwa kuwa na wapiga kura zaidi ya 24m, wafikiri kama pro CDM, really!!!!!

Kwa kuendelea kumfanyia promo zzk sasa hiyo channel yenu tutaisusa kama tbc na mawingu tv mtabaki kuonyesha mikutano ya ccm tu pale nyamagana
 
Kuna kipindi kinaendelea live star tv muda huu na mada ikiwa ni "kushuka kwa thamani ya shilingi".

Wageni waalikwa katika studio za star tv(wachambuzi) ni mchumi Donald Kasongi, akiwa anaongea katika studio za Mwanza na Zitto ambae atafuata kuongea akiwa studio za Dar-es-salaam.

Ni fursa nyingine kupima kauli za mwanasiasa huyu kwenye uchumi.

We acha tu, kasababisha nichelewe kunywa chai, uchumi wa nchi anaujua vizuri, juzi nilimsikiliza Mbatia yaani alikuwa anaongea pumba hadi roho ikaniuma eti waziri kivuli wa fedha hovyo kabisa. Zitto amekomaa kiuchumi, kuna mambo amenifungua macho, kuwa sasa uchumi wetu unategemea watalii mgodi wa Geita na mauzo ya viti vya plastic, ndo kilimo kifuate, hii ni habari mbaya kabisa kusikia.

Kushuka kwa kilimo cha pamba kwa 40% hii ni habari ya kushitua sana, wakati mjerumani alisema pamba ni white gold sie imegeuka laana. Japo mvua zinanyesha mashamba yote hayajalimwa, yale majembe ya kukokotwa na ng'ombe hayapo tena.

Pia amegusia kuwa upumbavu wa hawa jamaa kusema nchi hatatawalika kunaleta hofu kwa watu wenye mitaji yao.
 
Last edited by a moderator:
ukishathubutu kufanya hili /// KUIFUTA DHAMBI HII katika UMMA wa WATANZANIA NI /// VIGUMU SANA SANA ///YAANI UHARIBU NA KUHUJUMU HARAKATI ZOTE ZA MIAKA 15 /// KWA KITU KIDOGO
Adhabu yake aisubiri october ndio atazijua hasira za watanzania
 
mmeamka wote hata kusali hamwendi kisa zzk atawatoa kamasi
Uzi mlete nyinyi magamba na vibaraka wenu halafu hamtaki watu wachangie!Nyinyi mbona hamjaenda kusali mnaamka alfajiri kuleta thread za ayatullah hapa baada ya kuona yeye na kikundi chake cha act wasaliti hawajadiliwi tena hapa jukwaani.
 
Hili ndiyo tatizo la pro CDM kulazimisha kila mtu afikiri kama wao, kwamba wao wasipomsikiliza ZZK watanzania wengine nao wabadilishe channel.

Tanzania inayokadiriwa kuwa na wapiga kura zaidi ya 24m, wafikiri kama pro CDM, really!!!!!

Nimemsikiliza vizuri sana lkn hamna chochote kipya alichoongea pale
 
Na hakuna atakaye kulaumu kwa msimamo wako sababu ndo uwezo wako wa kufikiri ulipokomea. Udhaifu wa report ya PAC kuhusu sakata la escrow hauwezi kuhafifisha umakini wa ZZK katika masuala ya uchumi.

We kalaga baho!
Zzk hana umakini wowote ktk jambo la kimaendeleo,labda kuwazia jinsi ya kupiga ela za watanzania masikini.
 
Na hakuna atakaye kulaumu kwa msimamo wako sababu ndo uwezo wako wa kufikiri ulipokomea. Udhaifu wa report ya PAC kuhusu sakata la escrow hauwezi kuhafifisha umakini wa ZZK katika masuala ya uchumi.

We kalaga baho!
Zzk ni mchumia tumbo ndio maana akaanzisha ka vikoba kake kwa kupata kick ya ccm ili ashibe vizuri
 
Back
Top Bottom