JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,471
- 18,253
Hakuna jipya hapo,Sukuma,nyamwezi wa Tabora,Katavi,shy,Mwanza,au Mjita,mkulya,mzanaki wa Mara,ni vitu vile vile,ni Sawa na kusema Chaga,Pale,sambaa,wote ni wale wale,Huu mshituko nimeupata baada ya kuwa na project ya miezi 6 kwenye mikoa ya Morogoro na Katavi, kutokana na project hii nimekuja na mtazamo tofauti kabisa kuhusu kabila la wasukuma .
Mwanzoni nilijua wasukuma ni kabila la wavivu fulani waliojazana kanda ya ziwa tu kumbe siyo kweli kabisa. Nimegundua wasukuma aka akina Ngosha ni wachapakazi na wana umoja kupitiliza na wamejaa sehemu zote zenye fursa nchini!, nilipofika mkoa wa Morogoro kuanzia Ifakara hadi Malinyi madoni wenye maduka makubwa ni wasukuma na muda wote wanazungumza lugha ya Kisukuma tu.
Nilipoenda mkoa wa Katavi maeneo ya Mpimbwe kote huko madoni ni wasukuma wamekamata biashara zote kuanzia madukani hadi mashambani.
Nimegundua kuwachukia wasukuma ni kupoteza muda na kujitakia presha ya bure tu ,hamna namna utawashinda ,njia rahisi ni kuungana nao tu.
Kwa bongo,ishu ni jamii gani inamiriki uchumi?linaweza kuwa kabila kubwa,ila ndio choka mbaya hatari,unakuta middle class na njia zote za kiuchumi zimeshikwa na wakwe zangu wa Uchagani,