Mshahara gross laki 7 kwa mwezi, niukubali?

Hello wapendwa!

Samahani naomba tupeane elimu kidogo hapa. Nimepata kazi mahali fulani ambapo mshahara gross kwa mwezi ni laki saba lakini itanibidi nihamie Dar kwa ajili ya hiyo kazi.

Kwa sasa nafanya kazi mahali kama temporary na wananipa laki 4 ambayo haina Makato yoyote na pia nakaa nyumbani. Je wakuu huo mshahara ni fair kwa graduate au niikatae hiyo offer yao?

NB: Mkataba unasema nitakua napewa transport na airtime allowance kila wiki na baada ya probation ya miezi mitatu kuisha nitakua entitled to bonuses.

Wapi penye maslahi kati ya kuwa bank teller au police.
Addicted with majimama
Wewe mleta mada unazingua sana
 
Kuwa graduate sio sababu! inategemea umegraduate kwenye fani ipi!
Kuna kitu kinaitwa JOB EVALUATION, hapa maana yake ni kwamba inawezekana wote mkawa na shahada ya kwanza lakini wewe ni mwalimu na mwenzio na mhasibu.
Mnatofuatiana mishahara kwa kuwa wanafanya job evaluation. Job evaluation ni hatua ambayo kwanza unaorodhesha kazi zote za huyo mtumishi (job description). halafu kila kazi unaipa bei yake, mathalani kama ni mwalimu, unaweza kufanya hivi:
1. Kuaanda somo = 17,000/=
2. Kufundisha = 40,000/=
3. Kusahihisha = 46,000/=
Baada ya kufanya hivyo, kinachofuata sasa unajumlisha hizo bei za kila acitivity halafu unapata mshahara wa mtumishi huyo.
 
Sio lazima akija dar akae nyumba ya 100,000 kwani anakuja na familia?jamani hivi maisha ya kukaa nyumbani matamu eee aisee nimetoka home since Niko 18 na nime survive ukikaa home hutakaa ujue challenge za maisha lazima mtu ukomae ...dar ukitaka pawe pagumu patakua na ukitaka pawe parahisi pia patakua ...I'm not a graduate thou but nina experience na maisha ni bora ku face challenge za maisha ukiwa bado una nguvu kuliko ukiwa umri umesonga bora utoke nyumbani ujifunze maisha usiwe kupe sana bhana
 
ya dar usiende na ya bush achana nayo pia. kaz gan salary 400000? kaa home subir mwez huu utaitwa kaz salary 5,000,000. wanakupa nyumba,wanakupa 400,000 ya umeme na 200,000 ya maji kila mwezi,gari,mafuta na mke
 
Watu wanatafuta hadi laki 2,wewe una mbwela mbwela tuu.dar chuo kikuu utajiongeza uko uko.nenda
 
Bakia hapo kwa 400 soma channel za mshahara mkubwa kidogo ili kuendana na gharama za maisha ya sasa maana ukienda Dar hakika hiyo hela unaweza ishia kulipia bills mbalimbali na kula tena kwa kujinyima
 
mnaomshauri aje Dar...akija mtampokea!
Dar kuzuri ila changamoto ni nyingi huo mshashara haototosha kama hutajipanga vilivyo.
 
jf kuna vituko sana,watu wanamshauri huyu dogo eti asije Dar kisa laki 7 ndogo,ina maana hapo Dar kwenu kila mtu mshahara wake ni above 1m,mbona kuna mabank tellers wanapokea gross ya laki tano na wanaishi hapo hapo Dar?
Achen kutishana,Dar maisha ni ya kawaida kabisa ingawa kuna changamoto ndogo ndogo za hapa na pale.
 
Niliacha 650000 mkoan nimekuja dar kufata 600000 ni graduate kule nlikuwa afisa mikopo saivi huku pamoja na mshahar kupungua ila napata safari za mikoan kila kota salary loan nzuri tu.Maisha ni kuchagua nenda kweny laki7 hutajut
 
Back
Top Bottom