Mshahara gross laki 7 kwa mwezi, niukubali?

Matumizi na mahitaji hako si unayajua mwenyewe mkuu? Kuna mambo binafsi yasiyohitaji ushauri.
 
Sio graduate wewe..... km unashndwa kuchambua tofauti ya laki 4 na 7 kulingana na mazingira.....

Utaweza kuchambua iyo kazi unayotakiwa uifanye....


Kweli hawa graduates wa 2000's kazi kweli kweli....

Hivi ni swali la graduates hili kweli????

Haki ya MUNGU km ni graduates jiandae kula mvua jela... lazima ukaitoe loss kampuni.

Baki tu kwa mama hapo.
 
Mi nakushauri ubaki mkoani kwa hiyo laki nne ni hela kubwa sana kuliko laki 7 hapa dar, hiyo laki nne mkoani ukiamua kupanga unapata chumba kuzuri cha 25, umeme na maji mnashea, usafiri mkoani ni raha sana gari moja tu huku dar hata hilo moja ni tabu tupu, chakula dar ni tofauti na mkoani kama huwezi kula kipande cha pweza itakubidi ununue kuku wenye sumu tofauti na mkoani, unakula Takapojo (parachichi), ugali, samaki, mboga za majani, maharage vyote bei chee sio dar huku, mm sikushauri hapo mkuu
Jaman hamjajua yuko mkoa gani. Kuna mikoa ni nyoko.i.e mtwara. Ni bora aende dar tu
 
Acha Kuogopa Nenda Dar Kakomaze Akili Utakaa Kwenu Mpaka Lini? Kuamka Saa11 Alfajiri, Kukaa Kwenye Foleni, Kodi,umeme, Maji, Nyumbani Kwenu Wakusumbue Kidogo Maana Wanajua Umeshakuwa Boss, Upate Mwanamke Akuchune Kidogo Halafu Akusaliti Yaani Hapo Lazima Degree Ya Maisha Ya Mtaani Akili Ikomae Acha Uzoba Nenda Dar Kale Maisha Wewe! Kuna Koneksheni Na Wadau Kibao Woga Wako Ndio Umasikini Wako
 
Moja ya sifa ya usomi ni uwezo wa kufanya maamuzi, not everything you encounter you come here for advise.
 
Nenda dar wewe acha kuishi kwa wazazi nche ya kazi dar kunafursa kibao za biashara
 
hello wapendwa!
samahani naomba tupeane elimu kidogo hapa,nimepata kazi mahali flani ambapo mshahara gross kwa mwezi ni laki Saba lkn itanibidi nihamie Dar kwa ajili ya hiyo kazi..kwa sasa nafanya kazi mahali kama temporary na wananipa laki 4 ambayo haina Makato yoyote na pia nakaa nyumbani.so wakuu huo mshahara ni fair kwa graduate au niikatae hiyo offer Yao?
NB:mkataba unasema nitakua napewa transport na air time allowance kila week na baada ya probation ya miezi mitatu kuisha nitakua entitled to bonuses.


Kataa hii ofer ya Dar ya laki 7.....hii kazi haikufai hata kidogo. kaa tu nyumbani kwa wazazi. By the way, hii kampuni ya Dar inaitwaje? Una namba yao ya simu? Ni PM niwasalimie nina tenda nataka niwapelekee.
 
Mimi nimekaa dar nalipwa hiyo laki nne na ikikatwa inabaki laki tatu na visenti. nasomesha private shool na nalea. sembuse ww wa laki saba. acha uoga toka home. kama vipi kabla hujaondoka kwenye hicho kibarua hebu niunganishe mkuu
 
Back
Top Bottom