Mshahara wangu kwa mwezi ni 250,000/=. Kupangilia mtihani

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
175
618
Jamani!!!!

Ndugu jamaa na marafiki aka ndo kamshahara kangu ka mwezi! Kukapangilia sasa mtihani kwani nikienda bank naivuta yote naacha 5000 tu ambayo haitoki nayo ingekuwa inatoka wallahi ningeivuta niache 0% jamani ela ndogo, hii pesa haitoshi nikinunua chakula cha mwezi nabaki empty kabisaaaaa!

Naishiwa, kiasi kwamba ata ela ya kununua mboga zile zinazozungushwa sina. Matumizi yanakuaga kama ifutavyo; pango chumba 5000 ni kota, umeme 5000 natoa kwa mwezi, maji 4000 kwa mwezi, nilijitahidi kununua jiko la gesi ivyo situmiagi mkaa labda siku nikitaka kubandika maharagwe, lakini safari hii hata ela ya mkaa sina ivyo maharagwe sipiki kabisa labda nita bajeti mwezi ujao kwenye swala la mkaa, vyakula kwa mwezi ni kama ifuatavyo; viazi mviringo ndoo ndogo moja 12000/= mafuta galoni lita tatu 18000/= mayai tray moja 11000 mwazo ilikuwa 10000 saizi 11000 napenda sana mayai ya kuchemsha ivyo kwenye budget siwezi acha mayai,

Sukari kilo tatu 9000/= nanunuaga ya paketi kwaiyo paketi 3, maharagwe nachukuaga kilo 2 na kilo moja ni sh 2800 x 2/= unga wa ngano kilo 1@ 1200, na ninanunuaga kilo 5, sabuni dofu pact 5 paketi 1@ 1200/= mchele kilo 3, super geti 1@1500, vitunguu nanunua vya sh 3000/= chumvi sinunuagi mara kwa Mara nikinunua ya 500/= inaweza kaa miez ata miwili mitatu situmii sana chumvi, safari hii nikasuka nywele za sh 50000/= kichwa kilikuwa lafu sana. Lakini miezi ilopita nilikuwa sisuki nilikuwa nanyoa tu kupunguza gharama za kusukia.

Hapo bado sijaombwa ombwa tu ela na madogo jamani Mimi Niko empty sina ela na ninaishia kula chips tu na wali. Mboga sina, ela mfukoni haisomi siwezi kula ugali bila mboga nyanya nazo sina nilinunua za 2000 zimeisha na nikinunua nyingi zinaoza. Na hii ni ratiba yangu ya kila mwezi haibadiliki!!! Naifata kama ilivyo, mana bora ununue vitu vya mwezi kuliko kila siku kwenda dukani pesa haikai ndani unaweza pata shida ukalala njaa.

Kwakweli maisha ya laki mbili na nusu magumu sana kwangu sijui mshahara kuanzia laki ngapi utakuwa unanitosha ela inaishia kula tu hamna cha maana ninachofanya kwenye hii ela. Kwakweli unaweza ona kama kazi yenyewe haikupi faida ya Ku invest more!!!! Unaishia kula tu.

Kama kuna yeyote anaweza nipangia hii ratiba kwa ela hii nitashukuru lakini mayai usiyatoe kwenye ratiba na vyakula ninavyopendelea ni kama ifutavyo naona vipo ndani ya mahitaji hayo niliyoorodhesha hapo juu chips, wali, ugali nakula lakini mboga za majani kwangu mtihani kidogo samaki siwapendi labda dagaa mchanga (kigoma), napendelea mchicha, matembele sio mpenzi mboga ya maboga labda nitie karanga au nifanye mchemsho niweke chumvi na nyanya tu nichanganye na mchicha kidogo, chainisi ya kuunga tu kwa nyanya na kitunguu sipendelei labda niitie karanga, maharagwe napenda lakini nitie nyanya yasipokuwa na nyanya hamu ya ugali haipo, kabeji napenda lakini kwenye wali, sio kwenye ugali, na kama nikiitumia kabeji kwenye ugali labda kabeji ichanganywe na nyama the same kwenye chaina nikikosa karanga nichanganye kwenye nyama.

Asanteni...
 
Kama wewe ni ke inaweza isiwe shida sana kama ilivyo kwa me, tatizo lenu mkiwa pisi kali mnakuwa na wenge sana, full drama, mapozi debe, maringo kibao nk.
Sasa mtu anaeleza habari za budget wewe hizo za wenge na maringo umetoka nazo wapi ndugu yangu..? Ama ndiyo zinatumia pesa yake vibaya?

Si ungemshauri tu kuhusiana na hiyo 'budget' yake kisha mambo yake mengine ukamuachia mwenyewe?
 
Mafuta lita 3 kwa mwezi?

Sukari kg 3 ? Kwa mwez ? Unameza sukari?

Nywele za 50k ? Kisa nin?
Simply una matumizi mabaya ya pesa
My dear Mimi Sukari, kilo 3 inaisha coz unga wa ngano nauchezea sana. Hapo nitapika maandazi, mara cake, mara chapati za maji. Mafuta nitakaanga chips, sijui bisi. Mara nikaange karanga, kwangu ndo vitu ambavyo natumia sana mafuta & sukari. Chai hata sijazagi kikombe, mi sio mpenzi wa chai labda uji. Uji wangu napenda uwe na sukari nyingi.
 
My dear mimi sukari kilo 3 inaisha coz unga wa ngano nauchezea sana hapo nitapika maandaz,Mara cake,Mara chapati za maji ,mafuta nitakaanga chips,sijui bisi,Mara nikaange Karanga,kwangu ndo vitu ambavyo natumia sana mafuta & sukari.chai hata sijazagi kikombe mi sio mpenzi wa chai labda uji,uji wangu napenda uwe na sukari nyingi.
Ndio maana tumesema una matumizi mabaya
 
Back
Top Bottom