Msemaji Mkuu wa Serikali anazungumza na Wanahabari leo Juni 12, 2022 Jijini Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,840
12,043
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Serikali katika mkutano na waandishi wa habari leo Juni 12, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO, Dodoma.



Msigwa.jpg


MSIGWA: ASKARI ALIYEFARIKI ALICHOMWA MSHALE KICHWANI
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa askari ambaye alifariki Wilayani Ngorongoro katika eneo la Loliondo alifariki kwa kuchomwa mshale kichwani.

“Serikali inasisitiza kuwa hakuna askari aliyeenda kumfukuza Mkazi wa Loliondo kuondoka eneo lake. Eneo lina kilometa za mraba 4000, kwa makubaliano na wananchi tulitenga kilometa za mraba 2500 zitumiwe na Wananchi na 1500 zibaki kuwa hifadhi na wanachofanya maafisa ni kuweka alama za eneo la hifadhi,” – Msigwa.
 
Back
Top Bottom