Msekwa awa Makamu CCM!

bado ni kitendawili, kwani Makamba akirudi itakua ni aibu nyingine. Aliyoyafanya Tanga na Maswa yanatosha kumsimamisha na wala si kumbadilisha
 
Nafikiri Mzee Msekwa anastahili pongezi kwa hii nafasi halikadhalika kwa CMM pia maana huyu mzee ana kichwa kizuri na ni kweli atakisaidia chama katika kutoa majibu yenye akili kwenye hoja za wapinzania.

Kwa kumbukumbu zangu Mrs Msekwa ndiye mwenyekiti wa UWT! Na UWT ni moja ya vyombo muhimu vya CCM. Nini inaweza kuwa impact ya hili?
 
Kama ni kweli ndugu Maggid nasema asante kwa habari hizi. Ila nauliza kama ndiyo demokrasia hii kwamba awe mgombea pekee.Hapakuwa na wengine walio taka nafasi hizo ama Katiba inasema apendekezwe mmoja ?

Huenda haya ndio yale maandalizi ya kura za itifaki ambazo zimekuwa zikiwaumiza wagombea wa sisiemu mara nyingi.
 
Sad thing about this on Malecela is that he was never open to public if he was going to step down or not. This now sounds like demotion due to the fact that he was associated with other "wataka umakamu"!

Mzee wetu ataingia katika historia kama mtu aliyecheza Patapotea na akadhihakiwa!
Hata mimi nampa pole, ila angejifunza toka kwa mzee mwenzie, mhe Ndejembi aliyekuwa menyekiti wa sisiemu mkoa wa Dodoma. Mzee huyu aling'atuka na kutoa wosia kwa wazee wenzake kung'atuka. Malecela angefanya hivi nadhani angevuna heshima kubwa sana nani ya nchi. Funzo hili limfikie babu Kingunge pia.
 
Je, Msekwa atakuwa tayari kuhakikisha makundi ndani ya CCM yanavunjwa na pia kupambana na ufisadi, ula rushwa, mikataba mibovu na viongozi wanaojilimbikia mali ili kurudisha credibility ya CCM inayozidi kuanguka kila kukicha!?

1. kuvunja makundi ndani ya CCM
2. kupambana na ufisadi
3. mikataba mibovu
4. ula rushwa
5. viongozi walimbikiza mali

Sina hakika kama haya yote yamo katika 'work description' ya makamu mwenyekiti.

Pengine yote haya dereva mkuu ndio mhusika; bila yeye kuyavalia njuga hakuna litakalofanyika kuleta mabadiliko katika chama hiki kinachozidi kudidimia.
 
Jamani, pia Msekwa ndiye aliyekua Mwenyekiti wa Uchaguzi wa CCM kama alivyo Sitta katika uchaguzi huu wa kesho, na hivyo, anajua siri nyingi sana. Bado ni gogo. CCM pamoja na tofauti zao, WALINDA SIRI WAO HUWA WANAWALINDA SANA
 
bado ni kitendawili, kwani Makamba akirudi itakua ni aibu nyingine. Aliyoyafanya Tanga na Maswa yanatosha kumsimamisha na wala si kumbadilisha

Na aliyoyafanya Zenji mpaka CUF wakang'aka je? Ushayasahau? Sema saa mzee huyu ana ngekewa, akitolewa ukatibu mkuu ujue kuna mahali atawekwa tu, sisiemu haimtupi huyu!
We ngoja usikie tu.
 
...chaguzi kama hizi za mafisadi tuwaachie kina Kada na mwenzake Mwiba.
 
Msekwa ni most dikiteta.Ujue huyu Mzee ana majibu machafu sana na kumbuka kwamba huyu Mzee alifanya Bunge kuwa mali yake.Kumbukeni maamuzi yake .Msekwa kwake CCM kwanza na Tanzania nyuma. Connection ya RA naiona kwa kiasi kikubwa sana nina wasi wasi .

Kumbe Makamu wa CCM anakuwa picked not voted for ?

Malecela nilijua taanguka vibaya .Sasa kazi ya kupanga wizi wa kura na mikakati michafu anaichukua Msekwa na kama Nchimbi atalamba dume basi tegemeeni siasa chafu na za mabavu na makundi than ever .
 
Halisi, kwani Mwanri si amejitahidi, kwani jinsi ninavyomuona Mwanri anaweza kuuvaa Ukatibu Mkuu na hivyo Nape anaweza kuwa mwenezi. Lakini Makamba atakwenda wapi?

Makamba atakuwa mbunge tu wa kuteuliwa na mjumbe wa NEC,hivyo 2010 atapoteza Ubunge na ndio utakuwa mwisho wake kisiasa.kuna jamboa liharibu yeye na Lowassa na Muungwana hakupendezwa nalo,hasa suala la Tanga na wale Wabunge wa Arusha,
ila atakuwa akisaidiana na kina hizza kupika majungu
 
Msekwa ni most dikiteta.Ujue huyu Mzee ana majibu machafu sana na kumbuka kwamba huyu Mzee alifanya Bunge kuwa mali yake.Kumbukeni maamuzi yake .Msekwa kwake CCM kwanza na Tanzania nyuma. Connection ya RA naiona kwa kiasi kikubwa sana nina wasi wasi .

Kumbe Makamu wa CCM anakuwa picked not voted for ?

Malecela nilijua taanguka vibaya .Sasa kazi ya kupanga wizi wa kura na mikakati michafu anaichukua Msekwa na kama Nchimbi atalamba dume basi tegemeeni siasa chafu na za mabavu na makundi than ever .
hizi ni mbinu za rostam,Msekwa na Lowassa ni wamoja na wote ni mtandao maslahi,ila siri hii inafichwa sababu kuna baadhi ya watu wa mtandao walikuwa hawamtaki Msekwa,ila Msekwa naye ni mtandao per see

ila CCM bila Malecela,sijui nani atawasaidia kukomboa majimbo,Mnyika jiandae kukamata Ubungo,
Nchimbi kupewa Ukatibu mkuu itakuwa kama kuharalisha vita kati ya Membe na Lowassa.
 
hakuna jipya hapo,kinachofanyika ni kuongeza kundi la mafisadi ili kujijengea ngome imara ktk mtandao.
kipi kikubwa alichofanya msekwa ktk utumishi wake ambao hata leo mtu unaweza kusimama mbele ya umma na kumwagia sifa bwana msekwa zaidi ya kubadilisha wake.
 
Msekwa ni most dikiteta.Ujue huyu Mzee ana majibu machafu sana na kumbuka kwamba huyu Mzee alifanya Bunge kuwa mali yake.Kumbukeni maamuzi yake .Msekwa kwake CCM kwanza na Tanzania nyuma. Connection ya RA naiona kwa kiasi kikubwa sana nina wasi wasi .

Kumbe Makamu wa CCM anakuwa picked not voted for ?

Malecela nilijua taanguka vibaya .Sasa kazi ya kupanga wizi wa kura na mikakati michafu anaichukua Msekwa na kama Nchimbi atalamba dume basi tegemeeni siasa chafu na za mabavu na makundi than ever .

Well said Lunyungu,

Mtandao unazidi kujizatiti. I feel sorry for Malecela
 
nilishasema subiri kuiona CCM ya zamani ikirudi ! tena na bado, subirini mtakayosikia kesho na keshokutwa Mungu akipenda !

strong and at its best !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom