Msekwa awa Makamu CCM!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
Hivi punde tu, PIUS Msekwa amependekezwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti, CCM. Hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ndani ya CCM. Kwa habari zaidi katika picha, tembelea: http://mjengwa.blogspot.com
 

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,349
2,000
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,874
2,000
Kama ni kweli ndugu Maggid nasema asante kwa habari hizi. Ila nauliza kama ndiyo demokrasia hii kwamba awe mgombea pekee.Hapakuwa na wengine walio taka nafasi hizo ama Katiba inasema apendekezwe mmoja ?
 

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,698
1,225
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!

Kitila,

Kwa wakati huu, CCM walikuwa wanahitaji kiongozi makini, sio mpiga Debe, wananchi siku hizo wanayaona na kuyasikia wenyewe kwenye vyombo vya Habari, hawahitaji mpiga debe mwingine...

Nadhani pia CCM itafaidika kutoka kwa Msekwa kwa kuweza kudumisha demokrasia ndani ya chama chao,,, maana mtu ambaye amekuwa bungeni kwa miaka yote,,, nadhani hatapenda majungu sana...

Lakini la muhimu tunahitaji demokrasia idumu vizuri pia kwenye vyama vingine vya siasa sidhani huyu mzee atakuwa mtu mbaya...

Kwangu mimi naona ni BEST kutoka kwa wote waliotajwa... ingawa JF inaweza kuja na kashifa zake,,, lakini at least hatukuzisikia kashifa hizo tangu aastaahafu...

Dalili ni kwamba baada ya mkutano mkuu,,, pia katibu mkuu atakuwa mtu mzuri,,, maana Mwenyekiti,na Makamu wake wawili ndio hao watakao pendekeza katibu mkuu!!!
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,528
2,000
Sad thing about this on Malecela is that he was never open to public if he was going to step down or not. This now sounds like demotion due to the fact that he was associated with other "wataka umakamu"!

Mzee wetu ataingia katika historia kama mtu aliyecheza Patapotea na akadhihakiwa!
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
Nafikiri ni uchaguzi mzuri. Isingeliwezekana Lowassa kuwa makamu Mwenyekiti wa CCM na huku ni PM.

Hongera Msekwa, baada ya kutemwa Uspika sasa umepata nafasi nyingine.
 

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,164
1,225
Anastahili pongezi, ila naona kama ni kugawana na kuleta balance ndani ya chama, Mwenyekiti = mtandao, makamu sio mtandao.

safi kiaina!
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Nadhani, pamoja na KIBURI chake, Msekwa ni kiongozi mzuri, hasa ukizingatia amefanya kazi nyingi sana ndani ya chama tawala kwa miaka mingi na anakijua sana. Pamoja na hayo si mwanamtandao jambo ambalo JK alilitaka. JK alitaka majina, akapelekewa, Mangula, Sumaye na Msekwa, lakini yeye na watu wake walikua wakimwangalia zaidi Msekwa kama chaguo sahihi. Mangula walimuona kama mtu aliyekaa muda mrefu CCM kama kiongozi wa juu na hivyo anastahili kupumzika. Sumaye walimuona kama mtu HATARI kwani pamoja na kukana, bado anaweza KUUTAKA URAIS hapo baadaye, jambo ambalo badi si jema sana kwa wanatandao maslahi. Msekwa anatajwa kuwa karibu na Rostam Aziz, kama mtakumbuka kupitia VODACOM kama Mwenyekiti wa Bodi. VODACOM ndiko alikokua pia Mkurugenzi Mpya wa TANESCO, Idriss RAshid. KUNA SIRI KUBWA HAPO BADO
 

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,244
2,000
Kwa Msekwa kupendekezwa, inaweza kuwasaidia sana ccm kujibu hoja za wapinzani zinazoibuliwa kila kukicha. Binafsi namkubali kwamba anafaa kwenye hiyo nafasi
 

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!


Anaweza kuifanya CCM system iwe sensible kidogo...

Kwa mtaji huu Katibu Mkuu huenda akawa mtu very bogus kama E. Nchimbi.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,273
2,000
Nadhani ni malipo ya "nidhamu yake ya Chama". Licha ya kubwagwa vibaya kwenye kitu cha Uspika na kutopata ulaji mwingine mkubwa Msekwa amekuwa kimya. Bila ya shaka utii katika chama unalipa na natumaini ataleta kile kinachotamaniwa na wana CCM - whatever that is.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,826
2,000
Je, Msekwa atakuwa tayari kuhakikisha makundi ndani ya CCM yanavunjwa na pia kupambana na ufisadi, ula rushwa, mikataba mibovu na viongozi wanaojilimbikia mali ili kurudisha credibility ya CCM inayozidi kuanguka kila kukicha!?
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Anaweza kuifanya CCM system iwe sensible kidogo...

Kwa mtaji huu Katibu Mkuu huenda akawa mtu very bogus kama E. Nchimbi.

Hivi sasa Nchimbi atakua K.Mkuu ataachia UWAZIRI?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,273
2,000
Kama atapewa Ukatibu Mkuu, basi kwenye mabadiliko yajayo sitashangaa atatemwa. Ila itakuwa ni wrong choice.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Upo uwezekano wa kuwa NApe Moses NNAUYE kuwa Katibu Mwenezi... Kwa mwenye nyeti atupe....
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,273
2,000
Halisi, kwani Mwanri si amejitahidi, kwani jinsi ninavyomuona Mwanri anaweza kuuvaa Ukatibu Mkuu na hivyo Nape anaweza kuwa mwenezi. Lakini Makamba atakwenda wapi?
 

Zanaki

JF-Expert Member
Sep 1, 2006
545
195
Habari za hapa na pale ni kuwa Msekwa kapendekezwa na Mwenyekiti kushika kiti cha Malecela
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom