Msanii Soggy Doggy ajiunga CHADEMA

Msanii Soggy Doggy ajiunga CHADEMA

Yani ajiunge leo na atake ubunge? sio kuleta mtafaruku chamani kweli? Je aliogombea 2010 wakakosa watamuelewaje?

Kwanini asikae kwenye chama kwa muda hata wa miaka 15 tumjue ka kweli amevua gamba?
 
kaa kajiunga kundeleza mpambano wa kuwaelimisha vijana mabadiliko sawa
ila kama kajiunga ili awe mbunge hiyo nadhani chadema muwe makini
 
Ritz; Uroho umekujaa, kwani angehamia CCM ungesema amefulia kwenye music ndipo amehamia CCM? Kina Komba,Nakaaya Sumari na Vicky Kamatta wao bado wapo kwenye chat kimuziki?
 
Last edited by a moderator:
karibu sana Anselem Tryphone Ngaiza 'Soggy Doggy Anter' kwenye harakati za kumkomboa MTanzania kutoka kwenye udhalimu wa wenye dola..
 
Hahaha hana influance sitashangaa lakini ni aina ya chadema kuwa na viongozi kama kiina afande sele na sugu hahahha
 
kama Mpendazoe nae ataamua kugombea itakuwa ni mpambano mkali, yeyote atakayepita sawa bora jimbo liende Chadema.
safi Soggy maamuzi mazuri hayo.
 
Mliwabeza sana wasanii wakati wanazuunguka na CCM kwenye mikutano na kampenizao leo hii mmeona ni wa muhimu. Kweli naamini ccm ndio baba wa demokrasia na mfano wa kuigwa ktk siasa.
 
chama cha wasanii naa wahuni..... mijitu ikimeza maji ya chama bana ata shetani akijiunga nao atapongezwa, owh lkn kumbe tayari shetani amejiunga nao
 
Hivi ndivyo alivyo funguka Twitter na Facebook"Shikamoo Mbunge wa Segerea Bwana Makongoro Mahanga,imetosha sasa nadhani ni zamu yangu kuwatumikia wana-Segerea 2015 kupitia CHADEMA"
View attachment 99314

HONGERA sana msanii Soggy, ila sasa jitayarishe kuanza kupikiwa mizengwe na hao wapinzani wako wa kwenye SIASA
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Soggy Doggy huyuhuyu aliyekuwa mtangazaji wa Radio UHURU ya LUMUMBA? CCM mchukulie haya matukio ya vijana kujiunga na vyama vya upinzani kama changamoto kuu hii dhahiri inaonyesha kuwa chama chenu kinaendelea kukosa mvuto kwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya nchi kwa kila sekta.
 
Sasa nimeamini serikali itakayoingia madarakani 2015 ni serikali itakayoongozwa na Vijana!
 
Pamoja na kwamba ninapenda mabadiliko, lakini hii sio sahihi na siafiki. Umaarufu sio uongozi. Huyu Soggy hivi bungeni ataenda kufanya nini? Jamani, ebu tuwe wakweli; hivi tunamuweka kwenye mizani gani tukimsoma Soggy kupitia kwenye ujumbe wa nyimbo zake? Kweli ana uwezo wa kuchambua masuala mtambuka yanayoikabili nchi?


CHADEMA, ni heri kuliacha jimbo kwa CCM (kama kuna mgombea bora) kama kuliko kupoteza nguvu na fedha kwa mtu ambaye sio sahihi.
 
Baada ya kufulia kwenye music wanakimbilia kwenye siasa.


Kumbe wabunge wa CCM walifulia kwanza ndiyo wakaja kwenye SIASA ili kuchumia matumbo, sasa umetupa jibu zuri kwanini hawa watawala wetu wanashindwa kutimiza na kusimamia wajibu wao.
 
Pamoja na kwamba ninapenda mabadiliko, lakini hii sio sahihi na siafiki. Umaarufu sio uongozi. Huyu Soggy hivi bungeni ataenda kufanya nini? Jamani, ebu tuwe wakweli; hivi tunamuweka kwenye mizani gani tukimsoma Soggy kupitia kwenye ujumbe wa nyimbo zake? Kweli ana uwezo wa kuchambua masuala mtambuka yanayoikabili nchi?


CHADEMA, ni heri kuliacha jimbo kwa CCM (kama kuna mgombea bora) kama kuliko kupoteza nguvu na fedha kwa mtu ambaye sio sahihi.

Kwani huyo MAKONGORO alishawahi kufanya nini, waache wananchi wataamua wenyewe???
 
Back
Top Bottom