Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,626
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa declaration of Interest

Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wachache waliowahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa maandiko yangu, ya kulituhumu Bunge kujipendekeza kwa serikali, hivyo inaweza kuonekana nafurahia kinachompata Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai!. No!. Huyu ni Mkuu wa Mhimili wa Bunge wenye jukumu la kuisimamia serikali, haitakiwa Spika kujipendekeza kwa Executive, inambidi Mkuu wa Executive amuogope na kumheshimu Mkuu wa Bunge na Mahakama, siungi mkono jinsi Job Ndugai alivyodhalilishwa vile pale juzi.

Hili ni bandiko la kupinga ubatili unaendelea katika hili sakata la Spika. Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, kwanza niliuliza, Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kisha nikauzungumzia msamaha batilifu, Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu! ambao ulikataliwa, na mara baada ya msamaha huo kukataliwa nikauliza tena Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Jana barua hii ya taarifa kwa umma toka kwa Spika kuwa ameandika barua ya kujiuzulu uspika

Barua batilifu .jpeg

imesambaa kote. Kama ni kweli hii ndio barua ya Spika Job Ndugai kuuarifu umma kuwa ameandika barua ya kujiuzulu uspika, na kuipeleka kwa Katibu Mkuu wa CCM, kiukweli this looks fake!, ila kama sio fake, then tumsamehe bure Mhe. Job Ndugai, huku kutakuwa ni kutokana na kuchanganyikiwa tuu, barua hii nayo ni barua batilifu!, kwasababu kujiuzulu kwake kumekuwa addressed to a wrong person and to a wrong Institution. Bunge ni mhimili, Mkuu wa mhimili wa Bunge hawezi kujiuzulu kwa barua batilifu na tukaacha tuu hivi hivi, what precedence tunaweka for records?

Nashauri barua hii ikataliwe, Spika aandike a proper letter ya kujiuzulu kwenye a proper Bunge letterhead kama hii

A proper bunge letter head.png


Nakiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili baada ya kumsoma mwana je huyu
Nilifikiri barua ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai angeandikiwa Katibu wa bunge na nakala kupelekwa kwa Katibu mkuu wa CCM na siyo kinyume chake

Pascal Mayalla nipe uzoefu wako Tafadhali
Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist
it's true Job kachemsha!, barua ya kujiuzulu uspika ilipaswa kupelekwa kwa katibu wa Bunge, CCM ndio wanapewa copy. Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa Bunge la CCM. Usika wake ni kwa mujibu wa katiba, na kujiuzulu pia kumeelekezwa na katiba anaandika barua kwa nani, na sio kwa CCM!

CCM ilimpendekeza tuu, baada ya kuchaguliwa, anakuwa ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM!, hivyo hata kujiuzulu, anajiuzulu kwa kumuandikia Katibu wa Bunge na sio Katibu wa CCM! Kama Spika wa Bunge anayepaswa kuijua katiba na kuifuata, anaweza kujiuzulu kwa barua ya kienyeji namna hii, then this is a disgrace kwa nafasi ya Spika!

Huu sio utaratibu wa kufuata wakati wa kujiuzulu kwa Spika wa Bunge. Ingekuwa anajiuzulu kwa kujivua uanachama wa CCM hivyo kupoteza uSpika hapo ndipo anapeleka barua ya kujiuzulu kwenye chama chake, hata angekuwa amejiuzulu ubunge, barua ya kujiuzulu inakuwa addressed kwa Spika wa Bunge. Japo chama ndicho kimemdhamini kugombea ubunge, na uspika lakini baada ya kuchaguliwa mbunge au Spika, umechaguliwa na Watanzania/Bunge la JMT, unawajibika kwa Bunge na sio kwa chama chako.

Kikatiba, Spika wa Bunge akijiuzulu anatakiwa kufanya kutumia Ibara ya 149(1)(c) ya Katiba ya JMT inayosema iwapo Spika wa Bunge atajiuzulu, basi taarifa ya kujiuzulu aliyoiandika na kuitia sahihi yake ataiwasilisha kwenye Bunge.

Inakuwaje anaipeleka kwenye chama na Bunge lipokee nakala kutoka kwenye chama? . Msameheni bure tuu, Spika atakuwa amechanganyikiwa, maada kwa jinsi alivyokuwa anauringia na kuutambia, "mimi ni mhimili" halafu ghafla unatakiwa kuutema uspika, hata ningekuwa mimi, lazima mtu uchanganyikiwe!

Naendelea kusisitiza Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Bunge ni mhimili, Spika anapatikana kwa mujibu wa katiba, na akijiuzulu pia anajiuzulu kwa mujibu wa katiba, hawezi kujiuzulu tuu hivi kienyeji enyeji kwa ubatili na kukubaliwa, hata kama ni kujiuzulu, then ajiuzulu kwa mujibu wa katiba, kama kifungu hiki kilivyoeleza
johnthebaptist tuangalie kifungu 149 Kifungu (1) Kifungu kidogo(a)
Kifungu.jpeg
Mkuu Ukwaju thanks kwa kifungu hicho.

Hii tabia ya kuacha na kupuuzia mambo madogo madogo haya ya ubatili, it is now unbecoming, kuna siku tutajikuta tunatengeneza taifa la ubatili. Kama Katiba ndio sheria mama, na imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, there is no options and no negotiations katiba ifuatwe ajiuzulu properly kwa mujibu wa katiba na kujulia mafao yake manene ya 80% ya mshahara na marupurupu ya Spika.

Nakutakia Kustaafu Kwema, ndugu yangu na rafiki yangu, Job Ndugai.
Paskali
 
Wanabodi,

Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, ambao ulikataliwa...

Hii hoja ina mashiko sana.

Ni kweli CCM ndio waliomdhamini Job kugombea uspika na angeweza kushindwa kama wabunge wasingempa kura zao, na uhalali wa kuwa spika ulitokana na kura za wabunge (bila kujali wingi wa chama wanachotoka) na aliposhinda kwa kura alikula kiapo mbele za bunge kuwa spika wa bunge JMT.

Kaka mkubwa Paskali, hoja yako ina mashiko.

Maji yashamwagika, ila administratively iko haja ya ku-set a good precedence.
 
Ameshalimaliza hilo, anaendelea na mishe nyingine, anamsubiri kiherehere mwingine....
Kabisa, Job hakukusudia kushauri juu ya mikopo. Job amechukizwa na utaratibu mzuri wa matumizi sahihi ya mkopo wa 1.3T, na asingependa style hiyo ifanyike tena kwani ni miongoni mwa wanaotaka mama asikamilishe hata mradi mmoja. Samia amefanya sahihi saaana.
 
Wanabodi,

Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, ambao ulikataliwa.
Paskali,
Mtu yeyote anayejiamini kupita kiasi kwa vile ana fedha, nguvu au madaraka hufanya maamuzi ya ovyo mara zote.

CCM ni chama kinachoamini katika hayo yote hapo juu. Kwa imani yangu naamini Job hajaandika ile barua bali amepelekewa tu asaini na yeye kwa vile yuko depressed akasaini content bila hata kujiridhisha addressee ni nani. Sidhani kama Job ni mbumbumbu wa kanuni kiasi cha kutoelewa alitakiwa kwanza amwambie nani kwamba anajiuzulu.

Kuthibitisha kauli yangu, ni kitendo cha Chongolo (KM CCM) kuthibitisha kupokea barua na yeye kukiuka Katiba zaidi na kumwandikia Katibu wa Bunge barua ya kumjulisha kujiuzulu kwa Spika. Huu utaratibu kausoma kwenye Katiba ipi? Kautoa kanuni gani?
 
Hii serikali ina mambo mengi ,ukute ata ndugai kaletewa barua ma makachero wa ccm asaini uku ameshikiliwa AK47 achague moja uhai au risasi. Na ndo hao hao waliopeleka barua sehemu ambayo sio sahihi sababu hawajui utaratibu maana ndani ya ccm vichwa maji ni wengi....natania tuu.
 
Hii serikali ina mambo mengi ,ukute ata ndugai kaletewa barua ma makachero wa ccm asaini uku ameshikiliwa AK47 achague moja uhai au risasi. Na ndo hao hao waliopeleka barua sehemu ambayo sio sahihi sababu hawajui utaratibu maana ndani ya ccm vichwa maji ni wengi....natania tuu.
Hahahahahah hamna cha AK47 wala nini ni just tu aidha uachie madaraka kwa aibu zaidi ya kuvuliwa uwanachama na impeachment hata mie ninge opt kujiuzulu tu rather ya kuaibishwa zaidi.

Maana raisi akitangaza kakuvua uwanachama unapoteza ubunge straight away na sifa ya kuwa speaker inafutika on the Spot. Ni aibu kiasi gani yani😅

Namkumbuka Nyerere aliposema kuwa katiba yetu ni nzuri ila akitokea raisi kichaa katiba hii yaweza kuwa chungu balaa maana imempa raisi uungu mtu. Raisi ana madaraka mengi mno kiasi cha kuweza kupindua meza atakavyo na hakuna kitu mtamfanya.

Kwa yaliotokea na yanayoendelea kutokea nchini katika kipindi cha miezi 12 tu ni ushahidi thabiti kuwa tunahitaji kufanya reform ya katiba mpya. Ndugai pole yake ila mwisho wa ubaya ni aibu na dawa ya kiburi ni jeuri.

Heko mama Samia kwa kumuonjesha Ndugai a taste of his own flesh!😅 ndio aelewe kuwa alipokuwa anaumiza wenzie kwa cheo chake na dhamana kwa kiburi walijiskiaje. Kazi nzuri sana mama amefanya for 2022!
 
Wanabodi,

Baada ya Spika wetu Job Ndugai kutoa yale matamshi ya ukweli ya kizalendo kwa taifa letu kuhusu mikopo na deni la taifa, halafu akaja kuikana kauli yake na kuomba msamaha batilifu, ambao ulikataliwa...
Tunaposema KATIBA MPYA Yenye maudhui ya kitaifa na uwajibikaji ina maana sana. Sio katiba ya wapinzani.
Wapinzani walinyanyapaliwa sana sasa hawako bungeni kuchangia ona wameanza kurudiana wenyewe!
Katiba katiba ndio suluhisho.

Kusingizia kumezidi, hatuna.magaidi ila waropokaji wako.
Tanesco Tanesco mnatufanyia nini??
 
Back
Top Bottom