Msako wa mifuko ya Plastiki kuanza upya Dar es salaam

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametangaza operesheni ya kukamata mifuko ya plastic iliyokatazwa huku akiwataka wananchi kujiepusha na matumizi ya mifuko hiyo.

RC Makalla ametangaza operesheni hiyo leo Ijumaa Augusti 19, 2022 wakati wa kikao kazi na wazalishaji wa mifuko mbadala, kamati ya ulinzi na usalama na mamlaka za udhibiti ikiwemo TBS na NEMC baada ya kubaini mifuko iliyokatazwa inaendelea kutumika.

Aidha Makalla ameagiza kuitishwa kikao cha wenyeviti wa masoko yote ya mkoa huo na kutolewa maelekezo ya katazo la uuzaji wa mifuko hiyo masokoni.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa mkoa ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kurudi upya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya matumizi ya mifuko hiyo.

Makalla ametaja madhara ya matumizi ya mifuko hiyo ni uchafuzi wa mazingira, ukwepaji wa kodi kutokana na mifuko hiyo kuuzwa kinyemela pamoja na kuua viwanda vilivyopewa kazi ya kuzalisha mifuko mbadala.

Kwa upande wao Mamlaka za Udhibiti kupitia Wakurugenzi wa NEMC na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wametumia kikao hicho kutoa tamko la kusimamia operesheni hiyo ambapo wamemuahidi Makalla kuwa operesheni hiyo itafanikiwa.

Nao wazalishaji wa mifuko mbadala wamekiri uzalishaji kudorora kutokana na kuzagaa kwa mifuko iliyokatazwa kwenye masoko na maduka jambo linalosababisha viwanda vyao kufa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom