Msakila Kabende - CDM inayokataa BODABODA NA WANAWAKE inajivunia nini?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,398
1,266
WanaJf,
Salaam!

Haya ni maneno ya viongozi wa juu wa Chama cha Chadema:-
(a). Tundu Lissu - Tanzania ni nchi pekee duniani yenye watu waoga na wajinga. Aliongeza kuwa "nilitegemea kuona vijana na wanawake wakidai haki zao". Kwa mukitadha huu vijana na wanawake kutodai haki zao kwa mjibu wa CDM ni ujinga! CDM jichunguzeni.

(b). Godbless Lema - aliyoyasema kuhusu vijana wa bodaboda ni kuwakosea heshima vijana wetu, ni kuwakosea heshima wazazi wa vijana wetu, ni dhihaka kwa wanawake nchini. BODABODA NI KAZI YA LAANA.
CDM JICHUNGUZENI!

Nawakumbusha tu ili 2025 tusishangae kwenye kwa matokeo mabaya
 
Nchi hii kuna ujinga mwingi sana!
Nimemsikiliza Bw. G. Lema na nikarudia kumsikiliza. Na Kila nikimsikiliza napata ujumbe ule ule.
Msisitizo ni kuwa utitiri wa boda boda na VICOBA ni ishara kuwa umaskini umetamalaki. Yaani badala ya watu kuhoji ajira secure na decent wanabaki kumshambulia mtoa maoni!
Au ndo ile ishapitishwa kuwa boda boda ni ajira sahihi na VICOBA ni mfumo makini kabisa!

Nikarudia kumsikiliza T. Lissu. Ujumbe wake upo valid kabisa! Nchi hii watu wengi ni waoga na WAJINGA!

Wake up my people!

Choose not to follow the masses because in many occasions the M is silent or omitted altogether!
 
Lema ni mpuuzi sana!
Halafu mtu mwenye "kichwa cheupe" kama Godbless Lema eti naye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA!
CHADEMA ni debe tupu kabisa!
 
Tatizo kubwa la fikra za kimaskini ni kuridhika na mambo dhaifu na madogo madogo tu, tena yale yanayofanyika nje ya mfumo rasmi, na kuendeshwa kwa njia za kiholelaholela. Fikra kama hizi kamwe haziwezi kuchanganua kati ya sifa ya ubora wa vitu na wingi wa uwepo wake, uhalali na uharamu wake, ama pia haki ya kupata kitu cha msingi ikiitofautishwa na hisani ya kufanyiwa kitu.

Sera za CDM ni zile zenye kuegemea katika itikadi za kibepari, wakati zile za CCM ni za kijamaa ingawaje viongozi wake wanaishi katika mfumo laghai wenye matendo ya kibepari. Kupitia sera za chama chao, viongozi wa CDM wanaleta hamasa na kujaribu kuwafungua macho kwa kuwaelewesha wananchi kuhusu mambo ya msingi juu ya haki zao za msingi na ubora wa vitu, mathalani maeneo ya ajira, afya, uwekezaji, elimu, mafao ya wastaafu na wazee, kilimo, biashara n.k.

Upande wa CCM kwa kutambua sera zao zimefeli na kupitwa na wakati wanajitahidi kuficha ukweli huo. Wanatambua kuwa sera zao hazina jambo lolote lile jipya katika kuwakomboa wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli. Kwa hiyo hawana tena namna zaidi ya kujificha nyuma ya kivuli cha umaskini uliotamalaki miongoni mwa makundi ya vijana na wanawake, na kujaribu kuzikosoa sera za CDM kwa hoja hafifu.

Musa alipowaongoza wana wa Israel kutoka utumwani Misri na kuelekea nchi ya Kaanani, aliwaongoza kwa maono kuwa wanaenda katika nchi iliyojaa maziwa na asali. Licha ya hamasa hii kwa taifa lililotokea utumwani, kamwe halijawahi kuuona wingi huo wa maziwa na asali, zaidi ya msululu wa vita nyingi na mapambano magumu yaliyopelekea kuiteka na kujimilikisha nchi hiyo mpya.

Kwa hiyo basi, kauli ya Lema juu ya bodaboda na Vicoba inapotoshwa makusudi na wana CCM kwa kupitia tafsiri zao wenyewe, na fikra zao mufilisi na za kimaskini. Lakini kwa fikra pana na pevu, viongozi wa CDM wapo sahihi kabisa kwa ajili ya ustawi mwema wa maisha ya jumla ya wananchi katika siku zijazo. Ukweli ni ukweli tu, ingawaje wakati mwingine unauma, kuishi ndani ya maisha ya kimaskini katika taifa huru lililojaa kila aina ya rasilimali ni sawa kabisa na laana.
 
Sifa ya mwanasiasa ni kueleweka
Ukishindwa kueleweka ndo umeshindwa .....huwezi laumu watu .

..kuna genge la propaganda la Ccm ndilo linalolazimisha hoja kwamba Lema hajaeleweka.

..mimi ktk kufuatilia mikutano ya Lema nimeona wananchi wametoa muitikio mzuri kwa hoja yake kuhusu umasikini na bodaboda.
 
Laana !!!! No; Hatarishi YES

Kama vile ilivyowa wachimbaji wadogo, machinga n.k. ; Long term ni hatari kwa afya ya wanaofanya shughuli hio; ingawa wanaprovide need (service) lakini at what cost ?

Kama taifa long term tunapoteza we might be paying it back through medical / health costs
 
Kama bodaboda ni kazi halali, inatozwa kodi?.
Bodaboda ni kazi ya muda(not sustainable), kazi yenye hatari,kazi ambayo wahusika wengi ni illiterate, wengi wamekabidhiwa pikipiki za watu, wengi wao wakiwa hawana maadili.
Ukweli ni kwamba hii sio kazi ya kujenga taifa lenye nguvu.
Mtu anaifanya miaka kadhaa tu, miaka inayofuata ni mateso na kilio.
 
WanaJf,
Salaam!

Haya ni maneno ya viongozi wa juu wa Chama cha Chadema:-
(a). Tundu Lissu - Tanzania ni nchi pekee duniani yenye watu waoga na wajinga. Aliongeza kuwa "nilitegemea kuona vijana na wanawake wakidai haki zao". Kwa mukitadha huu vijana na wanawake kutodai haki zao kwa mjibu wa CDM ni ujinga! CDM jichunguzeni.

(b). Godbless Lema - aliyoyasema kuhusu vijana wa bodaboda ni kuwakosea heshima vijana wetu, ni kuwakosea heshima wazazi wa vijana wetu, ni dhihaka kwa wanawake nchini. BODABODA NI KAZI YA LAANA.
CDM JICHUNGUZENI!

Nawakumbusha tu ili 2025 tusishangae kwenye kwa matokeo mabaya
Yaani chadema ijichunguze kwa akili zako ndogo hizo pumbafu kweli,ishauri serikali yako badala ya kununua ma v8 itenge. Mapori kwa ajili ya skimu za umwagiliaji ichimbe visima na kununua matrekta yakutosha vijana wajiajiri huko pia iwatafatie masoko Bodaboda ni kazi ya laana.
 
Msakila Kabende ni mtu ninaye kufamu kiasi! Inasikitisha kuwa na wewe ulifaulu mitihani na ukaajituwa na Serikali kama Afisa Mipango!
 
..kuna genge la propaganda la Ccm ndilo linalolazimisha hoja kwamba Lema hajaeleweka.

..mimi ktk kufuatilia mikutano ya Lema nimeona wananchi wametoa muitikio mzuri kwa hoja yake kuhusu umasikini na bodaboda.
Ipo siku Ili genge litatoa tamko kuwa uchangudoa ni ajira nipo nimekaa pale.
 
WanaJf,
Salaam!

Haya ni maneno ya viongozi wa juu wa Chama cha Chadema:-
(a). Tundu Lissu - Tanzania ni nchi pekee duniani yenye watu waoga na wajinga. Aliongeza kuwa "nilitegemea kuona vijana na wanawake wakidai haki zao". Kwa mukitadha huu vijana na wanawake kutodai haki zao kwa mjibu wa CDM ni ujinga! CDM jichunguzeni.

(b). Godbless Lema - aliyoyasema kuhusu vijana wa bodaboda ni kuwakosea heshima vijana wetu, ni kuwakosea heshima wazazi wa vijana wetu, ni dhihaka kwa wanawake nchini. BODABODA NI KAZI YA LAANA.
CDM JICHUNGUZENI!

Nawakumbusha tu ili 2025 tusishangae kwenye kwa matokeo mabaya
Kuna mamb ambayo yanahitaji akili ya ziada kuyaelewa! Hii issue ya Lema na LISSU nadhan ungetulia na kuitafakar ili uelewe mantiki. Unavyojua haki dunian inaombwa? Je bodaboda ni kaz au ajira rasmi? Ni kwasababu ya ugumu wa maisha yetu bongo kuliko kukaa kijiweni, but bodaboda ni kaz ambayo ni risk san kwa vijana. Hata ww unajua hilo, nadhan ni hisia tu za kisiasa ndio zinakuongoza!!!
 
WanaJf,
Salaam!

Haya ni maneno ya viongozi wa juu wa Chama cha Chadema:-
(a). Tundu Lissu - Tanzania ni nchi pekee duniani yenye watu waoga na wajinga. Aliongeza kuwa "nilitegemea kuona vijana na wanawake wakidai haki zao". Kwa mukitadha huu vijana na wanawake kutodai haki zao kwa mjibu wa CDM ni ujinga! CDM jichunguzeni.

(b). Godbless Lema - aliyoyasema kuhusu vijana wa bodaboda ni kuwakosea heshima vijana wetu, ni kuwakosea heshima wazazi wa vijana wetu, ni dhihaka kwa wanawake nchini. BODABODA NI KAZI YA LAANA.
CDM JICHUNGUZENI!

Nawakumbusha tu ili 2025 tusishangae kwenye kwa matokeo mabaya
Sometimes nikisoma thread kama hizi huwa na Kumbuka Lowasa..... ELIMU, ELIMU, ELIMU....!!
 
Kama bodaboda ni kazi halali, inatozwa kodi?.
Mkuu nadhani hoja yako imegubikwa na ukakasi na technically does not hold water....., Kila kinachotozwa Kodi haimaanishi ni kizuri na kila kilicho halali haimaanishi kina tija...., in short tatizo kubwa la bodaboda ni afya / hatari kwa mtumiaji ingawa lina positives kama vile kufacilitate transport kwa watumiaji na ujira kwa waendeshaji
Bodaboda ni kazi ya muda(not sustainable), kazi yenye hatari
Ushasema sio kazi alafu unaji-contradict kwamba ni kazi ya muda, hatari yes kama vile ilivyo hatari kwa wachimbaji madini na hatari hio sio kwao tu hata kwa mazingira...
,kazi ambayo wahusika wengi ni illiterate, wengi wamekabidhiwa pikipiki za watu, wengi wao wakiwa hawana maadili.
hapa sasa umeanza kutoka kwenye mstari, kwahio kuwa kwao illiterate leo tukisema wakalime nyanya wataacha kuwa illiterate; how does one affect the other ? Na kutokuwa kwao na maadili ni ubodaboda boda wao ?
Ukweli ni kwamba hii sio kazi ya kujenga taifa lenye nguvu.
Mtu anaifanya miaka kadhaa tu, miaka inayofuata ni mateso na kilio.
In short hatuna kazi za kujenga taifa lenye nguvu wote ni madalali / middle men katika ngazi tofauti tofauti na wengine wachuuzi na wale madalali wetu wa high level ndio kila siku wanazunguka kukopa huku na kule na kutengeneza miradi vapor ili hawa waendesha Boda tozo wanazokamuliwa na zile za wajukuu zao zije kulipa madeni
 
WanaJf,
Salaam!

Haya ni maneno ya viongozi wa juu wa Chama cha Chadema:-
(a). Tundu Lissu - Tanzania ni nchi pekee duniani yenye watu waoga na wajinga. Aliongeza kuwa "nilitegemea kuona vijana na wanawake wakidai haki zao". Kwa mukitadha huu vijana na wanawake kutodai haki zao kwa mjibu wa CDM ni ujinga! CDM jichunguzeni.

(b). Godbless Lema - aliyoyasema kuhusu vijana wa bodaboda ni kuwakosea heshima vijana wetu, ni kuwakosea heshima wazazi wa vijana wetu, ni dhihaka kwa wanawake nchini. BODABODA NI KAZI YA LAANA.
CDM JICHUNGUZENI!

Nawakumbusha tu ili 2025 tusishangae kwenye kwa matokeo mabaya
Kwani wewe unasemaje ? Mbona hujajiajiri huko? Kutwa kucha uko mitandaoni.
 
Back
Top Bottom