Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,305
- 9,734
Ndugu zangu watanzania,
Hii ni rekodi mpya. Ni historia ya kipekee aliyojiwekea Rais Samia na serikali yake mitaani, haijawahi kutokea kiongozi wa kisiasa kuteka mijadala mitaani kupita hata habari za michezo na burudani, kwa Sasa Rais Samia ni zaidi ya habari za michezo maana kaweza kuteka Hadi mioyo ya wanamichezo ambao ushindi ukipatikana uwanjani unaona watu wanavyotabasamu na kusema kwa bashasha na furaha kuwa huu ni ushindi na zawadi kwa ajili ya mama yetu na Rais wetu mama Samia.
Kila Kona kila mahali Ni Rais Samia juu ya uchapa kazi wake na umahiri wake katika uongozi,ukienda kwa wakulima unawakuta wanatafuna mahindi ya kuchomaa na kumzungumza Rais Samia namna alivyowasaidia katika kilimo baaada ya kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni.
Ukienda kwa akina mama magengeni unawakuta na kuwasikia namna alivyowasaidia kuwatua ndoo kichwani baada ya kuwasogezea maji karibu yao na hivyo kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta maji,Ndio maana wanawake wengi Sana saizi mitaani wakijifungua watoto wa kike Ni kawaida kusikia mtoto anapewa jina la Samia Kama sehemu ya kufurahishwa na uchapa kazi na namna mama Samia alivyogusa maisha Yao, na siku zote jina jema huvuma na kukaa midomoni mwa watu na kukumbukwa na wengi Sana hata ikiwa mtu husika ametangulia mbele za haki Kama anavyokumbukwa Hayati Baba wa Taifa mwalimu Nyerere au Nelson Mandela au Dr Martin Luther King junior au John F Kennedy au George Washington.
Ukienda kwa wanachuo, vijana, wanafunzi, wafanyabiashara, wajasiriamali, bodaboda,madereva bajaji kwote huko unakuta Rais Samia Ameziteka nyoyo zao kwa namna alivyowawezesha na kuwasaidia kutimiza Ndoto zao na kufanya shughuli zao kwa amani pasipo bugudha Wala kero ilimradi tu watu wazingatie Sheria, kanuni na taratibu.
Ukienda kwa watumishi wa umma wanatamani hata uchaguzi ufanyike kesho ili wampigie kura za Ndio kwa kishindo Rais Samia kutokana na namna alivyowafuta machozi na kuwapa Tabasamu Katika Mioyo yao hasa baada ya kuwapatia Nyongeza ya mshahara ya 23%, kuwapandisha madaraja na kuwalipa kulingana na madaraja Yao, kuwalipa malimbikizo ya madeni Yao, kuwaboreshea mazingira ya kazi Hali iliyowapatia morali kubwa Sana ya kuchapa kazi kwa bidii kubwa Sana na kujituma katika kuwahudumia Watanzania.
Kwa Sasa Rais Samia Ni Kama maji usipoyanywa utayaoga tu, kwa hakika Rais Samia amepewa kibali na Mwenyezi MUNGU cha kuongoza Taifa letu, Mungu kambariki na Kumjalia uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi Rais Samia,kamjalia na kalama ya uongozi, kampa kila kitu anachopaswa kuwa nacho kiongozi wa ngazi ya juu kiuongozi Kama alivyo Rais Samia.
Rais Samia ni Kama Mti uliopandwa kandokando ya chemchemi ya maji isiyo kauka maji masika na kiangazi haukauki Wala kusinyaa majani yake ,Rais Samia hakauki Wala kukatika katika midomo ya Watanzania, watu wote wanayo amani na furaha ya uwepo wa Rais Samia, Rais Samia Anatazamwa Kama Mtumishi mwema na mnyenyekevu kwa watu, mtetezi na mfariji wa Taifa letu na kiongozi wa watu wote.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.