Msafara wa Zitto Kabwe wazuiwa Tunduru

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Jeshi la Polisi Wilaya Tunduru limezuia msafara wa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe likidai hawana taarifa ya ziara hiyo.

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye yuko kwenye ziara ya ujenzi wa chama mikoa ya Kusini msafara wake ulizuiwa ukitokea kata ya Namwinyu kwenda Kijiji cha Kajima.

Kwa mujibu Mkuu Jeshi la Polisi Wilaya ya Tururu, Eliachim Magambo baada ya kupokea taarifa ya ziara hiyo alijibu kwa kuwaeleza kuwa kidato cha nne wanaendelea na mtihani.

Hata hivyo Zitto amedai nchi ni ya vyama vingi vya siasa na kila mtu anaalipa kodi hivyo Jeshi la Polisi halipaswi kuwatisha wananchi.

"Mnavyoona hawa Polisi wanategemea mishahara inayotokana na kodi zetu hawapaswi kututisha hivyo wanapaswa kuacha Vyama vya Siasa kutekeleza majukumu yao,"amedai Zitto.

Hata hivyo Kiongozi huyo ameendelea na ziara yake huku Jeshi la Polisi likiwa limeimarisha ulinzi.

MWANANCHI
 
Zitto alisemaga Act wanaponya nchi, naamini hata hilo zuio ni sehemu ya uponyaji wa nchi
 
Back
Top Bottom