Wanajamvi kwa kuwa jf ni sehemu ya kubadilishana ujuzi/elimu naomba kuhabarishwa umuhimu wa gari za msafara wa raisi na viongozi wengine kwenda kasi hasa maeneo yenye miji mikubwa kam dsm. Nauliza hivyo kwa sababu kila siku wadau wa usimamiziwa usalama barabarani wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kwenda mwendo wa taratibu ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali. nina imani kama msafara wa raisi usingekuwa na spidi yule trafic asingegongwa au hata akigongwa labda asingepoteza maisha