Msafara wa Rais lazima uende kasi?

Msafara wa Rais lazima uende kasi?

Je zile BMW za kikwete si bullet proof...?

hawajilindi tu kwa kuogopa kuwa sniper anaweza kuwa na m107.50 caliber zinazojulikana kuwa ni za ma sniper ila wanajilinda hata kwa
dude kama hili


images
 
mimi sijui bana mambo mengine yanatia hasira, tukuchague kwa kura za wazi na kampeni kwenye mikutano ya wazi lakini leo hii unatukimbia barabarani kama upepo.

mimi sijui bana
 
Wanajamvi kwa kuwa jf ni sehemu ya kubadilishana ujuzi/elimu naomba kuhabarishwa umuhimu wa gari za msafara wa raisi na viongozi wengine kwenda kasi hasa maeneo yenye miji mikubwa kam dsm. Nauliza hivyo kwa sababu kila siku wadau wa usimamiziwa usalama barabarani wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kwenda mwendo wa taratibu ili kupunguza uwezekano wa kutokea ajali. nina imani kama msafara wa raisi usingekuwa na spidi yule trafic asingegongwa au hata akigongwa labda asingepoteza maisha
Hakuna haja huko ni kulewa sifa tu. Sasa wanamkimbiza utadhani wanamuwahisha hospitali wanamwogopa nani? Kama anaharaka si apande helkopita? Kwanza kwa nchi kama yetu msafara wake unapaswa uwe na magari matatu tu moja mbele la walinzi, katikati yeye kibosile na mwisho tena gari la askari. Mbele kabla ya magari kunatangulia pikipiki ya kufagia njia. Lakini kwa ujinga wetu mtu anaenda mahali pasipozidi km 1 anakuwa na msafara wa magari 40. Mimi naweza kusema hata huyo askari aliyekufa kifo chake kimesababishwa na msafara wa rais!
 
Hakuna umuhimu wa kwenda kasi. Ni kutaka sifa tu!
Sifa za kijinga! Msafara wa Nyerere ulikuwa unakwenda mdogo mdogo. Huyu wanamkimbiza utadhani jambazi au mwanamke anayekwenda kujifungua?
 
nadhani huwa kunamambo mengi yanayo zunguka uongozi wajuu,sio kwa bongo tu hata kwingine..sometimes ajali za ainahiyo inaweza kuwa planed ndomana kunawakati nivigumu kufanya maamuzi hayo unayofikiria..!!
Ni uoga tu wa viongozi wetu..kutokana na matendo yao mabaya..siku ikipata
ajali nadhani watakufa sana. Nakumbuka ilitokeaga ajali ya polis waliokuwa mbele kwenye msafara wa makamu wa Rais Gharib Bilal kule tanga.. hawakusimama kamwe! waliendelea na safari.. Askari wa tatu walikufa pale pale.. nikasema kweli viongozi wetu hawana utu..
 
Si lazima na wala si muhimu. Usalama unahatarishwa zaidi kwa mwendo wa kasi, nadhani ilikuwa nyakati za Ukomunisti na harakati za Ukombozi kusini mwa Afrika ndipo kulikuwa hakuna usalama na walijifanya kuhitaji kwenda kasi hivyo, vinginevyo ni kusababisha maafa kwa watu na askari. Hata ving'ora nadhani havina maana kama askari wanaongoza kwanini kuwe na vingora kuwapigia watu makelele. Si kila kitu tuige, tuwe wabunifu kulingana na hali zetu. Full stop!
 
Unataka msafara uende taratibu ili mmpopoe kwa mawe???

Ni kweli kabisa baba riz akisema aende na low speed usishangae kuona wamempopoa na mawe cuz watanzania ni wengi sana yafika almost 45mil kwa number bt only watanzania 5mil ndio waliomptisha so the rest wote hawamtaki. usitegemee kuona anaenda low speed hata siku moja cuz anajua threat ya usalama wake kuwa ipo kwenye degree ngapi.
 
Kwanza ni usalama pili kupunguza foreni maana akienda mwendo wa kinyonga foren yake hamiwez kudumu mtakua mnapigakelele tena aongeze mwendo tupunguze lawama.afu kingne niliona kuna mwanajamvi alipost jana kua ni gari ambayo ilichomekea foreni so msilaumu sana... ni karibia nchi zote zinafanya hivyo. huyo alosema mbona Obama afanyi hivo ikumbukwe raisi wa marekani na nchi zilizoendelea wana njia zao spesho so hawawez sababisha foreni kama kwetu.
 
Je zile BMW za kikwete si bullet proof...?
Ni Bullet proof ofcourse lakini wataalamu wa mambo ya usalama (simple physics) wanasema pamoja na bullet proof material, risasi inayogonga at 90 degrees inaweza kuwa na impact kubwa ukilinganisha na any other entry angle. Gari likiwa katika kasi ile si rahisi kwa snipper kurenga at 90 na hivyo kupunguza zaidi damage ambayo ingefanywa na say, a very poweful bullet.

Kama kweli mwendo kasi ungekuwa ni mbinu nzuri ya usalama basi msafara za rais wa Marekani ungekuwa unakwenda kwa kasi ya ajabu! Lakini kwa waliowahi kuhuhudia 'the beast' (gari analotumia rais wa Marekani) lina mwendo wa kinyonga.

Tanzania tunatakiwa kutumia akili zaidi na sio nguvu. Kinachotakiwa ni gari lenye kuhimili potential threats i.e bullet, bombs etc. Mwendo kasi ni utashi wa kijima na kamwe hauwezi kumueweka salama rais.

Jambo jingine, pamoja na nia nzuri ya rais kutembelea miradi jijini Dar es Salaam, lakini nilidhani team nzima ya Ikulu wangetafakari tena umuhimu wa rais kukatiza mitaani siku za kazi huku wakitambua adha ya foleni.

Walitakiwa wafirikie hasara na usumbufu utokanao na msafara wa rais -siku ya kazi- kwenye jiji la biashara, jiji ambalo foleni inagharimu uchumi. Wachumi wanaweza kufanya mahesabu ya hasara inayoweza kuletwa na misafara ya viongozi.

Ni kwanini - kama kweli rais alitakiwa kutembelea jiji - asifanye hivyo siku za weekend? Kuna ulazima gani wa kufanya ziara given halisi ya Dar es Salaam siku za kazi? Misafara ni kero sana hapa jijini na kama kuna namna ya kuipunguza (i.e kufanya ziara weekend) basi wafanye hivyo.

Mkuu sasa ukifananisha wamarekani na "the Beast" wao sio fair ati. Kwanza ungerejea specs za huyo the beast huwezi kufananisha na hizi zetu. Pili security system yao ipo far advanced kuliko yetu mfano, mara ngapi unawaona secret service wapo kwapa kwa kwapa na Obama? lakini angalia kwetu raisi anahutubia mtu kasimama kisogoni kwake mpaka anaharibu picha. Na by the way motorcade ya america kuna wakati inakimbia pia sio mara zote inatambaa kama kweye ceremonies za kuapishwa ati.

Pamoja na yote hayo natamani huyu wetu angekua anatumia chopper zaidi!
 
hata mimi huwa nashangaa msafara hata wa mama salma kikwete ulikuwa na magari yasiyopunguwa 40.. Huyo ni mama akiwa baba sipati picha; ajali hazitaisha
 
mimi sijui bana mambo mengine yanatia hasira, tukuchague kwa kura za wazi na kampeni kwenye mikutano ya wazi lakini leo hii unatukimbia barabarani kama upepo.

mimi sijui bana

Hili nalo neno ujue swahiba, wakishapata siye siyo binadamu tena wa kufuatwa kuombwa bali kukimbiwa, ona sasa yaliyojiri...
 
hiyo ni mbinu pia na yakinunuliwa magari ya kifahari kama ya rais wa marekani si ugomvi mwingine huo? mfano ni ndege aliyonunua Mkapa
 
Kwanza ni usalama pili kupunguza foreni maana akienda mwendo wa kinyonga foren yake hamiwez kudumu mtakua mnapigakelele tena aongeze mwendo tupunguze lawama.afu kingne niliona kuna mwanajamvi alipost jana kua ni gari ambayo ilichomekea foreni so msilaumu sana... ni karibia nchi zote zinafanya hivyo. huyo alosema mbona Obama afanyi hivo ikumbukwe raisi wa marekani na nchi zilizoendelea wana njia zao spesho so hawawez sababisha foreni kama kwetu.
Mkuu kawaida ni Ambulance na magari ya Zimamoto ambayo yanatakiwa kwenda kwa speed hiyo isiyoya kawaida na si gari la kingozi, kwani anakimbilia wapi, kupanda ndege kachelewa? kama anaenda eneo la tukio, tayari watu wanajua atakuja, na kama anarudi Ikulu, akishafika pale ile speed ilikuwa na maana gani ama kuna kitu gani anakimbilia kukiwahi kule Ikulu? Nenda popote duniani katika sheria za barabarani utakapokuta kuna sheria ya aina hiyo, labda ni Tanzania tu.
 
Mkuu kawaida ni Ambulance na magari ya Zimamoto ambayo yanatakiwa kwenda kwa speed hiyo isiyoya kawaida na si gari la kingozi, kwani anakimbilia wapi, kupanda ndege kachelewa? kama anaenda eneo la tukio, tayari watu wanajua atakuja, na kama anarudi Ikulu, akishafika pale ile speed ilikuwa na maana gani ama kuna kitu gani anakimbilia kukiwahi kule Ikulu? Nenda popote duniani katika sheria za barabarani utakapokuta kuna sheria ya aina hiyo, labda ni Tanzania tu.

Magari ya misafara yalikuaga na kawaida ya kqenda polepole mpaka hapo mwaka 1964 alpouwawa John kenedy kwa sniper baada ya hapo magari yakaanza kwenda kasi kwa sababu ya kuavoid kitu kama hicho ni balacade zote duniani zinaenda kasi labda kama uko dunia nyingi wewe angalia hata youtube tafuta misafara ya viongozi utaona. kingine wakienda polepole hizo foreni.mtaweza kuzimudu? wale wanaoendesha ni trained people ndo maana ni rarely sana kutokea ajali sababu wanajua wanachokifanya.
 
Nafikiri pamoja na suala la usalama tayari wanakuwa wameshakubaliana wataendesha kwa speed gani.
 
Back
Top Bottom