Msafara wa Makamu wa Rais Mbeya....

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
725
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Bilal amepita muda si mrefu eneo la Mwanjelwa jijini Mbeya akiwa na msafara wake wenye magari kadhaa.

Kilichoshitua watu wengi ni ile kasi ya mbio za mwenge waliyopita nayo bila kujali kwamba wananchi walijipanga kwa wingi barabarani ili waweze kumsalimia kiongozi wao japo kwa kumpungia mkono.

Kasi waliyopita nayo ilipelekea wananchi kadhaa walikuwa katika vikundivikundi wabakiwakijiluiza kulikoni? Wengine walikwenda mbali zaidi na kudai "ameshauriwa na viongozi wa CCM kwamba eneo hilo ni hatari hivyo wapite kwa spidi kali kama vile wanakimbiza mwenge kwa hofu ya kupopolewa?"
 
Amekosea sana aisee...angesimama japo kwa saa 1 hivi akawapa neno kidogo wananchi wake...sasa sijui alikuwa na haraka gani...
 
uko mbeya ni pagumu sana,jk mwenyewe anapaogopa,si mnakumbuka mkasa wa kupigwa mawe jamani au?
 
Ni ishara mbaya sana kwa wananchi. Kiongozi mzuri ni rafiki wa wananchi na kiongozi mbovu ni adui kwa wananchi. Viongozi wengi wa serikali ni maadau zetu zamani tulikuwa tunawaogopa kwa sasa wanatuogopa.
 
Wamepima upepo wameshaona pale hapafai aende tu awahi mazishi ya mama Blandina Nyoni kumuwakilisha musee ya sherehe na misiba!!!
 
Popoa mawe style!watu wa mbeya ni hatari,hamna staha hata kwa watawala wenu wa nchi,mnawafanya waogope Mbeya kama vile sio sehemu ya Tanzania bhana!
 
Hah hah Mbeya kwetu si mkyeso,lakini watakuja tu wakati wa kuomba kura na hapo ndipo tutakapowauliza''je waheshimiwa sasa hamuogopi kupopolewa ''
 
Amekosea sana aisee...angesimama japo kwa saa 1 hivi akawapa neno kidogo wananchi wake...sasa sijui alikuwa na haraka gani...

Hayo ndiyo yalikuwa matarajiyo yao.Na mwitikio wao ulikuwa mzuri kando kando ya barabara.Ila spidi ile, hakubaliki kama malaria!
 
Ni ishara mbaya sana kwa wananchi. Kiongozi mzuri ni rafiki wa wananchi na kiongozi mbovu ni adui kwa wananchi. Viongozi wengi wa serikali ni maadau zetu zamani tulikuwa tunawaogopa kwa sasa wanatuogopa.

Ipo haja ya kujifunza mbinu za ushawishi za muasisi wa taifa letu:Nyerere ambaye alijiamini sana.
 
uko mbeya ni pagumu sana,jk mwenyewe anapaogopa,si mnakumbuka mkasa wa kupigwa mawe jamani au?

Wananchi waligusia hilo, kwamba wanaogopa kupopolewa?Ni eneo hilohilo. Japo hawakujiandaa kwa hilo walikuwa na nia njema tu.
 
Back
Top Bottom