MASIHIHISHO KIDOGO MKUU,
Umati wa watu pembezoni mwa barabara kati ya maeneo ya Soweto, Mwanjelwa mpaka Mafiati ulitokana na kuzuiliwa kwa magari yatokayo katikati ya jiji na yale yatokayo Iyunga na Mbalizi kwa muda mrefu bila msafara kupita na hivyo abiria wengi kuamua kutembea kwa miguu pembezoni mwa barabara kutoka Kadege, Maghorofani, Eso,na Mafiati kuelekea Mwanjelwa na Soweto ;Na ndiyo maana watu wengi walikuwa wakitembea na siyo kusimama.
Wengi wao walilalamika kwa kukwamishwa kwa muda mrefu huku wale ambao safari zao zilikaribia mwisho wakishuka kwenye daladala na kuamua kutembea kwa miguu.
Udhaifu wa polisi,
Polisi walionekana kutojipanga vizuri kimawasiliano. Kwa mfano, nikiwa eneo la Mafiati nilishuhudia baadhi ya askari wakitumia simu za mkononi kuwasiliana kwa taabu na wenzao wa maeneo mengine, hii inatokana na kusumbua kwa mawasiliano ya simu kwa muda mrefu hapa Mbeya, na hasa mtandao wa vodacom.
Mawasiliano mabovu miongoni mwa askari yalipelekea waendesha magari kuingia ingia barabara kuu hata msafara ulipokaribia.
Polisi pia waliamini katika vitisho na mbwembwe kuliko mbinu za kitaalamu, walipita mara nyingi na mbwa wao kwenye magari huku wakiwaliza kwa makusudi ili kuwatisha watu ambao hata hivyo waliishia kuwadharau.Wengine walisema 'mbona siku za vurugu za wamachinga walinywea?'
Kuhusu mwendo mkali,
Binafsi niliutarajia kwani mashushushu waliotangulizwa lazima waliisoma hali halisi kuwa hakukuwa na raia yeyote aliyekuwa na interest na msafara wa bilal zaidi ya watu kuishia kukekejeli ufungwaji wa bendera mpya za sisiemu kwenye miti ya barabarani huku kwa siku mbili mji ukijaa ma-landcruiser hardtop yenye watu wenye T-shirt 'mpya'za kijani.
Nusura mwendo ule uwatokee puani askari waliokuwa kwenye land cruiser ya mwisho(wale FFU wenye sare zenye vifundo kwenye joint zote za miili yao mithili ya nzige atakae kuruka).Wakiwa konani pale Mafiati na spidi zao '120', nusura gari limshinde dereva aliyeamua kutumia breki na hivyo gari kuserereka kwa sekunde kadhaa huku watu wa pembezoni wakishikiria pumzi zao kwani nao wangeathirika ikiwa mambo yangeenda vibaya. Baada ya msafara kupita ilihitaji sekunde 20 tu kumrudisha kila mtumiaji wa barabar mahali pake, hakuna aliyeonekana kujali wala kujiuliza kuhusu msafara.
Nilihuzunishwa na sura za wliokuwemo kwenye magari kuanzia bilal , mkewe , mpaka wapambe wengine. Walionekana wenye sura za wasiwasi sana, namini wakisubiri jiwe la kwanza kurushwa!
.........niliendelea na safari yangu kwenye daladala kurudi nyumbani na mafuta yangu ya taa, niliYOyafuata Mafiati
kutoka Block-T,KWANI VITUO VYA MAFUTA VLIVYOKO MWANJELWA, SOETO, NA MAMA JOHN HAVIYAUZI KWA
MIEZI MITATU SASA.........PALE OILCOM SOWETO TANGAZO KUUKUU LINASOMEKA...'DEAR CUSTOMER WE HAVE
NO KEROSINE, MAY BE TRY TOMORROW!......HAPO HAKUNA ATAKAYE USUBIRI MSAFARA WOWOTE WA KIONGOZI
WA SERIKARI KWA HAMU HATA IWEJE, WATAPIGWA SANA MAWE SAFARI HII.