Msaada wa namna ya kupata mafao yangu ya NSSF

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,891
Habari wakuu,

Kuna ajira fulani nilikuwapo nafanya miaka minne nyuma ambapo niliifanya kama 4 yrs nikaiacha bila utaratibu maalumu maana nilipata Safari ya ghafla nikaona mambo yasiwe mengi.

Sasa leo katika kupekua pekua ID's zangu nimekutana na Card ile ya NSSF na nikakumbuka hawa jamaa walinikakatakata sana vihela vyangu

Sasa nahitaji kujuzwa na wale wanaojua haya masuala kwamba hapa naanzia wapi kufuatilia vichenchi vyangu au ndo sipati kitu kwenye ile saving?
 
Chukuwa kadi yako ya NSSF nendanayo kwenye tawi lao wakupe balance ya michango yako

Then waombe form ya kuomba madai ya Fao la kutokuwa na ajira watakuomba uandike barua ya kuomba madaia pia barua ya mwajiri wako wa mwisho uwe nayo
Mizunguuko ni mingi UVUMILIE watakupa 30% ya mafao yako utalipwa kidogo kidogo ndani ya 6 month

Kitambulisho cha mpiga kura na majina ya kitambulisho chako cha mpiga kura au Nida yafanane na yalioko NSSF hata taarifa zako za Bank majina yafane na majina yako ya kitambulisho cha uwanachama wa NSSF

Katika malipo yako utakutana na KIKOKOTO kuwa mvumilivu na MACHUNGU
 
Utapata 1/3 ya michango yako utayolipwa kama mshahara kwa miezi 6.Baada ya hapo ni kusubiri mpaka ufike miaka 60. Ukiona ngumu ishi kimjini mjini watu wakusovie mambo upate kibunda chote kamili.
 
Utapata 1/3 ya michango yako utayolipwa kama mshahara kwa miezi 6.Baada ya hapo ni kusubiri mpaka ufike miaka 60. Ukiona ngumu ishi kimjini mjini watu wakusovie mambo upate kibunda chote kamili.
Kumbe kuna mchongo kama hiyo..
 
Naongea kama nilivyopitia
Moja ya kanuni za kulipwa mafao yako kabla ya muda wa kustaafu ni kuachishwa kazi kama mgonjwa.
Nenda kwenye kituo cha TB (Kifua kikuu), ongea lugha sanifu wakuandikiea cheti kama muhanga
Peleka cheti NSSF kama umeachishwa kazi kutokana na maradhi, vuta mshiko wako potea, usimwachie hata buku mlinzi.
 
Nimwkucheki mkuu PM
 
Back
Top Bottom