Utofauti wa majina yangu kwenye vitambulisho umepelekea nishindwe kupata mafao yangu, nifanyeje?

erickelly

Member
Oct 5, 2018
23
9
Habari wapendwa,

Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF.

Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani.

NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika.

Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
 
Hapo wajanja wanataka hyo hela yako

Kuna mzee huku wakat yupo kazin akagundua mke aliemuoa atawah kustaafu kabla yake ili kuuwa soo asionekane ameoa kikongwe sijui akafanyaje akabadilisha tarehe zake za kuzaliwa ili astaafu mapema kabla ya mkewe

Kilichomkuta ni balaa kateseka balaa kupata hiyo hela sina uhakika kama ameshapata toka 2015 pamoja na kuwa alikuwa na marafik kibao halimashauri
 
Habari wapendwa.

Nina shida katika ya majina kitambulisho cha (NIDA) na (NSSF) majina sawa ila katika barua yangu ya ukomo wa (ajira) na (certificate) majina tofauti na ya hivyo vitambulisho cha NIDA na NSSF

Nimeongea na mwajiri wangu anisaidie kubalisha kwenye barua na certificate anasema haiwezekani

NIDA, mahakaman, aridhi, gazeti nimeshaenda lakini bado nahangaika

Nifanyeje ili niweze kupata mafao yangu?
Nenda stationary wata scan hizo barua na certificate watabadili majina tu yaendane na NIDA na NSSF mkuu ukikwama ni pm nikusadie

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Kula kiapo mahakamani kuyakubali kuwa yote hayo ni majina yako.
Lakini hakikisha majina yalioko benki yapo sawa na kiapo kimojawapo.
Kwa faida ya wengine, ili upate mafao yako vifuatavyo lazima vipelekwe kwenye mfuko wa mafao;-
1. Barua ya ajira
2. Barua ya kuthibitishwa kazini
3. Bank statement
4. Salary slip
5. Kitambulisho cha NIDA/Leseni ya udereva/mpiga kura
6. Barua ya cheo cha mwisho
7. Picha za PPS nadhani sita hivi
 
Mf mie
NSSF,kazini, NIDA, DL,Bank kuna majina ma3

Vyeti vya shule kuna ma2

Haitonisumbua lolote huko mbele?
Hili ni janga la nchi. Tanzania watu wanarahisisha sana mambo ka sababu ya uzembe. Watu hawako makini kuandika majina na wanajiandikia wanavyotaka. Hata tofauti ya herufi moja ni kosa kubwa na kisheria ni jina tofauti. Ni vizuri wakasumbuliwa na kukwama kabisa kwani wengi ni wabishi. Watu wanafanya uzembe hata kuandika maneno marahisi kabisa lakini ukimpa alert anakutukuna. Na hapa sizungumzii kukosea kwa bahati mbaya ambako mtu yoyote anaweza kufanya hivyo. Naongelea uzembe wa kutojali.
 
Kula kiapo mahakamani kuyakubali kuwa yote hayo ni majina yako.
Lakini hakikisha majina yalioko benki yapo sawa na kiapo kimojawapo.
Kwa faida ya wengine, ili upate mafao yako vifuatavyo lazima vipelekwe kwenye mfuko wa mafao;-
1. Barua ya ajira
2. Barua ya kuthibitishwa kazini
3. Bank statement
4. Salary slip
5. Kitambulisho cha NIDA/Leseni ya udereva/mpiga kura
6. Barua ya cheo cha mwisho
7. Picha za PPS nadhani sita hivi
Upo sahihi ndugu ila nilienda mahakamani nikapewa kiapo nikaenda aridhi kwa msajili wamajina akanipa deedpool na mihuri nyuma yatanganyika lakini nilivyopeleka nssf wakaniambia eti nikabadilishe ile card yao jina yafanane nikaenda sehemu yakubadilishia nikatoa 5000 lakini zoezi likashindikana hadi nida na nida yeneyewe ndio muzunguko huu mwezi 3 sasa nahangaika tu ndio maana nikaja humu kwa msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom