Msaada wa kisaikolojia unahitajika haraka

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,830
2,000
Binadamu yeyote anapoonesha kuwa katika msongo wa mawazo anahitaji kupewa msaada wa kisaikolojia haraka kabla hali haijawa mbaya.

Huyu mheshimiwa asaidiwe na wale aliokuwa akiwahudumia kama KM maana wamemtosa hata kum address kama KM mstaafu hawataki.

Kauli yake ya " Ili ubaki na dola tumia dola kubaki na dola" naona kwake mwenyewe imeshindikana.

Nimepewa taarifa toka mjengoni kuwa jamaa anahitaji uangalizi na ushauri.

Bashiru.JPG
Asaidiwe!
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
29,365
2,000
Bashiru atakuwa mjinga ikiwa ana mawazo ya kuachwa kwenye ukatibu mkuu KIONGOZI.
yaani umekaa Tu hapo mijihera inaingia Tu alafu uwe na mawazo?
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,925
2,000
Jela inamsubiri. Alimwambia mama "Tanzania kwa sasa haijawa tayari kuwa na rais mwanamke, unaonaje ukijiuzulu"

Baada ya kuapishwa mama akamjibu "aliyesimama hapa ni Rais mwenye jinsia ya kike".

USHAURI WANGU: Aende Ikulu na waandishi wa habari akaombe msamaha kama Nape kwa Magofool.

IMG_20210411_210541_348.JPG
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,399
2,000
Mtu analipwa pesa kibao hapo! Halafu unaleta kiherehere hapa! Hilo pozi tu zugia toto
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,110
2,000
Bashiru atakuwa mjinga ikiwa ana mawazo ya kuachwa kwenye ukatibu mkuu KIONGOZI.
yaani umekaa Tu hapo mijihera inaingia Tu alafu uwe na mawazo?
Mkuu haya machadema ndio yanataka kutuaminisha kwamba Bashiru ana msongo wa mawazo.

Na 2025 anaenda kuchukua jimbo au hata anaweza kulimwa uwaziri muda wowote.
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,401
2,000
Binadamu yeyote anapoonyesha kuwa katika msongo wa mawazo anahitaji kupewa msaada wa kisaikolojia haraka kabla hali haijawa mbaya...
Tuliowahi kukaa na huyu jamaa mitaa ya Kemondo -Maruku, Ilungami hizi huwa ndio pozi zake tu!

Alafu nikuulize mleta mada....Katibu Mkuu wa Chama chenye wabunge wengi na vitega uchumi kibao, mbunge wa kuteuliwa mwenye mshahara na miposho lukuki unadhani anawaza Sana kama wewe Mwl. Elizeus wa Shule ya Msingi Bunduku? Tuache utani Bashiru huyu aliyejituma kuanzia mwalimu wa kujitolea Kashozi sekondari hadi kuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

Watu wa aina ya Bashiru tamaa kwao sio sehemu yake! Siasa inemuita yeye na sio yeye aliyeitafuta kama Nape, Makamba jr, nk.
Watu waliojijenga wenyewe from zero huwa plan A ikibuma tayari wanakuwaga na plan B na C.

Hapo alipo Bashiru kwa tunaomfahamu panamtosha Sana sema Kazi aliyopewa ya kuongoza tume ya kubaini na kurudisha mali za CCM walizokuwa wamegawana watoto wa wakubwa akina Kingunge, Diallo, Gachuma nk ndio zimemtengenezea maadu wengi na sio vinginevyo!
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,110
2,000
Jela inamsubiri. Alimwambia mama "Tanzania kwa sasa haijawa tayari kuwa na rais mwanamke, unaonaje ukijiuzulu"

Baada ya kuapishwa mama akamjibu "aliyesimama hapa ni Rais mwenye jinsia ya kike".

USHAURI WANGU: Aende Ikulu na waandishi wa habari akaombe msamaha kama Nape kwa Magofool.

View attachment 1759343
Ukivyoandika tu inaonesha ulisikia hii stori shemeji yako akimsimulia dadako ndio nawewe ukaidaka kama ilivyo.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,156
2,000
Watanzania aina ya mleta mada ni wajinga sana jamani!

Mwenzio hapo anaondoka na milioni 11 per month nje ya marupu rupu mengine.

Ila wewe unaedemka hapa jf huku ukipiga miayo eti unataka umshauri kisaikolojia?

Akili au matope?
Unafikiri kila mtu anakuwa driven na hela?
Ingekuwa pesa ndo inaondoa msongo wa mawazo basi watu wenye hela wangekuwa hawapati depression!

Binadamu ana "nyota" mtu mwenye nyota kubwa bado atapata depression kutokana na vitu vinavyoendana na nyota yake
Na binadamu mwenye nyota ndogo, naye atapata depression kutokana na vitu vinavyoendana na nyota yake
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,850
2,000
Tuliowahi kukaa na huyu jamaa mitaa ya Kemondo -Maruku, Ilungami hizi huwa ndio pozi zake tu!
Alafu nikuulize mleta mada....Katibu Mkuu wa Chama chenye wabunge wengi na vitega uchumi kibao, mbunge wa kuteuliwa mwenye mshahara na miposho lukuki unadhani anawaza Sana kama wewe Mwl. Elizeus wa Shule ya Msingi Bunduku? Tuache utani Bashiru huyu aliyejituma kuanzia mwalimu wa kujitolea Kashozi sekondari hadi kuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam....
Watu wa aina ya Bashiru tamaa kwao sio sehemu yake! Siasa inemuita yeye na sio yeye aliyeitafuta kama Nape, Makamba jr, nk.
Watu waliojijenga wenyewe from zero huwa plan A ikibuma tayari wanakuwaga na plan B na C....
Hapo alipo Bashiru kwa tunaomfahamu panamtosha Sana sema Kazi aliyopewa ya kuongoza tume ya kubaini na kurudisha mali za CCM walizokuwa wamegawana watoto wa wakubwa akina Kingunge, Diallo, Gachuma nk ndio zimemtengenezea maadu wengi na sio vinginevyo!
Ataendelea kuteseka sana na bado hadi akonde kama msumari
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom