Msaada: Ufafanuzi juu ya Islamic Banking

Msaada: Ufafanuzi juu ya Islamic Banking

Riba sio biashara. Tehe tehe misaafu hii raha sana. Unanunua kitu 200 unauza 220 sio dhambi,ila ukikopa 200 ukirudisha 220 ni dhambi. etii tofauti ni kwamba hii ni riba ile ni faida ha ha ha.

Ndio maana waislamu wanadanganywa karibia kila siku
 
Mimi nitaelewa vizuri kama benki itakuwa inachukua bidhaa kiwandani na kuuza bei ya sokoni au kuagiza magari japani na kuuza bei ya showroom. Vinginevyo bado nitakuwa na mashaka.

Na vipi kuhusu huo mfumo wa kugawana faida huwa inakuwa kuwaje?

Mkuu....mashaka yako yatadumu kwa muda.mrefu sana ni kwasababu hujapata concept vizur. Muuzaji yeyote wa bidhaa anaamua viwango vya bei kulingana na factor mbalimbali...eg kalipa kodi, cost of fund ni kiasi gani, logistcs na vitu vingne. Hvo kusema bank iuze sawa na wakala wa beforwad itakuwa si sawa...maana befoward hakupi unafuu wa kulipa taratibu.

Kwenye kugawana faida ni rahisi tu..bank inafinance wazo la biashara wewe unachangia expirties na mambo mengine kwa jinsi mtakavokubalina. Sasa mtagawana faida na wakat huohuo wewe taratibu unanunua hisa au umilik ule wa bank kwenye hyo project ukimaliza bank inakuwachia. Ikitokea hapo njiani mradi ukafa basi bank inabeba hasara.
 
Sa faida Si Ndo RIBA

Faida = profit
riba = interest

Riba unalipa hata kama zile fedha hukufanyia biashara, na kila fedha ikikaa basi riba inaongezeka. Hiyo ni tafauti na faida, kwani mukishakubaliana faida ni shilingi ngapi basi haiongezeki.
 
Asante sana. Nikuweke sawa kuwa si kwamba unakichwa ngumu hapana. Iko hiv...lazma tukubaliane kuwa hapa sheria inayotumika hapa ni islamic...ambayo inatafsri mambo tofaut na common law au angalau kwa jinsi tulivozoea. Sasa basi kwa mujib wa sharia...hela siyo commodity by itself. Ni means of exchanging value of commodity. Kwa maana hyo huwez kumpa mtu hela halafu arudishe na nyngeza kisha uite faida...kwa mujib ya islamic law itaitwa riba. Kurejea mfano wa gari ...hapa shida yako si hela ni gari....ila muuzaji wa gari pale befoward anauza mil 10. Weww huna mil kumi ila kuna muuzaji mwingine anasema ntakuzia gari hilo hilo...ila ntaweka faida kiasi fulani. Huyu muuzaji wa pili anakwambia nafuu ntakayokupa ni weww utanilipa polepole...sasa hapo huwez kusema ni riba. Labda niulze swali unapoenda kununua kibiriti kwa mangi yeye kaweka faida tayri je utakuwa umelipa riba?! Bila shaka hapana. Kwhyo sasa fact iko hiv...kwa islm bank ni lazma pawe na mali katikati..si swala la pesa kwa pesa pekee.

Many practices of Islam are illogical. Kwa hiyo kununua kitu kwa 10mil na kumuuzia muislamu kwa 15mil ni hasara kuliko kumkopesha muislamu 10mil ili baadaye anirudishie 11mil pamoja na riba?
Muhamady kawaua sana hawa jamaa
 
Wao riba wameipooza makali ili wale hela za waislam,riba wanaita gharama za uendeshaji wa mkopo.
 
Many practices of Islam are illogical. Kwa hiyo kununua kitu kwa 10mil na kumuuzia muislamu kwa 15mil ni hasara kuliko kumkopesha muislamu 10mil ili baadaye anirudishie 11mil pamoja na riba?
Muhamady kawaua sana hawa jamaa

Asante sana. Riba ni halali kwa wasiokuwa na dini tu. Ukristo, Uislam na hata juadism unapinga riba kabsa....! Soma ndugu...soma...!
Ikumbukwe kuwa faida inayowekwa ni kitu pande mbili zinakubaliana kiwango. Na mtu anachoice yake. Riba itabaki kuwa riba na faida itabaki kuwa faida. Misingi ya uchumi wa marekani iliporomoka sana 2008 sababu kubwa ni kuwa ulijengwa katika misingi ya riba.
 
Ndio maana waislamu wanadanganywa karibia kila siku

Asante sana....naomba niulize swali dogo. Hiv kwann kijana wa miaka 17 akifanya ngona na binti say wa miaka 15 kisheria haisemwi kambaka...wakati huo kama kijana angekuwa na miaka 18 katika sheria angesemwa amebaka wakati tendo ni lilelile??
Au kwann wanandoa wakifanya ngono itaitwa tendo la ndoa na kinyume chake ni zinaa?! There is diff...that is a fact.

Nenda kwa wafanyakazi waulize waliokopa kwenye taasisi zinazochaji compaund interest then uje hapa useme kuna tofaut au lah!!
 
Sababu ni nyingi, kama vile unapomwagizia mchuuzi kesho akuletee samaki wakati ferry unapajua, au chinga akuletee kiatu aina fulani wakati vinapouzwa unapajua.
Vile vile, dalali hanunui ili akauze. Anachofanya ni kuwakutanisha muuzaji na mteja au umpe hela yeye akakununulie. Tofauti na anayenunua kwa pesa zake ili auze (anaitwa mfanyabiashara).

Tafauti na wanavyofanya hao wanaojiita Islami banking na machinga ni kwamba: Machinga huenda kununua bidhaa kwanza kabla ya hata kumjuwa mnunuzi wake lkn Islami banking wanasubiri mtu aje na shida zake ndio waende kununua halafu waje wamuuzie kwa gharama. Swali la msingi ni kwa nini hao wanaojiita Islami banking wasiwe na show rooms za magari wenyewe? kwa nini wasiwe na viwanda vya kufyatulia matufali vyao wenyewe? kwa nini wasiwe na maduka ya vifaa vya ujenzi vyao wenyewe? Hili swali linahitaji uelewa mpana na tafakuri ya kina. Inaelekea kuna ujanja ujanja tu ktk hizi zinazoitwa Islami banking. Mimi pia ni muislam lakini bado nina mashaka nazo.
 
Asante sana....hapa nadhan pana shida ya uelewa tu wa nadharia za islamic financial theories and practices...kwanza ieleweke kwanza bank zote zinaoperate kwa kutumia hela za wateja walioweka bank. Hvyo hakuna bank inaweza kutumia hela za akiba za watu kufungua maduka au viwanda ikiwa na matumain kuwa wateja watakuja...tizama bank zote...hawawez kufanya kitu kama hiko. Sasa dhana kwamba zina ujanja ujanja si kweli...chukulia mfano mkopo wa kuanzisha biashara say apartments. Hapa unaingia ubia na benk...bank inafinance wazo lako...wote mnamiliki na mnashare profit....lakin wakati huo wewe unakuwa unanunua umilik wa bank katka hyo project month by month..mpaka unapomaliza ....mie sioni tatizo hapo....labda ufafanue hasa huo ujanja uko sehem gan hasa maana kila kitu kinawekwa clear kabsa.

Kikubwa tusiitafsir dhana ya islamic banking kwa kutumia dhana ya convention banks.
 
Asante sana....naomba niulize swali dogo. Hiv kwann kijana wa miaka 17 akifanya ngona na binti say wa miaka 15 kisheria haisemwi kambaka...wakati huo kama kijana angekuwa na miaka 18 katika sheria angesemwa amebaka wakati tendo ni lilelile??
Au kwann wanandoa wakifanya ngono itaitwa tendo la ndoa na kinyume chake ni zinaa?! There is diff...that is a fact.

Nenda kwa wafanyakazi waulize waliokopa kwenye taasisi zinazochaji compaund interest then uje hapa useme kuna tofaut au lah!!

Kwa muislamu ukisema kitu kichafu kwa kiswahili unaitwa ------ na kitu hichohicho ukikisema kwa kiarabu unaonekana shujaa.......
Uislam is a very complicated ideology na hainaga logic
 
Asante sana. Riba ni halali kwa wasiokuwa na dini tu. Ukristo, Uislam na hata juadism unapinga riba kabsa....! Soma ndugu...soma...!
Ikumbukwe kuwa faida inayowekwa ni kitu pande mbili zinakubaliana kiwango. Na mtu anachoice yake. Riba itabaki kuwa riba na faida itabaki kuwa faida. Misingi ya uchumi wa marekani iliporomoka sana 2008 sababu kubwa ni kuwa ulijengwa katika misingi ya riba.

Mineno mbofu mbofuuu
 
Kwa muislamu ukisema kitu kichafu kwa kiswahili unaitwa ------ na kitu hichohicho ukikisema kwa kiarabu unaonekana shujaa.......
Uislam is a very complicated ideology na hainaga logic

This is very interesting argument....ilogical ideology according to who?! Nadhan kutokukubaliana na kitu hakukifanyi kitu kuwa logical au ilogical...fact remain tu. Chukulia mfano wa ndoa za jinsia moja...logic yake kwa baadhi ya watu haieleweki ila kwa mahakama kuu ya marekani inaeleweka...so logic au ilogical inategemea na umesimama wapi tu...nothing more or less.....! Hapa tunazungumzia kwa mtizamo wa sharia
 
Habari wana Jf.

Kwa mwenye kujua, ninaomba anifafanulie namna benki zinazoendeshwa kwa kufuata misingi ya kiislamu (Islamic Banking) zinavyoendeshwa.

Zaidi ni jinsi gani mikopo hutolewa na namna gani mikopo hiyo hurudishwa.

Ningekuwa karibu, ningeweza kutembelea matawi yao kupata ufafanuzi, lakini nipo huku Kyerwa mkoani Kagera. Na nilipopitia ktk website za mabenki hayo, ufafanuzi walioutoa sikuupata vema.

Nitashukuru kama pia nitapata msaada wa mchango kutoka kwa watu waliowahi kukopa katika mabenki yanayoendeshwa kwa taratibu za Kiislamu hapa nchini.

Nawasilisha.

Nakutakieni Baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhan ziwe juu yenu.

Kwa ufupi.

Bank hii ilianzishwa misri mwaka 1963, na Mitghar local saving bank.

Inafata misingi ya shariah (Quran, prophet Mohammed S.W na scholarly interpretation). na mambo yasiotakiwa katika bank hii ni riba, kamari na gharar.

Ukiangalia hii bank ni commercial bank kivitendo kuanzia kazi zake, leseni, na utaratibu wa pesa.

Ina changamoto kubwa ya neno riba, ambao usema faida (Profit), ukisikia maelezo yake ni riba tuu.

Wanahuduma kama..Murabaha, ijara, musharakah, mudarabah, Qard hasab, amanah, wadiah na salam...hizi ndio huduma utolewazo na bank hii....

Utafungua akaunti kama bank nyingine as saving n fixed (amanah) no interests, current (wadiah), mikopo wanayotoa ni kama, wanakunulia kitu labda gari (murabaha), wanakuongezea mtaji (mudarabah), wanajiunga pamoja katika business (musharakah), wanakuazima kitu (ijara) n.k pote hapa upewa let say Tsh 400,000/= unaambiwa utapata faida (margin profit) ya Tsh 100,000 upeleke 50,000 kwa miezi sita mfano, so unarudisha 450,000/= lazima faida ije.

Product moja tuu ndio wana share profit and loss Musharakah.

Hiyo ndio kwa ufupi tuu.

Zaidi nicheck nikueleweshe.

0715-011-406
 
Kweli ni raha sana....ila raha zaidi ni pale utakapoelewa hizi falsafa zinafanyaje kazi hasa...napendekeza hebu jarib kufanya kautafit kidogo....tu..halafu njoo ushare hapa....karibu

Mkuu nifanye utafiti gani tena hapo? Mimi mara kadhaa nimefuatilia credit policy ya KUTAYBA taasisi ile kiislamu. Nachelea kusema kuwa mmbo yanabadirika wakati,,na mifumo pia. Leo hii chini ya mfumo wa soko huria kilichokatazwa ndio kinachofanyika.
 
Asante mkubwa wangu...sina elimu na jinsi kutaiba inavofanya kazi...naomba uweke hapa hayo mapungufu au hicho unachodhan siyo sahihi then tukipime. Kimsingi mie nimekuwa nikijaribu kuzungumzia general principles za islamic banking.
 
Ndio maana waislamu wanadanganywa karibia kila siku

Riba sio biashara. Tehe tehe misaafu hii raha sana. Unanunua kitu 200 unauza 220 sio dhambi,ila ukikopa 200 ukirudisha 220 ni dhambi. etii tofauti ni kwamba hii ni riba ile ni faida ha ha ha.
aloycious, Jile79, MR UNINFORMED
Kawaida mwanadamu anajifanya mjuaji, lakini mambo yako wazi ! Biashara ina mabo mawili, 'faida' na 'hasara'
Biashara katika Uislaam inasimamia hapo, kuwa mna share faida au hasara. Lakini mtoza 'riba' yeye hawezi hata siku moja kukubali kubeba hasara, ndio maana anashikilia hati yako ya nyumba.

Mwenyezi Mungu anasema kuwajibu wale wasio amini na wanaoendekeza riba:

'Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zungwa na Shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwakuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara (profit and loss) na ameiharamisha riba. Basi aliyefikiwa na mawaidha (ujumbe huu ) kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia (kushiriki biashara ya riba hata kama nyuma huko aliwahi kufanya) basi yake ni yaliyo kwisha pita (amesamehewa) na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia (wabishi) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

Na Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. (ndio maana mabenki yana filisika !)

Enyi mlio amini (Waislaam) Mcheni Mwenyezi Mungu ! na acheni riba zilizo baki (compound) ikiwa nyinyi ni Waumini.

Basi mkifanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu (mkiacha) basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.

Qur'an: 2: 275- 279.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom