Msaada: Tumetapeliwa!

NEXT LEVEL-CRIME NAMPA SALUTE HUYO MWAMBA KUBLOCK ACCESS ZOTE HIZO NA KUCHUKUA PESA KIRAHIS..PIA POLE SANA MKUU.

TUWE NA SUBIRA ATAKUJA MJUZI MDA SIO MREFU KUELEZA JINSI ALIVO FANYA FANYA MPKA AKAFANIKIWA KUIBA HIZO HELA.
Huyo mwamba ni hatari.
 
Unacho kiamini sivyo ndivyo kilivyo unaweza ukaibiwa na bado hao cyber wako unao waamini wakabaki wameduwaa na wasimpate mhalifu hata kama namba wanayo
 
Nasikia mbinu wanayotumia hawa jamaa ni kwamba, Anapofika kwa wakala anauliza kama analo salio la kutosha. Baadaye anamwambia wakala nitumie fedha kwenye simu yangu, anataja namba. Lakini namba hiyo anayotaja anaikosea makusudi namba moja. Kwa wakala ambaye hayuko makini anatuma hiyo fedha. Baadaye yule mwizi anasikilizia taarifa ya kupokea fedha haifiki. Anaanza kulalamika. Anamwambia wakala; we kwani umetuma kwenye namba gani? Wakala anapoisoma hiyo namba, yule mwizi anamwambia umekosea namba ya mwisho. Yule Wakala anapojaribu kufuatilia muamala wake anakuta yule aliyemtumia ambaye ni mshirika wa yule mwizi anakuwa ameshaitoa na hivyo kujikuta hawezi kulipwa na yule aliyemwambia amtumie kwa sababu fedha hazikuingia kwake, ndiyo anakuwa kaibiwa tena.
 
HahahHh dah aisee kweli, haikuwa siku yako... Hao jamaa huwa wana mbinu sana, ukimpa mwanya tu basi story ita badilika
 
Hii tofautii...!!
 
Hahahah akili yako ni ndogo sana lengo sio jina lake,ukipata namba moja kwa moja umepata na eneo namba hiyo inatumika na unapata mawasiliano yake yote ya nyuma na njia zote alizotembea na hiyo laini
 
Unacho kiamini sivyo ndivyo kilivyo unaweza ukaibiwa na bado hao cyber wako unao waamini wakabaki wameduwaa na wasimpate mhalifu hata kama namba wanayo
Hahahah bongo hatuna hackers wa viwango vya juu ki hivyo ila wizi wa mtandaoni huwa unaacha ushahidi ambao ni rahisi kumpata tofauti na wizi wa nje ya mtandao
 
Utawapata wasiohusika huwajui vibaka wewe.
Tena unaweza kupata ndugu zako, si wanaenda na vinida vyao kusajili laini au hawaendi? Kama wanaenda hamna jambo mkae kwa kutulia tu
Unajua ile laini/chip ukiiweka kwenye simu tu ni tracker nzuri sana yaani kupitia hiyo mtu anaweza elezea safari yako ilianzia wapi na ikaishia wapi hata akiitupa huwa tunachora mduara kutoka laini ilipotupwa mpaka mhusika alipo na ile laini kama ashawahi itumia kwa matumizi yoyote ya kupiga/kupokea,text,internet taarifa zote zinapatikana
 
Huwezi fanya tukio la wizi au ujambazi kwenye simu usikamatwe labda wasikufuatilie tu,ndo maana magaidi hawatumii simu kufanya ugaidi
 
Hiyo ishu kwa polisi ni ndogo sana kama wakiamua wanamkamata

1)kuna laini aliyojiamishia pesa

2)kwa wakala aliyetoa hiyo pesa Mara nyingi matapeli wanakuwa na namba za mawakala wao akifanya utapeli tu anaitoa fasta

2)kuna simu aliyoitumia inaweza kusoma laini zote ambazo ziliwahi kuwekwa humo

Kwa kutumia hivyo vitu 3 polisi wanauwezo wa kumkamata huyo mwizi

Lakini utashangaa jinsi utakavyo zunguushwa ila kama angemtikana raisi fasta tu angekamatwa hii nchi bado sana
 
Ahahahaha boss haya mambo yetu ujue.
Huwezi kumkamata hata ufanye vipi huwa wanatumia stingrays ku-trace location ya simu n.k
.
Sasa mimi nimekuja na Nokia tochi OG moja ya simu zenye strong security ambayo ina laini yangu ya Vodacom niliyoisajili kiwizi kutoka kwa Ashura Justin bila yeye kujua nikaiba fedha zako nikajitumia nikaenda nikatoa fedha nika-block IMEI nikaitupa utanipataje?
 
Not easy as you think.
Inahitaji muda na kuna 95% ya kukamata wasiohusika na pengine wasiomjua kabisa.
.
Siku hizi simu used mitandaoni nyingi sana hata kwenye maduka ya simu mnauziwa simu used bila kujua!
 
Nilianza kuandika hapa ila nimefuta ila iko hivi hakuna assurance ya security ukiwa na kifaa chochote kinacho radiate EM waves, Yani ukiwa ndani ya network tu kuwa tracked down ni swala la muda na expertise ya wanaokutafuta, Ukitaka safety 100% Usitumie kabisa vifaa vya kielectronics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…