Teh mpendwa huyo hawezi kunirubuni bana
Hahahah mie nimetoa angalizo tu
Wee mlengeshe huyo mumeo kwanguu akuage yuko sfr alafu ahamie kama wiki uje kutufumaniaa tukiwa tunafanya tabia mbaya.
Habari za jumapili waungwana,
Kimya kingi kina mshindo mwingi....... iko hivi nataka kuachika. ..... sababu nimechoka. ( vituko vya pombe)
Vituko vimezidi nimekuwa nikiongea na tunayazungumza na mwenzangu ila anarudia yale yale. Nataka kusonga mbele niendelee na maisha maana kama kulia nimelia sana kama kuvumilia nimevumilia sana.
Msaada wako ni niambie nifanyaje au nitumie njia ipi niachike bila ugomvi bila mimi kuwa na mchepuko bila kumlipizia visa alivonifanyia. Pia sitaki kutoroka nataka nikiachika niondoke na mwanangu na si kuwa baada ya hapo ntaanza mahusiano mapya laah. Nataka nijitawale mwenyewe nifanye yale nnayotaka na kumpa mwongozo mzuri mwanangu aje kuwa mtu mzuri baadae.
Mwenzenu nimechoka nimechoka sitaki cha padri wala askofu wala maongezi ya familia wala kikao cha ukoo.
Naomba nisaidie ikiwezekana January nianze 2016 maisha mapya.
Ubarikiwe kwa maoni yako.
Pole sana kwa mtazamo ulionao, baba anarudi pombe kila siku, anakutukana na kukudhalilisha mbele ya mwanao halafu bado wafikiri kuwa kila uleapo, lazima malezi ya wote wawili? Nina rafiki ambaye akimfumania mumewe anapigwa na panga anashikiwa, watoto wanaona, hakuna hali ya kulinda wala kumsaidia mtoto hapo, MKUNDE wewe wajua maisha unayoishi, usijevumilia ukafa ndani ya nyumba, ataoa mwingine, fanya ambalo kwako ni jema ameshauri mtu hapo juu uwe na concrete reason nenda mahakamani fanya utakalo, jinsi gani utaishi baada ya talaka pia ni juu yako, fanya mambo sahihi, mtangulize Mungu, hata kwenye biblia talaka haikatazwi inakatazwa kuolewa tena.Mkunde Jina lako linaniambia Wewe ni DaDa Yangu kikabila Ingawa Sitaki kuamini Hivyo.
Ingawa Sipo katika ndoa lakini kwa Hili nitajaribu kukushauri kwa Kiasi nijuavyo. Mapenzi au ndoa ni Ya mke na mume na Hata ikitokea mikwaruzano Hukaa na Kuijadili kisha Kutafuta Suluhu na Hatimaye kumaliza Ugomvi.
Kutaka Kujitawala bila kujua Athari Zake ni kukosa Maono Ya Mbele Uendako... Usiongee kwa kuwa upo na uwezo wa Hilo lakini angalia ni Athari Zipi ambazo zitampata mtoto kwa kukosa malezi Ya Baba?
Kusema Kuwa Huna Mchepuko na Wala Hata Ukiachwa Hutaanzisha Uhusiano mpya hapo ni Kujitetea tu lakini watu wenye Akili zetu tunaelewa kuwa yupo ambaye ameshakushika Sikio na Unataka Kuondoka Ili Ukajitawale Kwa Huyo Mtu..
Lakini Kumbuka Thamani ya mtu haipimwi kwa kulipa ovu kwa ovu bali kwa wema..
NDOA NI
UVUMILIVU
KUJALI
KUTHAMINI
KUHESHIMU.
Kuwa Muangalifu Dada Usije kuruka mkojo ukakanyaga Kinyesi.
My dada BADILI TABIA hebu tulia basi.... usianze kuharibu hii great mission. Teh teh
End will justfy means....
Ukila na kipofu usimshike mkono..
exactly!....mpuuzi tu,afu eti ni mama!....linajifikiria lenyewe tu hili zuzu!
....kwenye ndoa tungekuwa tunahesabiana makosa,NANI ANGESIMAMA?!
Tanzania kungekuwa na 'no-fault divorce' ningekushauri uchukue mkondo huo.
Hapo huhitaji sababu ingine zaidi ya 'kumchoka' 'kutoendana' au kuwa na 'tofauti zisizoweza patanishwa'.
Huhitaji kuonyesha kosa alilofanya mwenza wako. Raha sana kwa kweli.
Ila kibongo bongo hapo itabidi utumie njia mbadala.
Jaribu hizi: acha kuoga na kujisafisha mara kwa mara; acha kupiga mswaki; acha kujiremba na kujipodoa; acha kunyoa kwapa na kule sehemu sehemu; acha kupaka deodorant na kiachie kikwapa kiteme harufu kali.
Kwa kifupi, kuwa mchafu halafu uone kama yeye hajakuacha.
MMMMhn,mie napita manake mwenyezi mungu hapendi watu waachane....
Wanawake wa kabila/lugha hiyo kwenye red wakishaona wameanza kujiweza kimaisha huanza vitimbi vya kutaka kuachika. Hatushangai kwa uamuzi wako huo. Ni dhahiri mumeo kuwa mlevi ni wewe unamfrustrate. Bahati mbaya huyo jamaa yako si mchaga mwenzio ndiyo maana hata mazungumzo naye wala na jamaa zake wala na viongozi wa kanisa lake huyataki.
Teh movie hamna mpendwa, starring kafa hata kabla ya mpambano
Teh twajuana kwa vilemba yakheHahaaaa hao ni waarabu wa pemba BADILI TABIA
Mbona umesahau nyepesi ambayo inawezekanika, usimpe unyumba ama kama hakupi unyumba kwa zaidi ya miezi kadhaa waweza tumia hilo kuomba talaka maana umechoka kuishi kama kaka na dada, ama mnyime akuchoke akuache.