brenda18
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 5,687
- 5,297
Babu nawe uzee utakuletea shida sasa, nilisema sababu kuu ni nimechoka. Kwenye mabano nikaweka visa vya pombe nilimaanisha alcohol na si the elected president.
Nataka kuachika kwa kuwa nimechoka sitaki tena kusuluhisha. Maana hayo nilishayafanya sana ila anarudia makosa yale yale yaani ni mfululizo wa visa.
Ngachokaa mbee na ndo hapo nataka nifanye kitu kimoja tuu yeye mwenyewe aseme sikutaki tena.
Mahakamani atanishinda na pesa zake after all hata akisema nguo zangu niache ntaacha maana sihitaji pesa yake wala mali yoyote niliyochuma nae wala mali niliyochuma kabla sijaolewa vyote namuachia. Nataka mwanangu tuu basi nikaanze upya.
Nikisema nimechoshwa na visa mjue nimechoka kwelikweli.....
Natamani kujua ni visa gani hivyo umevichoka kiasi hiki mpaka unaomba kuachika,kweli pesa si kila kitu😢😢