Msaada: SMS ninazochat na mwanafunzi zimekamatwa

Msaada: SMS ninazochat na mwanafunzi zimekamatwa

Kwa mara nyingine tena Adamu wa morogoro kalishwa tunda.
Subiri kufukuzwa edeni, mamaeee.
 
Habarini wadau.

Mimi ni baba wa familia ya mtoto mmoja na mke ambaye tunapendana sana. Pia Mimi ni mwalimu mpya wa shule moja hapa jiji kasoro bahari nina kama miezi mitano (5) hapa shuleni ila naona muda wowote naenda kufukuzwa.

Kisa chenyewe.
Mwezi huu mwanzoni kuna binti wa kidato cha tatu alinifuata ofisini jioni na maswali kadhaa ya somo ninalofundisha. nikamuelekeza kwa muda baadae anavyoondoka akasema anaomba namba yangu akawape wazazi wake pindi watakapomuuliza kwanini amechelewa kurudi home, nilikubali maana sikuona unayaendeleza wowote, usiku WA saa 4 hivi nikapokea message nyingi zikijitambulisha ni yule binti nikachukuliwa kawaida tu na nilimjibu kawaida maana wife alianza kuchukia so nikaacha kuchat.

Ila yule binti hakukoma aliendelea na siku moja usiku alinipigia nikiwa kwenye bia kupunguza mawazo,, alivyonipigia nadhani aligundua nimelewa akaanza kunichombeza ingawa sikuwa nimelewa sana ila nilishindwa mkataa pindi aliponiambia ananipenda maana kilakotu nilijibu sawa mpaka alivyokata simu.. Siku yako Pili asubuhi ndo nikakumbuka kama aliniambia vitu vya ajabu nikajilaumu sana na kabla sijatoka nyumbani kwenda kazini akatuma message yenye maneno ya mahaba sikumjibu.

Baada ya siku kadhaa nikajikuta nachat nae kuhusu mambo ya mahaba, ingawa sikupanga kuonana nae kwa namba yoyote.

MSAADA NINAOTAKA.

juzi usiku nilitumiwa message nyingi kwa namba ngeni nilivyojibu ndo akawa anasema baba ake ameona message amempiga haswa na anampango wa kuja shuleni kesho, wadau Msaada wenu muhimu je nifanyaje Wakuu na nijiteteaje?

Asanteni
Sasa unataka ushauri gani? Muhimu nenda police sema mwanafunzi alitaka kukubaka basi...jamhurii inaweza kukupunguzia adhabu kwa kua ni kosa la kwanza la huyo mwanafunzi kutaka kukbaka!
 
Kuna mwenzako wa mum alikuja field/ipt kibaha, kampa mimba Mwanafunzi wa Form I! Mwambie ajiandae, bint ameshamtaja!
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Kwahy kwenye kuchat alikua anakuita mwalimu nanii na amekusave mwalimu naniii?
Au alivyouliza ndio kakutaja
 
Mfate huyo mzee muombe radhi, hata akitaka hela mpe, au nenda hata na vilaki mbili au tatu muombe radhi, mwambie wewe ni binadamuuu, ni shetan tuu alikupitia, pls usipuuze ushaur huu mfate mzeee kabla, kesho haijafika,
 
Mfate huyo mzee muombe radhi, hata akitaka hela mpe, au nenda hata na vilaki mbili au tatu muombe radhi, mwambie wewe ni binadamuuu, ni shetan tuu alikupitia, pls usipuuze ushaur huu mfate mzeee kabla, kesho haijafika,
Mkuu mzee mwenyewe anamaisha mazuri sana kiasi kwamba hizo laki 2 ni ndogo sana na ni Don sana kiasi kwamba nikimfuata naweza kuangamia
 
Apo mzee Fanya kumfuata mkuu wa shule kueleza kisa kizima afu mbadilishie kesi uyo dg Kwamba anakutaka leo hii aandikiwe baba ake barua Kwamba mwanae anamakosa ya kinidhamu gemu kwisha asubuh j3 aletwe mbele ya shule nzima na ueleze tabia yake bila ivo utakuwa umekwisa......... .......... Hii mbinu nilimpa rafiki angu na alishinda kila La heri..........afu Kumbuka usifute wala kuficha message yoyote ile..... Utaumbuka ........over
Acha kumpoteza.Anakwambia alikua ana chart nae.sms zitamfunga.Cha msingi angeweka hio charting humu.All in all mchawi pesa.Mtafute mzee mkae muyazungumze.mtwange bahasha ya pesa kama kiomba radhi.yatakua yamekwisha na utaendelea kumbonya mwanafunzi wako mpaka utakapokula 30yrs jela
 
Pole sana kaka nakuhakikishia Hakuna kitakachokupata kazi hutapoteza wala Familia haitaharibika, chakufanya sasa nenda kwa mzazi kamwombe msamaha sana mbembeleze. Ukimaliza kama mzazi reaction yake bado mbaya nenda kwa mkuu umweleze ulipofikia. Atakushauri cha kufanya.
Ushauri wangu acha pombe
Acha uzinzi wadogo
Maana najua it's not your first time Mungu amekuonya maana Mungu hatoi adhabu bila onyo usiposikia utafungwa.
 
Kuna shauri mbili tu hapa za kukuokoa endapo utafanikiwa ktk kuzifanyia kazi. 1. Kuna jamaa amesema ukaongee na Mkuu ili dogo apewe msala kwamba alikshawahi kukusumbua kwa kukutaka

2. Kuwahi kuongea na Mzazi na kumuomba radhi huku ukimuweka wazi mazingira yote ya huyo denti.

NB: hiyo ya kwanza ikitiki inamaliza yote kwa kiasi kikubwa sana
 
Acha kujidharirisha na kimshusha mkeo alafu mbona siku hizi hamuheshimu maagizo ya Mungu juu ya ndoa.
 
MKUU NIMEGUNDUA HIVI VITU

-Huyo denti ulishawahi kumtafuna(umepindisha maelezo)

-Ulimkubali kwa utashi wako ila unaisingizia POMBE ili tukuone hukukusudia wakati mlichati kimahaba ukiwa mzima kabisaaa(TUOMBE MSAMAHA WALEVI)

*Ungeongea ukweli wote na txt mlizokua mnachati tungejua namna nzuri ya kukusaidia kukwepa msala wako

1:sikurupuke mkuu ongea na huyo mzee mwambie huyo binti alichukua namba zako na alikua anakutafuta kama mwanamke mwingine na hukujua kwamba ni mwanafunzi wako pia uwe mkali usioneshe uoga wowote

-NENDA KWA MKUU WA SHULE MUELEZE HALI HALISI PIA MUOMBE AKUSAIDIE MAMBO YAISHIE OFISINI HUYO MZEE AKIJA MUYAMALIZE ILI AFICHE AIBU YAKO


*KILA LA KHERI*
 
Kosa kubwa ulilolifanya Ni kujibu sms vile ye anataka hapo ndo patafunga na wala haitakumbukwa kwamba aliomba namba ili awape wazazi wake,
Ni herii hata ungemweleza mke wako,, kubaki kimya inamaanisha ulikuwa na mpango wa kufanya nae mapenzi
USHAURI
1. Kama unaipenda kazi nenda kawapigie magoti wazazi wake, kamwage swagaa wakelewe
2. Kama unataka uwasubirie nenda kaongee na mwalimu mkuu, ikiwezekana mwanafunzi atishiwe kufukuzwa shule kwa kumiliki simu na kuitumia kuwatongoza walimu, hii itawafanya wazazi washuke na kukubali kukaa
mezani
3. Ukipona hapo hama kabisa hapo shuleni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom