Msaada: SMS ninazochat na mwanafunzi zimekamatwa

Msaada: SMS ninazochat na mwanafunzi zimekamatwa

Baba Moreen

Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
82
Reaction score
110
Habarini wadau.

Mimi ni baba wa familia ya mtoto mmoja na mke ambaye tunapendana sana. Pia Mimi ni mwalimu mpya wa shule moja hapa jiji kasoro bahari nina kama miezi mitano (5) hapa shuleni ila naona muda wowote naenda kufukuzwa.

Kisa chenyewe.
Mwezi huu mwanzoni kuna binti wa kidato cha tatu alinifuata ofisini jioni na maswali kadhaa ya somo ninalofundisha. nikamuelekeza kwa muda baadae anavyoondoka akasema anaomba namba yangu akawape wazazi wake pindi watakapomuuliza kwanini amechelewa kurudi home, nilikubali maana sikuona unayaendeleza wowote, usiku WA saa 4 hivi nikapokea message nyingi zikijitambulisha ni yule binti nikachukuliwa kawaida tu na nilimjibu kawaida maana wife alianza kuchukia so nikaacha kuchat.

Ila yule binti hakukoma aliendelea na siku moja usiku alinipigia nikiwa kwenye bia kupunguza mawazo,, alivyonipigia nadhani aligundua nimelewa akaanza kunichombeza ingawa sikuwa nimelewa sana ila nilishindwa mkataa pindi aliponiambia ananipenda maana kilakotu nilijibu sawa mpaka alivyokata simu.. Siku yako Pili asubuhi ndo nikakumbuka kama aliniambia vitu vya ajabu nikajilaumu sana na kabla sijatoka nyumbani kwenda kazini akatuma message yenye maneno ya mahaba sikumjibu.

Baada ya siku kadhaa nikajikuta nachat nae kuhusu mambo ya mahaba, ingawa sikupanga kuonana nae kwa namba yoyote.

MSAADA NINAOTAKA.

juzi usiku nilitumiwa message nyingi kwa namba ngeni nilivyojibu ndo akawa anasema baba ake ameona message amempiga haswa na anampango wa kuja shuleni kesho, wadau Msaada wenu muhimu je nifanyaje Wakuu na nijiteteaje?

Asanteni
 
Nani atatusaidia watoto wetu, nyie walimu ndo tunaowaamini matokeo yake ndo haya sasa!

Kabla hujaanza kuchat na wanafunzi mfikirie!Moreen, ungependa nae apitie hayo unayompitisha huyo mwanafunzi?!
Kama sio, jiadhibu kabla hujaadhibiwa!!

Wazazi mmeona, tujitahidi sana kuwapa watoto wetu malezi yenye hofu ya Mungu jamani, tusisahau kuwaombea hawa watoto!
 
Baba Moreen, Yaani sijui kama itasaidia.

Ila fanya hivi we sema kwamba ndioo huyu mtoto alikuja, akaomba namba na akasema anawaletewa ninyi wazazi wake.

Ila baada ya hapo ulipigiwa simu na mdada mtu mzima akajitambulisha na,akasema namba ali mtuma mtu aje kuchukua kwangu na si kumuuliza ni nani maana namba una gawa hovyo sasa ukawa unachati nae mara kibao.

Ila kila ukimwambia muonane hataki. Ndo ikabidi niwe na chat nae kawaida tu.

Ila kiukweli sikujua kama ni huyu mtoto maana huyu mara ya mwisho kuonana ili kuwa ni ofisi na alikuja na maswali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom