Msaada: Sidhani kama nitakuja kuoa, nimeathirika na suala hili

Msaada: Sidhani kama nitakuja kuoa, nimeathirika na suala hili

Jipe muda wakujitafakili wapi umekosea ili wakati ujao usitoe nafasi ya kugongewa kirahisi.
baada ya Hilo tukio kama limekuumiza na umeamua kuingia kwenye mahusiano mapya basi jipange kisaikolojia na uamini kwamba hakuna mwanamke wa peke yako, tofaut na hapo basi tafuta mwanamke ambaye ataoa future kwaajili ya kizazi chako kijacho zaanae mtunze kama mke lkn ajue kabisa anapata huduma Zote kasoro kupata ndoa., hili litakufanya uishi kwa kujiamini kwamba Dunia ni mahali salama wakati huo unaendeleza uchunguzi wakina kuhusu huyo mwanamke ukiona anakufaa basi utampa zawadi ya ndoa, ukumbuke kwamba mwanamke anaweza kuigiza hata miaka 10,tuangalie machimbuko ya Familia zao pia ili tusije kulalamika.
 
Wajomba!
Ambao hatujaingia kwenye ndoa please jitafakari mara 10 kabla hujavaa pete na kusaini vyeti uchwara.

Nimeathirika na tukio 1 ambalo kiukweli nimejitahidi sana kulitoa akilini ila mara zote nikikumbuka tu ni kama limetokea jana.

Ipo hivi mwaka fulani hapo nyuma nilikuwa na mwanamke niliyempatia promises zote za ndoa na kumuamini na kumtengeneza kuwa mke wa maisha yangu na familia yangu.

Najua kosa langu lilikuwa ni kumuaminisha kuwa yeye ndio chaguo langu pekee na hakuna mwingine, kifupi nilimpa uhakika wa ndoa na niliwekeza kwake, kosa la pili.

Alijiweka sawa kwenye mahusiano na mara zote alikuwa clean na msiri sana, kila kitu alikipangilia vilivyo hadi pale nilipomkamata anacheat na jamaa mwingine na bahati mbaya au nzuri nilianza kuona viashiria ila nikajipa muda na kumuacha wenda atajirekebisha, "kosa la tatu hilo."

Mwanamke alicheat hadi akapata mimba na kibaya rafiki yake ambaye alikuwa naye muda wote walifanya mpango akatoa ile mimba na wakati huo nilikuwa safarini kikazi basi alinidanganya kuwa anaumwa sana malaria,Amiba na mengine basi nikatuma pesa ya matibabu akaendelea kupona taratibu.

NILIMKAMATA VIPI?
wajomba, kuna siku simu yake iphone ilianguka chini ikazima ghafla nikiwa naye basi nikaipeleka kwa fundi kutengeneza, hakuwa na mashaka sababu kila kitu ameficha na sms zote huwa anafuta, simu iliwaka nikatoa lock then nikawa nacheki vitu normal tu hadi nilipoenda kwenye sms, sikuona kitu cha maana sana pale maana sms zilikuwa nyingi ila hazikuwa zikionesha mashaka.

Wakati naenda home nikapata wazo nipitie sms za rafiki yake ambaye yupo naye muda wote na wanaitana "Girlfriend" wakuu humo ndio nilikuta uchafu mwingi sana wakipeana details za mwana kuja kumkamia demu wangu kisha wampe muda jamaa then aje amkamue yule manzi mwingine...wakuu mimba ikaingia wakamuambia jamaa kisha wakaenda kuitoa kisiri sana bila mimi kujua.

Wajomba nilikuwa naendesha gari na AC kali sana ila nilijisi joto moja la hatari sana nikapaki pembeni kufikiria cha kufanya, wakuu nilifika kwangu nikampatia simu nikiwa normal tu sikuwa na shida ila siku hiyo nililala kama mpumbavu.

Kufupisha story.
Nilimkaushia sikumuambia lolote siku ile, nikasubiriq siku nimemtoa kwenda beach pahali ndio nikamuomba anieleze nini kilimfanya anifanyie ukatili ule, alilia sana akiomba msamaha, alichanganyikiwa pale kila mtu aliona kelele tu mwanamke akilia kama kuna msiba, haikuwa rahisi mimi kumbembeleza nilimuacha hadi akatulia mwenyew, nilimchukua tukarudi home akiwa hajielew na full misamaha, nikienda kazini simu zinakuwa nyingi sana za misamaha na kujutia alichofanya.

Nikampatia nafasi amrudie yule jamaa wakafanye zaidi kwa uhuru nisiwasumbue kwa namna yoyote ile.

Majuzi nimejipatia mwanamke kutoka kwa family friend na kila kitu kinaenda sawa na ni mwanamke msafi na poa sana ila nikikumbuka yale matukio basi moyo wangu unakuwa mgumu sana kukubali masuala ya ndoa, nashindwa nini cha kufanya yaani kifupi sijui hatima yangu mbele kwenye masuala ya ndoa itakuwaje na sielew nifanye nini wajomba naombeni ushauri.

NAOMBA USHAURI NINI NIFANYE ILI NIPONE WAKUU NATESEKA SANA. 🙏🙏
Simp......ukiwa simp wanawake watakutumia sana na hawatakuonea huruma kamwe.
 
Ilitakiwa siku hiyo mmetoka beach, ndio siku hiyohiyo anaondoka.

No, ,no ilitakiwa siku ile umesoma sms ndio anaondoka.
 
Achana na mpango wa kuoa mwanamke wa kutoka family friend, ukiwa na uwezo wa kuchimba kizazi chake kwanzia mababu labda nje na hapo utajuta
 
Kumbe hata haukuoa hivyo usiunganishe wote kwa matendo ya mwanamke wako maana hayajakushinda bado yangekushinda usingeingia mahusiano mapya
 
"Wajomba nilikuwa naendesha gari na AC kali sana ila nilijisi joto moja la hatari sana nikapaki pembeni kufikiria cha kufanya"

Ulikua unadrive huku unaperuzi dereva au sio......

Matendo ni mawili tu kuoa au kuolewa mengine utachagua mwenyewe
Nami nilitaka niulize hilo swali. Utunzi nk kipaji ujue!

Nakazia "Its either uoe ama uolewe".
 
Usimuamini sana mwanamke hata kama hakucheat, we usijiaminishe sana et ni wako pekeako utaishi maisha marefu sana.
 
Wanawake wema na wenye sifa zote za kuitwa mke wapo tele! Pole kama hujapata bahati ya kumpata wa hivyo! Ila mpaka mwanamke wako analiwa na kutiwa mimba nje na wewe jitafakari mkuu!
 
Wanawake wema na wenye sifa zote za kuitwa mke wapo tele! Pole kama hujapata bahati ya kumpata wa hivyo! Ila mpaka mwanamke wako analiwa na kutiwa mimba nje na wewe jitafakari mkuu!
Huwez kumlinda mzee hizo nyuchi zikiamua kuliwa haziangalii nyuma
 
Au kwa lugha nyepesi niseme Subiri kama mwaka hivi
 
Back
Top Bottom