Msaada: Pete ya ndoa imetumbukia chooni

Msaada: Pete ya ndoa imetumbukia chooni

Huwaga inapwaya nikiwa naogaga ila ktk mazingira ya kawaida huwa ipo tight. Na pia huwa naivuaga nyakati za kuoga ama kufua kwa kuifanya isifubae

Hiyo tabia ya kui put on and off ndo hupelekea kupotea mara nyingi!
Ukute uliisahau bafuni Kama kunaingia watu wengine ambao si waaminifu wanaiiba kimya kimya !
Katengeneze ya kukutosha vizuri isikupwae wala kukubana Hata unaposhika Maji Au mapovu!
Hilo linawezaekana kabisa!
Hayo mambo ya kusema itapauka binafsi sioni Kama yana msingi wowote,
Zikipauka pelekeni kwa sonara mkasafishe na siyo kuvua wakati wa kuoga Au kufua na kisha kuvaa tena!
Kwa mwenendo huo utakuwa unapoteza mara kwa mara !
 
Not big deal,ndoa sio pete ni maisha yenu mtakavyoishi nyinyi wawili kwa maekewano na masikilizano, the rest ni cosmetics zisizo na ulazima, so forget about it
 
Habarini wana jamvi.

Naombeni msaada pete ya ndoa imetumbukia chooni na imeshaflashiwa.

Je kuna namna ya kuweza kuipata. Leo ni siku ya 06 tangu tukio hilo litokee.
nenda ufungue kwenye chemba 1 inayopokea uchafu ndio iingize kwenye main chamber ukikosa fungua mifuniko yote ya kabla ya kufikia chamber 1 halafu angalia humo ukikosa weka mtu mmoja mmoja kwenye kila mfuniko halafu flash maji mengi kutoka kwako atakayeiona inateremka ataichukua. all the best
 
Dah inaniuma sana. Ilikuwa nzuri na ya gharama sana..
Ya gram ngapi? linganisha gharama ya kutengeneza nyingine na gharama ya kumweka kibarua wa kuitoa. itakuwa katika shimo ndogo tu ya choo, hivyo unamtafuta mtu kuzibua choo. ni rahisi sana tu, anafunuia mfuniko, anatoa uchafu wote. Pia unakuwa umaefanaya kazi mbili kwa mpigo, ya kutoa pete na kusafisha chemba.
 
kama ina gm 2 na kuendelea hata usipoitoa wanaume wakijua wataitoa fasta na vyuma vilivyokaza maana hiyo thamani yake kwa sasa bila shaka siyo chini ya kilo moja na nusu.
 
Kama umeshindwa kuiweka ndoa akilini, hata kidoleni haitakaa kamwe!
 
Kama imetumbukia chooni kwako haina shida, tafuta nyingine...

kama imetumbukia ukiwa na mchepuko maeneo, Karma itakutafuna...


cc: mahondaw
 
Tafuta nyingine kama hiyo iliyopotea unaipeleka Kanisani unamweleza Baba Paroko hali halisi anaibariki, siku nyingine ukumbuke kuivua pale inapohitajika kuvuliwa.
 
Wanaume wa siku hizi sijui tumekuaje yani mada za kijinga nyingi tunaanzisha sisi!.. Kapotelewa na pete analeta uzi eti MSAADA sasa tuje saidia nyonya uchafu chooni.
 
Back
Top Bottom