Msaada NSSF - nahitaji kupata hela zangu

herman3

JF-Expert Member
Feb 7, 2015
509
659
Habarini ndugu JF.
Mimi ni kijana ambaye nimemaliza mkataba kwenye shirika ambalo nilkuwa nikifanya kazi. Katika kufuatilia nilijulishwa kuwa kwa mtu mwenye elimu kama yangu "certificate" anaruhusiwa kupata pesa zake zote na sio 33.33%, Hivyo nilijaza fomu zote na kurejesha nikitarajia kwamba nitapokea pesa zangu zote. Lakini matokeo yake wananipa 33.33% (mwezi wa kwanza kupewa ni November 2023).
Hivyo, nimekuja hapa kuomba ushauri nifuate hatua gani ili kuweza kukata rufaa au kupata ushauri wa namna bora ya kushughulikia changamoto yangu.

Ahsanteni
 
Kwanza unachukua maokoto yako yote Ili ufanyie nn?Usikute unapalilia penzi Kijana?Halafu hayo ni mafao ya uzeeni,wewe unataka utumbue sahizi Ili uzeeni uje kutukana Kila mtu sio?
 
Nimecheka Sasa sema we jamaa ni TAPELI.Hela zetu hamuwezi kutupa uzeheni ,Hela ya kutumbua ujanani ni tamu bhana
 
Kwanza unachukua maokoto yako yote Ili ufanyie nn?Usikute unapalilia penzi Kijana?Halafu hayo ni mafao ya uzeeni,wewe unataka utumbue sahizi Ili uzeeni uje kutukana Kila mtu sio?
Kila mmoja na mipango yake, wengine wakati tupo kazini tulikuwa na vibiashara, sasa kazi imekwisha ni muda wa kupata maokoto yangu, niongeze mtaji wa biashara. Huko uzeeni nitaishi vizuri kama nitawekeza kwenye biashara nikiwa bado kijana. Thamani ya hiyo pesa uzeeni haitakuwa sawa na nikiiwekeza umri huu.
 
Habarini ndugu JF.
Mimi ni kijana ambaye nimemaliza mkataba kwenye shirika ambalo nilkuwa nikifanya kazi. Katika kufuatilia nilijulishwa kuwa kwa mtu mwenye elimu kama yangu "certificate" anaruhusiwa kupata pesa zake zote na sio 33.33%, Hivyo nilijaza fomu zote na kurejesha nikitarajia kwamba nitapokea pesa zangu zote. Lakini matokeo yake wananipa 33.33% (mwezi wa kwanza kupewa ni November 2023).
Hivyo, nimekuja hapa kuomba ushauri nifuate hatua gani ili kuweza kukata rufaa au kupata ushauri wa namna bora ya kushughulikia changamoto yangu.

Ahsanteni
Ushauri wa Bure kama unauhakika unacho kiandika haudanganyi nakushauri ukaandike barua ya kukata shauri na uwe na vithibitisho kweli wewe sio mtaalam, lakini kama hauna uhakika wa hilo unataka mseleleko basi usifanye hivyo jamaa wapo smart sana wale mifumo yao inasomana. So akili kichwani mtu wangu
 
Back
Top Bottom