NSSF ni utapeli kama Kalynda na Forever living, tushirikiane kuutokomeza

Restless Hustler

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
4,742
17,986
Naomba tujadili UBABAISHAJI wa NSSF.

Mtu umefanya kazi alafu unalazimishwa kuwekewa akiba. Siku mkataba wa azi ukiisha, tunaandika barua ya maombi ya pesa zako zilizopo kwenye mfuko wa NSSF.

Hao NSSF wanakuambia "subiri tukachakate maombi yako"(yaani hela yangu niliyojinyima nikaweka akiba leo ni maombi kulipa)

Baada ya miezi 3 unawekewa 33% ya monthly basic salary yako kwa awamu sita tu. Hela nyingine iliyobaki NSSF haitoki tena, utaambiwa "utafute ajira ili tukukate hela nyingine tukutunzie ili tukupe uzeeni"

Maswali ya kujiuliza:

1. Kwanini nilazimishwe kutunziwa Akiba wakati naweza kutunza mwenyewe kwa njia mbalimbali ikiwem UTT, dunduliza account, TANESCO Sacco's etc?

2. Kwanini utaratibu wa kupata hela yangu iliyoshikiliwa na NSSF ni mrefu wakati ule sio mkopo Bali ni pesa zangu halali?

3. Kwanini baada ya mkataba wa ajira kuisha sipewi akiba zangu zote, nalazimishwa nikatafute ajira nyingine ili niendelee kuchangia NSSF, je kama nimeachana na kuajiriwa nitalazimishwa nitafute ajira?

4. Kama hiyo ni Akiba, kwanini Ina makato badala ya riba?

Hoja ni nyingi, Ukiuliza unaambiwa ipo kwa mujibu wa Sheria. Sasa Sheria Gani hii ya kuleteana umaskini?

Karibu kwa mjadala
 
N

Na kwa sisi tusio na ajira unatushaurije?
 
Back
Top Bottom