Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

It's hard to trace its fons et origo. But since the human mind is capable of imagining things and coming up with fairy tales, it is no surprise to me that that is perhaps where (the mind) it started.

Just ask yourself, do leprechauns really exist? What about Santa?



Simulizi na maongezi.



Kwa vile ni vigumu sana kufuta ujinga ndo maana bado hata hivi sasa wapo watu wanaoendelea kuamini hayo mambo kichawi.

Na mara nyingi watu wakiwa hawana majibu ya jambo au tukio fulani basi default sababu huwa inahusisha mambo ya imani, iwe uchawi au dini (mungu).


Hebu yasome tena maswali yangu vizuri kwa kuyatafari kwa kina halafu ukiona unaweza kuyajibu ndiyo uje kujibu..ila usiyasome ili uyajibu tu kama unafanya mtihani wa shule ya msingi.
 
dawa ya mchawi ni Jina la Yesu.Marko 16:17-18,Yohana 14:14,Matendo 3:6.omba kwa hilo jina kwa imani,uone timbwili atakalolipata huyu mama.
 
Yaani wewe umeamua kuweka masharti kwenye maombi. Duh.

Hivi unajua Yona aliomba akiwa tumboni mwa samaki katika ukaidi wake na akaponywa? Na kuokoka ni nini? Unless awe analiitia jina la Yesu huku haamini kama ni mwokozi

Thibitisha kwamba habar hizo ni za kweli!.Sasa mtu aombe akiwa ndani ya tumbo la samaki we umejuaje?.
 
Hatutapata majibu kwa sababu hakuna majibu. Hakuna majibu kwa sababu hakuna mungu.

Mtoa maada anahitaji msaada.

Anahitaji msaada wa elimu.Elimu ya kuelewa kwamba uchawi ni stories tu, na anko wake anaweza kuwa kafariki kwa cardiac arrest au ugonjwa mwingine tu unaoweza kumuua mtu ghafla akiwa katika mshtuko/mabishano yanayoweza kumhamanisha mtu.

Nimeuliza hapa, wanaokimbilia kusema habari za uchawi hata post mortem wamefanya?

Sijajibiwa.

Afrika tunashindwa kuendelea kwa sababu za kuendekeza ujinga kama huu wa kuamini mungu na uchawi.[/QUOTE

Mkuu, kama sijakosea, kunasehemu umeuliza "uchawi ni nini" Cha ajabu nashangaa unapinga ambacho hujui ni nini.
Pia hii thredi haijazungumzia anko kufa, ila wewe umekurupuka na kuongelea ishu ya anko kufa.
 
ha ha haaah! ss mkuu risasi na kombora la uyo mama citageuzwa maji:smile-big::smile-big:
 
Kuna ishu imenikumba juzi kati wakati nilipokuwa nafuatilia shamba la mzee wangu kwa ajili ya kulifanyia mchakato wa kulisafisha.
Kufika huko nimekutana na kitu tofauti na matarajio yangu.Yaani shamba limemegwa na mama mmoja na taarifa zikadai hajauziwa ila amekuja kuvamia.

Nilichokifanya nilimchukua anko wangu tukaanza kumtafuta huyo mama bahati nzuri tulikutana naye njiani siku moja.

Anko alipomuhoji kwanini amevamia eneo sio lake hakutujibu badala yake alimrushia anko jini akabaki anagalagala chini na yule mama akaondoka zake mpaka sasa anko kapooza na shamba limemegwa na nikiangalia msimu wa kilimo umekaribia.Je nifanyeje wadau ili niweze pata haki yangu.
N.B

Shamba lina hati zote ila uchawi tu ndio unanitisha.

Mkuu achakuamini nguvu zagiza utkufamasikini nenda mahakamani kadaihakiyakokamakweli unauhakika kwamba shamba in lenu na sio bla bla bla.
 
Uhm ulijuaje kama amemtupia jini? Ulishuhudia...kama ulishuhudia kwann haukuchukuwa hatua zozote na kwa maneno yako inaonesha ww ni mzima!
 
jibu rahisi sana njoo Ngende au Pemba ndiyo makao makuu ya uchawi wa kijini upate dawa yake kama hutaki acha kabisa hilo shamba maana utakufa tu.
 
jibu rahisi sana njoo Ngende au Pemba ndiyo makao makuu ya uchawi wa kijini upate dawa yake kama hutaki acha kabisa hilo shamba maana utakufa tu.
Ahsante mkuu nita tafuta nauli ya kuja huko
 
Mamlaka na power ya kujiongoza hana....
Ubongo wa mtu hauna uwezo kupanga yajayo katika muongozo wa kuishi ulimwenguni..
Labda uwezo wa kuongoza milango ya fahamu tu..

Hujajibu maswali.

Hilo, hata kama litakuwa kweli, halithibitishi kwamba uchawi upo na si stories tu.
 
Mkuu, kama sijakosea, kunasehemu umeuliza "uchawi ni nini" Cha ajabu nashangaa unapinga ambacho hujui ni nini.
Pia hii thredi haijazungumzia anko kufa, ila wewe umekurupuka na kuongelea ishu ya anko kufa.

Ni vizuri kwamba umeanza kwa kuandika "kama sijakosea". Kwa sababu umekosea.

Mtu kuuliza "uchawi ni nini?" haimaanishi automatically kwamba hajui uchawi ni nini. There is such a thing as "the Socratic method". Read a little.

Ni muhimu kufanya hizi basic definitions. Kwa sababu mtu mwingine anaweza kusema mtu atakayekupulizia unga wa ricin na kukuua ni mchawi, wakati huyo si uchawi, hiyo ni chemistry tu.

Ili kuepuka mabishano ambayo hata hayazungumzii kitu kile kile, ni muhimu kudefine mambo.

Duniani kuna watu wabaya wanaotaka kuua wenzao? Naam.

Watu hao wanaweza kumpa sumu mwingine afe? Naam.

Duniani kuna watu wana uwezo wa kichawi wa kumroga mtu kwa manuizo na tunguli na kumuua bila kutumia scientifically established methods, including the powerful psycholovical effect? Uchawi huu haupo, ni fikra za mabaki ya zama za ujinga tu.

Kama upo basi mchawi aniloge mimi hapa.
 
dawa ya mchawi ni Jina la Yesu.Marko 16:17-18,Yohana 14:14,Matendo 3:6.omba kwa hilo jina kwa imani,uone timbwili atakalolipata huyu mama.

Yesu na wachawi wote ni uongo mmoja tu.
 
nani kakuambia ila yakikuelewa utautafuta msaada wake.

Msaada gani?

Na kaama yeye ni mwingi wa upendo hivyo, kwa nini asubiri mpaaka niufuate msaada wake wakati anaweza kunisaidia kabla?
 
Hujajibu maswali.

Hilo, hata kama litakuwa kweli, halithibitishi kwamba uchawi upo na si stories tu.


Uchawi ni nguvu za giza zinazotumiwa na jamii nyingi, hasa za Kiafrika, kwa ajili ya mtu kuumiza watu wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujilinda au kwa ajili ya kujifurahisha kwa kuwatesa watu wengine kwa kuwachukua msukule au kuwafanya waugue au wafe. Mara nyingi, wachawi hudai kwamba wanaweza kuwasiliana na roho kama mashetani, majini, vigwengo, vinyamkera na kushirikiana navyo.

Kadiri ya dini mbalimbali watu wote wanaotumia nguvu hizo za giza wapo kinyume na Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia.
 
Hujajibu maswali.

Hilo, hata kama litakuwa kweli, halithibitishi kwamba uchawi upo na si stories tu.

DALILI KUWA UCHAWI UPO, KUTOKA KATIKA QURANI NA KATIKA SUNNAH (MAFUNDISHO YA MTUME (SAW))
Katika Surat Yunus aya ya 77 MwenyeziMungu anasema:
"Akasema Musa:"Mnasema (hivi) juu ya haki ilipokujieni, (kuwa) Huu ni uchawi? (Mbona umefaulu basi) Na wachawi hawafaulu".
Hii ni dalili kwamba uchawi upo na MwenyeziMungu anatufundisha katika aya hii kwamba uchawi haufaulu.
Na katika sutaul Falaq akasema:
"Na (najikinga na) shari ya wale wanaopuliza mafundoni".

Katika kuifasiri aya hii, mmoja katika maulamaa wakubwa wa tafsiri ya Qurani Imam Al Qurtuby amesema:
"Maana ya neno "Nafaathaat", ni wachawi wanapopuliza katika nyuzi huku wakizipiga fundo.
Na Ibni Kathiyr katika tafsiri yake akinukuu kutoka kwa Ikrimah na Mujahid na Al Hassan Al Basry (RA) amesema:
"Hawa wanaopuliza mafundoni ni wachawi, na MwenyeziMungu anatuamrisha tujiepushe na shari zao.

Amma hadithi za Mtume (SAW) zinazotufahamisha kwamba uchawi upo na kwamba uchawi ni katika madhambi makubwa sana, ni hizi zifuatazo:

Kutoka kwa Abi Huraira (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema:
"Jieupusheni na (mambo) saba Yaangamizayo'.
Wakasema:
'Ni yepi hayo ewe Mjumbe wa MwenyeziMungu?"
Akasema:
"Kumshirikisha MwenyeziMungu, Uchawi, kuiuwa nafsi iliyoharimishwa na MwenyeziMungu ila kwa haki yake, kula riba, kula mali ya yatima, kurudi nyuma (kukimbia) katika vita vya Jihadi (huku ukiwaacha wenzio wanapigana), na kuwasingizia uwongo wanawake wema wasio na makosa".
Bukhari na Muslim
Ndugu yangu Muislamu, Mtume (SAW) aliposema kuwa mambo hayo 'Yanayomuangamiza', maana yake ni kuwa yanamuangamiza mtu katika moto wa Jahannam.
Ukirudia kuisoma tena hadithi hiyo utaona kuwa Mtume (SAW) ameutanguliza uchawi kabla ya dhambi ya kuuwa, ingawaje kuuwa ni dhambi kubwa sana, na MwenyeziMungu anasema katika Suratu Nnisaa aya ya 93
"Atakayemuuwa Muislamu kusudi, basi jaza yake ni Jahannam atakuwa humo milele na MwenyeziMungu Ataghadhibika naye na Atamlaani na amemtayarishia adhabu kubwa".

Juu ya ukubwa wa dhambi hiyo ya kuuwa, lakini Mtume(SAW) ameipa uzito zaidi dhambi ya Uchawi kwa kuiweka nafasi ya pili baada ya Shirki na kabla ya dhambi ya kuuwa.
 
Back
Top Bottom