Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Nitafute 075 421 1726 nitajaribu kukusaidia.
Kuna ishu imenikumba juzi kati wakati nilipokuwa nafuatilia shamba la mzee wangu kwa ajili ya kulifanyia mchakato wa kulisafisha.
Kufika huko nimekutana na kitu tofauti na matarajio yangu.Yaani shamba limemegwa na mama mmoja na taarifa zikadai hajauziwa ila amekuja kuvamia.

Nilichokifanya nilimchukua anko wangu tukaanza kumtafuta huyo mama bahati nzuri tulikutana naye njiani siku moja.

Anko alipomuhoji kwanini amevamia eneo sio lake hakutujibu badala yake alimrushia anko jini akabaki anagalagala chini na yule mama akaondoka zake mpaka sasa anko kapooza na shamba limemegwa na nikiangalia msimu wa kilimo umekaribia.Je nifanyeje wadau ili niweze pata haki yangu.
N.B

Shamba lina hati zote ila uchawi tu ndio unanitisha.
 
Tatizo humu watu wanapinga vitu ambavyo hata hawavijui.

Usipovitaja na kuelezea hawavijui kwa vipi na wewe unaongezea tatizo.

Maana hata hawatajua kwamba wana tatizo na tatizo liko wapi.
 
Hujajibu maswali uliyouliza, uliyojibu hujaulizwa.

Ukishindwa hili tu, utajua dalili zote za magonjwa yote?

UCHAWI UMEANZA ZAMA ZA NABII SULEIMAN (AS) ?
Wachawi wanaposoma talasimu zao huwadanganya watu kwa kuanza kusoma baadhi ya aya au sura ndogo ndogo za Qurani na kulitajataja jina la Nabii Suleiman na utawasikia daima wanamnasibisha Mtume huyu (AS) na kufru zao hizo ili wajinga wanaowafuata wadhani kwamba hayo yamo katika dini.
Uchawi haujaanza zama za Nabii Sulaiman kama wachawi wanavyozuwa na kumsingizia Nabii Huyu wa MwenyeziMungu, bali ulikuwepo kabla yake kwa miaka elfu nyingi.
Uchawi ulikuwepo tokea zama za Nabii Saleh (AS) aliyekuja kabla ya Nabii Sulaiman kwa miaka elfu nyingi.
MwenyeziMungu anasema:
"Wakasema: (kumuambia Nabii Saleh); "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa".
Ash Shuaraa - 153

UCHAWI NI KUFRU
Wachawi na wafuasi wao hupenda kumsingizia Nabii Suleimani kwa kuinasibisha na kufru yao hiyo na Mtume huyu mtukufu ambaye MwenyeziMungu alimpa ufalme ambao hajaupata mwengine baada yake kwa sababu alimpa uwezo wa kuwatiisha majini, upepo, na alipewa uwezo wa kujua lugha za wanyama n.k.
MwenyezMungu anasema:
"Basi tukamtiishia upepo unaokwenda pole pole kwa amri yake, anakotaka kufika (unamfikisha).
Pia tukamtiishia mashetani, kila ajengaye na azamiaye (lulu).
Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake).
Sad - 36-38

Katika tasfiri yake, Ibni Kathiyr amenukuu kauli ya Ibni Abbas (RA) kuwa amesema:
"Asif - alikuwa mwandishi wa Nabii Sulaiman na alikuwa akilijuwa jina tukufu la MwenyeziMungu (Al ismul aadham), na alikuwa akiandika kila kitu katika daftari kwa amri ya Nabii Sulaiman na kulificha daftari hilo chini ya kiti cha Nabii Sulaimani. Alipofariki Nabii Suleiman, majini wakayatoa maandishi hayo wakachanganya na kuandika baina ya kila mistari miwili uchawi na kufru yao, kisha wakawaambia watu wao kuwa hayo ndiyo maandishi ya Nabii Sulaiman na ndiyo aliyokuwa akiyatenda, na Mayahudi wakayasadiki maneno hayo, wakawa wanamtangazia Nabii huyu kuwa ni mchawi.
Mpaka alipokuja Mtume (SAW) na kuteremshiwa aya ya 102 katika Suratul Baqarah:
MwenyeziMungu anasema:
"Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani (wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii) Sulaiman; na Sulaiman hakukufuru (Kwa sababu uchawi ni kufru) bali mashetani ndio waliokufuru wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani) na (uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili Haruta na Maruta katika (mji wa) Babil (Babylon). Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie "Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru. "Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo) Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya MwenyeziMungu.Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa.
Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi)".
 
Uchawi ni nguvu za giza zinazotumiwa na jamii nyingi, hasa za Kiafrika, kwa ajili ya mtu kuumiza watu wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujilinda au kwa ajili ya kujifurahisha kwa kuwatesa watu wengine kwa kuwachukua msukule au kuwafanya waugue au wafe. Mara nyingi, wachawi hudai kwamba wanaweza kuwasiliana na roho kama mashetani, majini, vigwengo, vinyamkera na kushirikiana navyo.

Kadiri ya dini mbalimbali watu wote wanaotumia nguvu hizo za giza wapo kinyume na Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia.

Unaweza kuthibitisha kwamba uchawi, mungu, shetani etc ni kweli vipo na si simulizi zisizo na ukweli tu?
 
Skiliza kijana kuwa makini na huyo mama Usije ukamfata by face to face hata kama ume beba biblia au qur an mkononi tumia akili mpeleke mahakamani simama nae mahakamani uchawi upo. Na wao pia wanaamini mungu na wanakubaliwa maombi yao na inakuwa kama mtihan jua huo ni mtihani pigana utashinda wafate wazee ktk familia yako watakushauri kiundani zaidi
 
UCHAWI UMEANZA ZAMA ZA NABII SULEIMAN (AS) ?
Wachawi wanaposoma talasimu zao huwadanganya watu kwa kuanza kusoma baadhi ya aya au sura ndogo ndogo za Qurani na kulitajataja jina la Nabii Suleiman na utawasikia daima wanamnasibisha Mtume huyu (AS) na kufru zao hizo ili wajinga wanaowafuata wadhani kwamba hayo yamo katika dini.
Uchawi haujaanza zama za Nabii Sulaiman kama wachawi wanavyozuwa na kumsingizia Nabii Huyu wa MwenyeziMungu, bali ulikuwepo kabla yake kwa miaka elfu nyingi.
Uchawi ulikuwepo tokea zama za Nabii Saleh (AS) aliyekuja kabla ya Nabii Sulaiman kwa miaka elfu nyingi.
MwenyeziMungu anasema:
"Wakasema: (kumuambia Nabii Saleh); "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa".
Ash Shuaraa - 153
Rudi juu

UCHAWI NI KUFRU
Wachawi na wafuasi wao hupenda kumsingizia Nabii Suleimani kwa kuinasibisha na kufru yao hiyo na Mtume huyu mtukufu ambaye MwenyeziMungu alimpa ufalme ambao hajaupata mwengine baada yake kwa sababu alimpa uwezo wa kuwatiisha majini, upepo, na alipewa uwezo wa kujua lugha za wanyama n.k.
MwenyezMungu anasema:
"Basi tukamtiishia upepo unaokwenda pole pole kwa amri yake, anakotaka kufika (unamfikisha).
Pia tukamtiishia mashetani, kila ajengaye na azamiaye (lulu).
Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake).
Sad - 36-38

Katika tasfiri yake, Ibni Kathiyr amenukuu kauli ya Ibni Abbas (RA) kuwa amesema:
"Asif - alikuwa mwandishi wa Nabii Sulaiman na alikuwa akilijuwa jina tukufu la MwenyeziMungu (Al ismul aadham), na alikuwa akiandika kila kitu katika daftari kwa amri ya Nabii Sulaiman na kulificha daftari hilo chini ya kiti cha Nabii Sulaimani. Alipofariki Nabii Suleiman, majini wakayatoa maandishi hayo wakachanganya na kuandika baina ya kila mistari miwili uchawi na kufru yao, kisha wakawaambia watu wao kuwa hayo ndiyo maandishi ya Nabii Sulaiman na ndiyo aliyokuwa akiyatenda, na Mayahudi wakayasadiki maneno hayo, wakawa wanamtangazia Nabii huyu kuwa ni mchawi.
Mpaka alipokuja Mtume (SAW) na kuteremshiwa aya ya 102 katika Suratul Baqarah:
MwenyeziMungu anasema:
"Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani (wakadai kuwa yalikuwa) katika ufalme wa (Nabii) Sulaiman; na Sulaiman hakukufuru (Kwa sababu uchawi ni kufru) bali mashetani ndio waliokufuru wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani) na (uchawi) ulioteremshwa kwa Malaika wawili Haruta na Maruta katika (mji wa) Babil (Babylon). Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie "Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru. "Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo) Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya MwenyeziMungu.Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa.
Na kwa yakini wanajua kwamba aliyekhiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi)".

Kitabu chako hicho unachokikariri, ukianza kukisoma tu, utaambiwa mungu ndiye mtoa rehema zote za kumjua yeye.

Kuna watu atawapa rehema watamjua kirahisi tu, na wengine hata wajitahidi vipi, hawapi neema hii, na hivyo hawatamjua.

Kisha wakishakufa, siku ya kiyama, mungu huyu huyu aliyegawa rehema ya kumjua yeye apendavyo yeye mwenyewe, atawahukumu watu hawa.

Wale aliowapa rehema ya kumjua watazawadiwa kwenda peponi, na wale ambao mungu aliwanyima rehema ya kumjua wataenda motoni.

Nakueleza habari hii kukuonyesha ujinga wa hicho kitabu.

Kwamba mungu mwenyewe anagawa rehema ya kumjua kwa matakwa yake.

Na walioandikiwa kumjua watamjua hata wajifanye wabishi vipi.

Huku walioandikiwa kutomjua hawatamjua hata wajitahidi kumjua vipi.

Sasa huyu mungu akiwahukumu wale aliowanyima rehema ya kumjua, kwa utashi wake mwenyewe, itakuwa sawa kuwahukumu hawa watu aliowanyima rehema yeye mwenyewe?

Ninakueleza jambo hili kukuonyesha kwamba chochote utakachoandika hapa kwa kutumia Quran kama authority hakiko above ujinga wa kizamani kama huu nilioutaja hapo juu.

Tafuta a more reasonable authority.
 
Unaweza kuthibitisha kwamba uchawi, mungu, shetani etc ni kweli vipi na si simulizi zisizo na ukweli tu?
Mkuu unataka uthibitisho wa aina gani
1). Kuona ?
2).kusikia?
3).au mifano hai
Kuwa uchawi upo vp na shetani yupo vp pamoja na nguvu ya mungu ina angaza vipo
Kabla ya kuthibitisha nikuulize wewe kwanza una roho ngapi??
 
A logically consistent construct.

Hujanijibu kuhusu ujinga wa Quran bado.
 
Kiranga naomba kujua mtazamo wako juu ya mtu kama Dynamo the Magician au Chriss Angel. Nadhani unahabari kuwa hawa watu wanatembea juu ya maji, wanapaa, wanapita kwenye mageti bila kufungua, wanaweza wakaamua kutobebeka kwa kujiongezea uzito usio wakawaida, telekinesis, telepathy na mengine mengi. Je unaamini kuna kanuni wanazofuata kufanya hivyo au wamezaliwa tu na uwezo huo? Kama kuna kanuni/masharti je yametoka wapi? Asili yake ni nini?
 
Last edited by a moderator:

Hata mtu kupita kwenye ukuta wa matofali si kinyume na kanuni za fizikia.

Na hivyo si uchawi.

Michezo mingine ni mazingaombwe tu, karata tatu. Mingine kuna tricks wanatumia. Ukipata vitabu na videos zinavyoonyesha watu wanavyofanya hizi "magic trick" utacheka.

Mambo mengine ni training ya hali ya juu, mengine ni planning ya hali ya juu.

Kuna mtu aliuvizia mti wakati uko mdogo na mteke, akapandikiza kiwembe kimoja humo ndani, kingine akabaki nacho. Baada ya miaka kadhaa akawa anafanya mazingaombwe pale kwenye mti. Mti ulishakuwa mkubwa kiasi. Akawambia watu mnakiona kiwembe hiki? Akafanya abracadabra zake pale, akawaambia kiwembe kitatokea ndani ya mti. Kuuvunja huo m branch wa mti kweli, kiwembe kimetokea. Watu wakamuona mchawi.

Huyu trick yake ilikuwa ndogo tu, planning years ahead.

Maengine ni mazoezi tu, kama yule Nick Wallenda anayetembea juu ya waya huku kafumba macho. Jamaa alianza kufanya mazoezi tangu mdogo. Binadamu tuna uwezo wa kufanya mambo mengi kama hayo kama tuna practice, tatizo wanao practice ni wachache.

Sasa mtu kama yule akija bongo huko na kuanza kutembea juu ya waya watu watasema mchawi.

Kumbe ni practice tu.

http://www.skyscraperlive.com/

Mtu anaweza kuwa kakulia timing, mmegombania shamba, mmezozana, anajua mtakutana sehemu fulani, mkikutana anakumwagia sumu fulani ya kunyunyuzia, unaanguka na kufa, watu hata kabla hawajafanya "post mortem" washarukia kusema uchawi wakati ni mambo ya chemistry tu.
 
Kitabu chako hicho unachokikariri, ukianza kukisoma tu, utaambiwa mungu ndiye mtoa rehema zote za kumjua yeye.

Kuna watu atawapa rehema watamjua kirahisi tu, na wengine hata wajitahidi vipi, hawapi neema hii, na hivyo hawatamjua.

Kisha wakishakufa, siku ya kiyama, mungu huyu huyu aliyegawa rehema ya kumjua yeye apendavyo yeye mwenyewe, atawahukumu watu hawa.

Wale aliowapa rehema ya kumjua watazawadiwa kwenda peponi, na wale ambao mungu aliwanyima rehema ya kumjua wataenda motoni.

Nakueleza habari hii kukuonyesha ujinga wa hicho kitabu.

Kwamba mungu mwenyewe anagawa rehema ya kumjua kwa matakwa yake.

Na walioandikiwa kumjua watamjua hata wajifanye wabishi vipi.

Huku walioandikiwa kutomjua hawatamjua hata wajitahidi kumjua vipi.

Sasa huyu mungu akiwahukumu wale aliowanyima rehema ya kumjua, kwa utashi wake mwenyewe, itakuwa sawa kuwahukumu hawa watu aliowanyima rehema yeye mwenyewe?

Ninakueleza jambo hili kukuonyesha kwamba chochote utakachoandika hapa kwa kutumia Quran kama authority hakiko above ujinga wa kizamani kama huu nilioutaja hapo juu.

Tafuta a more reasonable authority.
Mkuu umekariri vibaya tafsri ya kumjua mungu... katika quruan
Tafsri ya kumjua mungu imelenga ni iman ya kuamini uwepo wa mungu katika maisha so mungu katupa mtihani wa kuweka juhudi ya kumtambua katika roho zetu na ndipo atatupa zawadi ya pepo na mambo mengine mazuri hapo siku ya mwisho na kwa yule asiyekua na iman na akashindwa kujitahidi ku ubughudhi moyo na akili yake katika kumtambua yeye basi yupo katika hasara kubwa
Na ndio maana mungu akakuweka katika dunia na sio sayari nyingine ili upate changamoto ya kiroho
 
Hata mtu kupita kwenye ukuta wa matofali si kinyume na kanuni za fizikia.

Na hivyo si uchawi.

Michezo mingine ni mazingaombwe tu, karata tatu. Mingine kuna tricks wanatumia. Ukipata vitabu na videos zinavyoonyesha watu wanavyofanya hizi "magic trick" utacheka.

Mambo mengine ni training ya hali ya juu, mengine ni planning ya hali ya juu.

Kuna mtu aliuvizia mti wakati uko mdogo na mteke, akapandikiza kiwembe kimoja humo ndani, kingine akabaki nacho. Baada ya miaka kadhaa akawa anafanya mazingaombwe pale kwenye mti. Mti ulishakuwa mkubwa kiasi. Akawambia watu mnakiona kiwembe hiki? Akafanya abracadabra zake pale, akawaambia kiwembe kitatokea ndani ya mti. Kuuvunja huo m branch wa mti kweli, kiwembe kimetokea. Watu wakamuona mchawi.

Huyu trick yake ilikuwa ndogo tu, planning years ahead.

Maengine ni mazoezi tu, kama yule Nick Wallenda anayetembea juu ya waya huku kafumba macho. Jamaa alianza kufanya mazoezi tangu mdogo. Binadamu tuna uwezo wa kufanya mambo mengi kama hayo kama tuna practice, tatizo wanao practice ni wachache.

Sasa mtu kama yule akija bongo huko na kuanza kutembea juu ya waya watu watasema mchawi.

Kumbe ni practice tu.

http://www.skyscraperlive.com/

Mtu anaweza kuwa kakulia timing, mmegombania shamba, mmezozana, anajua mtakutana sehemu fulani, mkikutana anakumwagia sumu fulani ya kunyunyuzia, unaanguka na kufa, watu hata kabla hawajafanya "post mortem" washarukia kusema uchawi wakati ni mambo ya chemistry tu.

Kwa hiyo unaniambia kuwa mazingaombwe ya kutembea juu ya maji, kupaa, kupita kwenye ukuta, kumtowesha tembo ni just a trick ambayo ukinong'onezwa waweza fanya? Na yale mapepo/majini ambayo humpanda mtu akaanza kuzungumza mambo yaliyositirika ni ukanjanja tu?
 
Kuna vitu vingi sana, kuna peer pressure, kuna hypnotism, kuna fakery, kuna mengine inabidi tujifunze zaidi ili kuyaelewa.
But that does not mean the answer is supernatural.

Tatizo kitu tusipokielewa tunakimbilia majini/mapepo/shetani/mungu/uchawi.

Zamani mababu zetu walivyoona wazungu wanatembea na redio waliona uchawi.

Mzungu akitabiri eclipse waliona uchawi.

Sasa siku hizi tumeelewa haya mambo yanavyoenda tunaweza kuyaelezea bila kuhitaji theory ya uchawi na majini/ mapepo.

Ndio mule mule tu. Mnakuwa kama wale watu walioona redio wakaona wazungu wachawi.
 
Mkuu hiyo supernatural aliyonayo mtu akiitumia vibaya ndio huleta madhara kwa mtu/watu lazima ulewe na kutambua kuwa majini yapo na shetani yupo..katika ulimwengu
Mawazo ya zaman ya babu kumuona mzungu na radio na kusema ni wachawi that period palikuwa na transition ya mawazo tu kwasababu mzungu alikua na nia yake hapa africa kifupi kulikua na utapeli fulani hivi
 
Yesu ndio kiboko ya wachawi wote mtafute yeye kwa bidii uyo mama hatorudisha shamba tu bali na yeye atakufa sababu biblia inasema usimuache mwanamke mchawi aishi kwaiyo kijana usijariibu kwenda kwa waganga sababu waganga na wachawi ni.sawa na uvccm.na ccm ni.kampuni moja matawi tofaut so omba watu wa maombi wakufanyie maombi au tafuta jina la uyo mama nitumie hpa nimtumie moto wa Yesu mtaenda kwenye mazishi yake soon.
 
Kuna vitu vingi sana, kuna peer pressure, kuna hypnotism, kuna fakery, kuna mengine inabidi tujifunze zaidi ili kuyaelewa.
But that does not mean the answer is supernatural.

Tatizo kitu tusipokielewa tunakimbilia majini/mapepo/shetani/mungu/uchawi.

Zamani mababu zetu walivyoona wazungu wanatembea na redio waliona uchawi.

Mzungu akitabiri eclipse waliona uchawi.

Sasa siku hizi tumeelewa haya mambo yanavyoenda tunaweza kuyaelezea bila kuhitaji theory ya uchawi na majini/ mapepo.

Ndio mule mule tu. Mnakuwa kama wale watu walioona redio wakaona wazungu wachawi.

Nakubali kuwa kuna vitu vingi mfano infrared, electromagnetic waves, n.k. ni mambo ambayo mpaka leo kuna watu yanawatatiza lakini ni electronics ya kawaida tu.

Wazungu (Matajiri na Marais wa Marekani) mbona wanatambika kwenye misitu ya Bohemian Grove!.
Na hata wanapojenga majengo yao kuna geometry ambazo wanazifuata kimasonic zaidi, vivohivyo kwa wayahudi na kabalah yao.
Pia waarabu(hawa husoma dua), wachina, wahindi, waafrika, na wajapan hawajengi majengo makubwa bila kutambika na si kwasababu wamerithi huo utamaduni bali wameisha pata kasheshe ya madaraja/majengo kuvunjika bila sababu wakati fizikia yote ilizingatiwa, wageni kufa hovyo kwenye mahoteli, mabomba mapya kutoa maji ya kutu n.k. Bila kusahau watu waliogandiana na kushindwa kutoka baada ya kufumaniwa wakila uroda bongo (walipelekwa hospitali ya temeke, FFU wakavamia na kutawanya halaiki ya watu) na Kenya pia ambao ni uchawi unaoitwa tego. Ndiyo maana nasema mpaka utakaposhuhudia ndipo utaweza kuangalia kutoka pembe nyingine.
 
Usipovitaja na kuelezea hawavijui kwa vipi na wewe unaongezea tatizo.

Maana hata hawatajua kwamba wana tatizo na tatizo liko wapi.

We unasema uchawi hakuna, lakini nikikuuliza je huo uchawi unaujua ni nini si ajabu hata ukawa haujui ni nini huo uchawi.
 
Mkuu hiyo supernatural aliyonayo mtu akiitumia vibaya ndio huleta madhara kwa mtu/watu lazima ulewe na kutambua kuwa majini yapo na shetani yupo..katika ulimwengu
Mawazo ya zaman ya babu kumuona mzungu na radio na kusema ni wachawi that period palikuwa na transition ya mawazo tu kwasababu mzungu alikua na nia yake hapa africa kifupi kulikua na utapeli fulani hivi

Mtu ana supernatural gani?

Wapi umepata habari hii?

Comprehension please!
 
Nakubali kuwa kuna vitu vingi mfano infrared, electromagnetic waves, n.k. ni mambo ambayo mpaka leo kuna watu yanawatatiza lakini ni electronics ya kawaida tu.

Wazungu (Matajiri na Marais wa Marekani) mbona wanatambika kwenye misitu ya Bohemian Grove!.
Na hata wanapojenga majengo yao kuna geometry ambazo wanazifuata kimasonic zaidi, vivohivyo kwa wayahudi na kabalah yao.
Pia waarabu(hawa husoma dua), wachina, wahindi, waafrika, na wajapan hawajengi majengo makubwa bila kutambika na si kwasababu wamerithi huo utamaduni bali wameisha pata kasheshe ya madaraja/majengo kuvunjika bila sababu wakati fizikia yote ilizingatiwa, wageni kufa hovyo kwenye mahoteli, mabomba mapya kutoa maji ya kutu n.k. Bila kusahau watu waliogandiana na kushindwa kutoka baada ya kufumaniwa wakila uroda bongo (walipelekwa hospitali ya temeke, FFU wakavamia na kutawanya halaiki ya watu) na Kenya pia ambao ni uchawi unaoitwa tego. Ndiyo maana nasema mpaka utakaposhuhudia ndipo utaweza kuangalia kutoka pembe nyingine.

Wazungu ndiyo stsndsrd ysko ys ukweli?

Mzungu akitambika basi uchawi upo?

Kuna wakati karibu dunia nzima iliamini jua linazunguka dunis, did that make it so?

Estu wakigandiana kwa nini unakimbilia kusema uchawi?

Unafahamu rare biological phenomena zote?
 
Back
Top Bottom