Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Dalili gani?

Utajuaje dalili ambazo hujaziona?

Wewe ni mtaalamu wa forensic science?
Mfano mgonjwa anatamka na hisi sehemu ya mwili inauma tangu jana lazima utaelewa kuwa hizo ni dalili za ku umwa
 
Mkuu,

Dawa ya uchawi ni Yesu Kristo pekee.

Ngoja nami 'nishee' nawe stori kama yako iliyonipata mwaka 2013. Ilikuwa hivi;
1. Baba yangu alinunua shamba kijiji cha mbali kidogo na kijijini kwetu. Aliyemshawishi kununua shamba hilo ni rafiki yake. Jina lake anaitwa mzee Chai (siyo jina lake halisi).
2. Katika mauziano ya shamba, baba hakumshirikisha mzee Chai ila alimtaarifu baadaye juu ya manunuzi hayo. Haya yalitokea kama miaka 15 hivi iliyopita.
3. Baadaye mzee Chai akaomba kulilima shamba hili sababu lilikuwa karibu na nyumbani kwake. Baba alimruhusu kwa masharti kwamba atakuwa anarejesha kiasi fulani cha magunia ya mahindi kama malipo kwa kutumia shamba. Walikubaliana na maisha yakasonga.
4. Mwaka 2010, baba alifariki dunia. Mwaka mmoja baadaye mzee Chai akasitisha kupeleka nyumbani marejesho ya mavuno yake kama walivyokuwa wamekubaliana na marehemu baba. Nilipomuuliza sababu akanijibu haoni sababu ya kuendelea kuleta marejesho kwa kuwa amekuwa anavuna kiasi kidogo sana.
5. Kama familia, tukamtaka arudishe shamba letu ili tumpatie (kumkodisha) mtu mwingine. Aliposikia hivi akaja juu na akanitishia 'kunitengeneza'. Pia akadai kuwa shamba hilo ni lake sababu walikubaliana hivyo na marehemu baba. Kifupi ni kuwa alitaka kutudhulumu kwa sababu alijiamini na 'silaha' zake. Nilichomjibu ni kuwa kwanza, shamba ni letu kwa sababu tuna uthibitisho wa umiliki wake (tunazo hati za mauziano). Pili, hataweza 'kunitengeneza' sababu aliye ndani yangu ni mkuu zaidi ya vyote pamoja na 'silaha' zake.
6. Nilichoamua kufanya baadaye ni kumtafuta mzee mmoja hukohuko kijijini na nikamueleza 'stori' yote na pia nikamuomba aende kwa mwenyekiti wa kijiji lilipo shamba ili wamwite mzee Chai na kuongea naye.
7. Mzee Chai alipoitwa aling'ang'ania kuwa shamba ni lake na mke wake akathibitisha hilo mbele ya viongozi wa kijiji. Kikao hicho kikaamua kuwa kwa kuwa kila mmoja anadai shamba ni lake, basi kila mmoja alete ushahidi wa madai yake.
8. Nilituma 'copy' ya mauziano siku chache baadaye. Ilikuwa kama saa saba hivi ya siku hiyo. Usiku wa siku hiyohiyo kama saa nne hivi usiku nilipata ajali mbaya sana pale Tazara mataa kama unaenda uwanja wa ndege, Dsm. Nilikuwa naendesha gari, Toyota Carina, kutoka uelekeo wa uwanja wa ndege kuelekea Temeke. Niligonga ukuta wa barabara karibu na mataa ya Tazara, gari ilipaa ikatua katikati ya barabara ( ikaziba barabara ya kutoka uwanja wa ndege). Nilipotua tu nikaona lori linakuja kwa kasi toka uwanja wa ndege na lilikuwa linakuja kugonga ubavuni mwa Carina. Mungu mkubwa lori likanikosa na kupita pembeni upande wa Azam. Injini ya gari ilipasuka pamoja na 'gear box'. Matairi yote yakapasuka. Mimi nilitoka nikiwa mzima sijachubuka kata kidogo.
9. Kesho yake mchana wakati nashughulika kutoa gari polisi, mzee Chai alinipigia simu. Sikuweza kupokea simu yake sababu nilikuwa 'bize'. Jioni yake nikampigia na katika maongezi yetu nikamwambia shamba ni mali yetu hatoweza kamwe kulidhulumu.
10. Mwisho alikuja omba radhi kwa uongozi wa kijiji na familia kwa kudanganya na kujaribu kudhulumu shamba letu. Kwa sasa, bado analilima shamba lakini kwa makubaliano mapya na familia yetu. Tuliamua kumpa yeye mwenyewe, mzee Chai.

Ndugu, hakuna jambo linaloshindikana kwa Yesu.


Tafakari.

Kuna ishu imenikumba juzi kati wakati nilipokuwa nafuatilia shamba la mzee wangu kwa ajili ya kulifanyia mchakato wa kulisafisha.
Kufika huko nimekutana na kitu tofauti na matarajio yangu.Yaani shamba limemegwa na mama mmoja na taarifa zikadai hajauziwa ila amekuja kuvamia.

Nilichokifanya nilimchukua anko wangu tukaanza kumtafuta huyo mama bahati nzuri tulikutana naye njiani siku moja.

Anko alipomuhoji kwanini amevamia eneo sio lake hakutujibu badala yake alimrushia anko jini akabaki anagalagala chini na yule mama akaondoka zake mpaka sasa anko kapooza na shamba limemegwa na nikiangalia msimu wa kilimo umekaribia.Je nifanyeje wadau ili niweze pata haki yangu.
N.B

Shamba lina hati zote ila uchawi tu ndio unanitisha.
 
MWENYEZI MUNGU ndio muweza wa tatizo lako,mkimbilie kwa amani kila kitu kitakuwa sawa na utapata haki yako bila gharama..
 
Viumbe visivyo onekana umejuaje kwamba vipo na si stories tu?

Nimekuuliza unaweza kuthibitisha nguvu za giza zipo? Unaniambia ziko yangu enzi hizo kabla.mimi.sijawa mtoto, hilo si swali nililouliza.

Umejibu swali ambalo hujaulizwa, uliloulizwa hujajibu.

Firauni kuwa mtawala wa Masr is a matter of record.




Ninajua kwakua mimi sio wa kwanza kuwa hapa tangu enzi za kuanzishwa ulimwengu kulikua na viumbe wema na wasio wema... vitabu vingi vya kiroho vimeyazungumza haya pia najua unanielewa
Nguvu za giza zipo na uthibitisho wake upo kwa mtu unaye mjua naye ni firauni
Records zipi zilikujulisha unayemsoma ndie firauni??????
 
mpe matibabu kwanza anko wako mengine yatafuata na kwenda vizuri..
 
ukimuona njiani mwagie petrol na umchome moto, uko shinyanga nini
 
Ninajua kwakua mimi sio wa kwanza kuwa hapa tangu enzi za kuanzishwa ulimwengu kulikua na viumbe wema na wasio wema... vitabu vingi vya kiroho vimeyazungumza haya pia najua unanielewa
Nguvu za giza zipo na uthibitisho wake upo kwa mtu unaye mjua naye ni firauni
Records zipi zilikujulisha unayemsoma ndie firauni??????

Unajuaje kwamba vitabu vya kiroho havikujazi ujinga?

Habari za firauni zimeandikwa kwenye peer reviewed journals za Egyptologists.

Hujathibitisha kwamba nguvu za giza zipo.
 
Unajuaje kwamba vitabu vya kiroho havikujazi ujinga?

Habari za firauni zimeandikwa kwenye peer reviewed journals za Egyptologists.

Hujathibitisha kwamba nguvu za giza zipo.

Ujinga unatoka wapi katika mambo ya kiroho???
Hebu soma chanzo cha nguvu za giza :::::

BIBLIA inasema hivi kumhusu Muumba wetu: “Mungu ni nuru na hakuna giza kamwe katika muungano na yeye.” (1 Yohana 1:5) Hilo ni kweli hasa kuhusu mambo ya kiroho. Kwa hiyo, je, Mungu wa kweli anaweza kuwa ndiye chanzo cha uchawi? Au je, kuna nguvu fulani ya uovu inayoongoza uchawi?
Baadhi ya mazoea ya kiuchawi ambayo watu hujihusisha sana nayo ni uaguzi na kuwasiliana na pepo kutia ndani unajimu, ubashiri wa kutumia namba, usomaji wa viganja, kuwasiliana na “wafu” na vilevile ulozi. Mazoea hayo yana historia ndefu, kwani mengi kati yake yalianzia Babiloni la kale, ambalo magofu yake yanapatikana huko Iraki. (Isaya 47:1, 12, 13) Kutoka Babiloni, mazoea ya uchawi yalienea kote katika ulimwengu wa kale na kutia mizizi katika tamaduni na jamii nyingi.
Fikiria tukio lililotokea katika jiji la Filipi lililokuwa katika Makedonia ya kale. Kikundi kidogo cha wahudumu Wakristo, kilichotia ndani mtume Paulo na daktari Luka, kilikutana na msichana aliyekuwa na nguvu za kufanya uchawi. Ona jinsi Luka, mwandikaji wa Biblia, alivyofunua chanzo cha nguvu hizo. Aliandika hivi: “Kijakazi fulani mwenye roho, roho mwovu wa uaguzi, akakutana nasi. Yeye alikuwa akiwapatia mabwana zake faida nyingi kwa kufanya ufundi wa kubashiri.”—Matendo 16:16-18.
Naam, msichana huyo hakupata nguvu hizo kutoka kwa Mungu wa kweli, Yehova, bali kutoka kwa roho mwovu. Hiyo ndiyo sababu Paulo pamoja na waandamani wake walikataa kumsikiliza. Huenda unajiuliza hivi: ‘Roho waovu ni nani? Nao walitoka wapi?’ Hebu ona majibu ya Biblia.
Roho Waovu Ni Nani?
Mapema kabla ya kuwaumba wanadamu, Yehova aliumba ‘wana wa Mungu’ wa roho huko mbinguni, wenye akili na walio wengi sana. (Ayubu 38:4, 7) Kama wanadamu, wao pia wana uhuru wa kuchagua, na kwa muda mrefu walikuwa washikamanifu kwa Mungu. Lakini kwa ghafula hali hiyo ya furaha ilikatizwa. Jinsi gani?
Baada ya Mungu kuwaumba wanadamu, kiumbe mmoja wa roho alianza kutamani kitu ambacho hakikuwa chake —ibada. Kama vile mtu mwenye ustadi anavyoweza kufanya ionekane kana kwamba sauti inatoka katika mwanasesere, malaika huyo mwovu alitumia nyoka kumshawishi mwanamke wa kwanza, Hawa, asimtii Muumba wake. (Mwanzo 3:1-6) Biblia inamtaja malaika huyo mwasi kuwa “yule nyoka wa zamani, yeye anayeitwa Ibilisi na Shetani.” (Ufunuo 12:9) Yesu alimtaja kuwa “muuaji” ambaye “hakusimama imara katika kweli,” halafu akaongeza hivi: “Anaposema uwongo, yeye husema kulingana na mwelekeo wake mwenyewe, kwa sababu yeye ni mwongo na ndiye baba ya uwongo.”—Yohana 8:44.
Baadaye, ‘wana wengine wa roho wa Mungu wa kweli’ walijiunga katika uasi huo wa Shetani. (Mwanzo 6:1, 2) Wanajulikana kama “wale malaika waliofanya dhambi” na wale “malaika ambao hawakubaki mahali pao pa kwanza bali wakayaacha makao yao wenyewe yanayofaa,” au mahali pao walipogawiwa huko mbinguni. (2 Petro 2:4; Yuda 6) Wakaja kujulikana kama roho waovu. (Yakobo 2:19) Zaidi ya hilo, wameazimia kuwaondoa watu wengi iwezekanavyo kutoka kwenye ibada ya kweli, kama vile tu walivyowafanya Waisraeli katika nyakati za Biblia. (Kumbukumbu la Torati 32:16, 17) Vivyo hivyo leo pia, kama vile ilivyokuwa nyakati zilizopita, Shetani pamoja na roho waovu hutumia ujanja kufundisha uwongo wa kidini.—2 Wakorintho 11:14, 15.
Jilinde!
Hata ingawa roho waovu wana nguvu zinazopita zile za wanadamu, kupitia msaada wa Mungu, tunaweza ‘kuchukua msimamo kuwapinga’ na kuwa washindi. (1 Petro 5:9) Hata hivyo, ili kupata msaada huo, tunahitaji kujifunza yale ambayo Mungu anataka tufanye na kutenda kupatana nayo. Akizungumza kuhusu Wakristo walioishi wakati wake, mtume Paulo aliandika hivi: “Sisi . . . hatujaacha kusali kwa ajili yenu na kuomba kwamba mjazwe ujuzi sahihi wa mapenzi yake katika hekima yote na utambuzi wa kiroho, ili mtembee kwa kumstahili Yehova kwa kusudi la kumpendeza yeye kikamili.”—Wakolosai 1:9, 10.
Wale ambao walipata ‘ujuzi huo sahihi’ walitia ndani watu kadhaa kutoka jiji la Efeso ambao walifanya uchawi. Ona jinsi ujuzi kuhusu kweli ulivyowasaidia. Biblia inasema hivi: “Hesabu kubwa ya wale wa
 
Kabla ya mgonjwa kumuona dokta lazima akutambulishe dalili kuwa anaumwa nn..then utamshauri kuwah hospital

Hujajibu maswali uliyouliza, uliyojibu hujaulizwa.

Ukishindwa hili tu, utajua dalili zote za magonjwa yote?
 
Wewe ni daktari? Unajua magonjwa mangapi?

Mimi sio dokta ila na utimamu wa kelewa kuwa mtu yupo normal au anaumwa...
Hospitali kuna vifaa tiba vya kutambua ugonjwa kwa undani zaidi...
 
Hujajibu maswali uliyouliza, uliyojibu hujaulizwa.

Ukishindwa hili tu, utajua dalili zote za magonjwa yote?
Nikuulize mkuu wewe kwa mfano nduguyo anakohoa mara kwa mara na yupo nyumbani
Je kwa utimamu wako utaelewa nn hapo??
 
Mimi sio dokta ila na utimamu wa kelewa kuwa mtu yupo normal au anaumwa...
Hospitali kuna vifaa tiba vya kutambua ugonjwa kwa undani zaidi...

A false sense of competence is characteristic of ignorance.

While the real doctors would be second guessing every hue of every hair in search of exellence.
 
A false sense of competence is characteristic of ignorance.

While the real doctors would be second guessing every hue of every hair in search of exellence.
Sio kweli mkuu before somebody to be patient there must be pre features to show up how deep disease is

Na ndio maana unampeleka hospitali baada ya kuhisi dalili
 
Sio kweli mkuu before somebody to be patient there must be pre features to show up how deep disease is

Na ndio maana unampeleka hospitali baada ya kuhisi dalili

Wewe unafahamu dalili zote za magonjwa yote?

Na una uwezo wa kumuina mtu mpaka ndani ya mwili wake hata pale dalili zisipoonekana kwa nje?
 
Mi sijaona sababu ya maana ya kuja kuomba msaada humu hali ya kuwa ushajiridhisha kwa kuamini kuwa kinachomsumbua Anko wako ni uchawi,na wewe ni muumini wa ukristo hivyo ungeenda kutafuta msaada wa hayo matatizo uliyonayo sehemu husika katika dini yako,kuliko kuleta tatizo lako humu kwenye watu wenye imani tofauti na mitazamo tofauti..matokeo yake ndiyo kama unavyoona wengine wanakushauri umuuwe huyo mama,wengine wanakwambia uende kwa mganga,wengine ndiyo wanakwambia hakuna uchawi kabisa.
 
Hivi kama kweli uchawi ni uzushi tu mi najiuliza maswali:

1.Je, ni wapi palipoanzia uzushi huu hadi ukasambaa dunia nzima?
2.Je,ni njia gani ilitumika kusambaza uzushi huo hadi ikafanikiwa dunia nzima?
3.Kama zama hizo watu waliamini uchawi kwa sababu ya ujinga je,vp sasa hivi bado watu wanaendelea kuamini huo uchawi?
 
Kuna ishu imenikumba juzi kati wakati nilipokuwa nafuatilia shamba la mzee wangu kwa ajili ya kulifanyia mchakato wa kulisafisha.
Kufika huko nimekutana na kitu tofauti na matarajio yangu.Yaani shamba limemegwa na mama mmoja na taarifa zikadai hajauziwa ila amekuja kuvamia.

Nilichokifanya nilimchukua anko wangu tukaanza kumtafuta huyo mama bahati nzuri tulikutana naye njiani siku moja.

Anko alipomuhoji kwanini amevamia eneo sio lake hakutujibu badala yake alimrushia anko jini akabaki anagalagala chini na yule mama akaondoka zake mpaka sasa anko kapooza na shamba limemegwa na nikiangalia msimu wa kilimo umekaribia.Je nifanyeje wadau ili niweze pata haki yangu.
N.B

Shamba lina hati zote ila uchawi tu ndio unanitisha.

Pande zipi unapatikana ? nikuelekeze kanisani umlete huyo anko wako tuzivunje kazi za ibilisi huyo
 
Back
Top Bottom