Msaada: Ninataka kufuga nyoka, wapi nitaweza kununua au kupata nyoka

Nahitaji mimi pia kufuga chatu na kenge, kwa mapambo tu!
Hahaha... Kufuga kenge na chatu kwa ajili ya mapambo! Kweli una hatari na unachokitafuta utakipata 2 hakuna mamna
Habari zenu waungwana

Nina shida, natafuta nyoka aidha green snake au black snake.
ninapoishi saizi kuna tatizo la panya na Mende wanasumbua sana.


hivyo nimeona njia sahihi ni kufuga nyoka ili niweze kuwatokomeza viumbe hivi .
Uwepo wa nyoka utanisaidia kupungua kwa panya na Mende,sababu hawa wadudu watakuwa kitoweo cha nyoka.

msaada kama kuna mtu anaweza kunipatia nyoka nitamlipa kiasi chochote tutakachokubaliana na kama watapatikana nyoka wawii itakuwa vizuri zaidi.Au kama nikipewa maelekezo wapi nitawapata nyoka hao itakuwa msaada kwangu mimi.

shukran.

Unataka kuruka jivu ukanyage moto? Unataka kumuua mende kwa risasi?

Wazo zuri sana hilo,ngoja nikutafutie jamaa yangu mmoja yupo Mwanza yeye hao huwa anawachezea muda wote.
 
Hivi unauwezo wa kukaa sebleni na huyo nyoka asiye na madhala mpaka umchokoze
Hakuna tatizo kama haumchokozi wala kumbughudhi mbona haushangai dubai watu wanakaa na chui sebuleni

Kama ukiishi wena na mnyama huyo asilani hamtogombana,chukulia mfano nyoka akimuona mtoto mbona hsmdhuru na pengine hucheza kabisa

Nyoka hana uadui na mtu ,uadui hujengeka pale mkigeukana
 
Sh ngap kiongozi

Na ni wa aina gani
Yule nyoka alikuwa wa ukoo na alikuwa analinda shamba baada ya babu kufa aliniachia na kunipa maelezo juu yake,ila ana mambo yake si ya kitoto.

Yupo sehemu moja inaitwa Bumera huko tarime vijijini.

Bei ni milion 3
 
Hakuna jiwe linatibu sumu za nyoka usidanganye watu
Mkuu nina ushahidi wa kutosha kua hilo jiwe lipo na linatibu kwa kufyonza sumu ya nyoka na ukitaka kujua kuhusu hilo jiwe ulizia naamini utaongeza maarifa Dunia ina mengi maajabu
 
python-snake-418169.jpg

kazi kwako ila inabidi ufuate utaratibu wa maliasili na pia ukiwa unaishi na familia yako bila wageni itakusaidia sana maana atawakalili wote harufu zenu nje ya hapo kuna siku utakuta shangazi aliyekuja kukusalimia kutoka uyole bila taarifa yuko tumboni mwa chatu.
Hahahaaaaaaaaa!
 
Mkuu nina ushahidi wa kutosha kua hilo jiwe lipo na linatibu kwa kufyonza sumu ya nyoka na ukitaka kujua kuhusu hilo jiwe ulizia naamini utaongeza maarifa Dunia ina mengi maajabu
Ata mimi nilishasikia, lakini kuna wakati Salim Kikeke (BBC) aliwahoji wataalamu wa nyoka wakakanusha.
Note; walidai hao wazushi hawajakutana na nyoka mwenye poison
 
Wazushi wapi wakati mimi nilisha ona laiv linatibu,usikatae mkuu hao walio kataa ni watu kila kitu huwezi kukijuwa kwenye dunia hii
 
Yule nyoka alikuwa wa ukoo na alikuwa analinda shamba baada ya babu kufa aliniachia na kunipa maelezo juu yake,ila ana mambo yake si ya kitoto.

Yupo sehemu moja inaitwa Bumera huko tarime vijijini.

Bei ni milion 3
du, ataweza kumfuga kweli huyo.. Akifanya masihara anaweza jikuta anafugwa yeye. Nyoka wa kuachiwa na babu si mchezo mchezo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom