Una tatizo la panya nyumbani kwako ,suluhisho ni NYOKA tu ndani ya wiki panya wote watakimbia

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
439
1,000
Je una tatizo la panya wasumbufu kwako ?

Ni dhahil ya kwamba panya wamekuwa wasumbufu sana majumbani ,panya hupenda kuvamia nyumba yenye vitu vingi na uchafu lakini pia hata nyumba safi ni destiny ya panya.Watu wengi wanatumia mbinu mbalimbali ili kuwadhibiti panya moja ya njia ni kufuga paka lakini kwa paka hawa wa siku hizi paka wa kimjini au paka wa sayansi na teknolojia wamekuwa less effective yaani hawana sumu ni mabishoo unakuta nyumba ina paka lakini panya wanazidi kuzaliana.

Paka anatizama TV na yupo makini sasa unategemea paka huyu ndio awadhibiti panya ? Kitu ambacho hakiwezekani.

Paka wa mjini usitegemee kabisa eti panya wataisha kwako


* kuna mnyama ambaye anachukiwa na watu lakini ni hodari sana na hana ubisho si mwingine Bali ni nyoka.Tuelimishane kuna nyoka wa aina 2

1) venomous snake -nyoka mwenye sumu

2)Non venomous- nyoka wasiokuwa na sumu

Nyoka chakula chao pendwa ni wadudu kama panya ,chura ,mende nk na hawa wadudu wote wanachukiwa na watu.

Nyoka ni suluhisho ya panya nyumbani kwako.Unaweza kujiuliza ni nyoka yupi anafaa umweke ili awakimbize panya nyumbani kwako usipatwe na shida

1)rat snake huyu nyoka ni maarufu sana nchini Australia sababu wapo wengi na huku Tanzania wapo hawa nyoka hawana sumu na wanapenda mno kula panya na hata panya akimbilie chini ya kochi nyoka huyu atamfuata huko huko na kummaliza .Rat snake ni huyo kwenye picha ,ameitwa rat snake sababu panya kwake ni kama vile wali kwa watu wa pwani.Na anapenda kuingia majumba ya watu haswa vijijini kusaka rodents kama panya ,ndege nk

2)python mdogo ,kuna chatu wadogo hawa hawana madhara kwa mtu sababu hawang'ati na hawana sumu sababu hawana fangs ,nyoka huyu anawapenda sana panyachatu mdogo ,.hana madhara kabisa kwa mtu aidha kwa kutisha au kung'ata na ni msaada mkubwa kwa kutokomeza panya

Nb:Hii ni njia rahisi kutokomeza panya fanya experiment kama nyumba yako ina panya wengi chukua nyoka wa aina hii muweke wiki tu hakika panya wote watakimbilia nyumba ya jirani na baada ya hapo mrudishe nyoka kwake .wiki tu na wala sio siku nyingi .Nyoka hawa 2 hawana madhara yeyote ile kwa mtu na ndio maana tunawaona baadhi ya watu wakitembea na small python na kuwachezea

moja ya nyumba wanayofuga nyoka,picha inaonyesha nyoka akimkamata panya aliyenona kwa kufanya uharibifu ,nyoka akatimiza wajibu wake na nyoka hawa hawacheki na kima pindi wakimuona panya tofauti na paka ,nyumba hiyo ndani ya wiki panya wote watahama makazi kunusuru maisha yao
 

MO11

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
17,345
2,000
kweli mtoa mada ulifikiria hali ya maisha ya huku kwetu au kiimani dhidi ya nyoka kisha ukatoa ushauri tufuge ?????
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
638
500
mbona hizo picha ni za wazungu bhana tuonyeshe picha za mbongo anayefuga nyoka nyumbani kwake ili kudhibiti panya,, una masihara na nyoka ww bora niishi na panya mia kuliko huyo Python mmoja unaesema hana sumu nani kakuambia kamuweke nyumbani kwko
 

gbefa

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
3,496
2,000
Mungu alitupa huwezo wa kuua na kukanyaga nyoka leo unasema!?
Paka wanafanya nini mkuu au wanadokoa mboga jikoni na maziwa kama makanikia
 

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
429
1,000
Labda uje ukae nae Huey nyoka wewe mwenyewe kwangu mm nihame na familia wiki ikifika uondoke na nyoka wako mm nirud
 

Nfumu

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
612
1,000
hata kama ni panya bora waendelee kujazana tu kuliko kufuga kisichofugika
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom