Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,596
Bwana Buddha alikuwa Uhindini huko zamani sana. Sasa uhindini kulikuwa na dinimaelfu kwa maelfu,kila mtu anahubiri dini yake.Tunajifunza mengi kutoka kwao.
Mimi pia nachokumbana nacho sijui nimwamini nani, nisiowaamini hao wapo verified tatizo kujua mtu wa maana wa kwenda nae sasa ni shida. Nimezungukwa sana na watu wanafiki... wanaong'ata na kupuliza kama sijakosea.
Leo yupo nawe kesho anaongea mengine...
Watu wakamuuliza, Bwana Buddha, wewe una umakini wa hali ya juu, tusaidie.Tumechanganyikiwa.Kila mtu anahubiri dini yake, dini zina mahubiri tofauti. Hatujui cha kuamini kipi na cha kuacha kipi.
Akawaambia,usiamini kitu kwa sababu kimesemwa na kuhani mashuhuri, wala kwa sababu kinakubaliwa na wengi, wala kwa sababu kimeandikwa katika misahafu mashuhuri,walakwa sababu umeambiwa na unaowaheshimu walimu na wazee. Usiamini kwa sababu kitu ni utamaduni wa muda mrefu.Usiamini hata ninachokuambia mimi. Kipime mwenyewe kwa mawazo yako, kwa weledi. Kwa akili na uchunguzi."