Msaada nataka kumfungulia mtoto account ya USD kwa ajili ya kumtunzia hela

elijaah

JF-Expert Member
Jul 13, 2023
468
836
Mambo vp wadau kama kuna mtu yoyote anaweza kunisaidia kujua faida na hasara kwa kufungua acc ya usd kwa kuhifadh hela naomba anifafanulie nipate uwelewa vizuri.
 
Ni nzuri tu, ila service charge za dollar huwa IPO juu. Unaonaje ukienda kuuliza bank?
 
Kamfungulie UTT ... hiyo hela itakua kwa rate nzuri kuliko kwenye bank akaunti. Au kaweke kwenye bonds au nunua shares.
 
Mambo vp wadau kama kuna mtu yoyote anaweza kunisaidia kujua faida na hasara kwa kufungua acc ya usd kwa kuhifadh hela naomba anifafanulie nipate uwelewa vizuri.
Kuwa mzalendo, mfungulie account ya shilingi.
 
Mambo vp wadau kama kuna mtu yoyote anaweza kunisaidia kujua faida na hasara kwa kufungua acc ya usd kwa kuhifadh hela naomba anifafanulie nipate uwelewa vizuri.
Faida:
1. Utaweza kutunza thamani ya pesa yako, kwa sababu kushuka kwa thamani ya pesa ya kigeni sio sawa na pesa ya Kitanzania.

2. Kuna faida kwenye baadhi ya akaunti za watoto. Faida siyo kubwa sana ni kama 0.5% kwa pesa ya kigeni kwa mwaka.

Hasara
1. Mara nyingi kwenye kutoa pesa cash hawakupi dollar ila wanakupa equivalent ya dollar kwa bei yao ya kununua yaani ni kama unawauzia pesa ya kigeni ili wakupe pesa ya Kitanzania. Bei zao za kununua hua siyo rafiki na ni ngumu kubadili kwenye maduka yenye rate nzuri au black market.

2. Huwezi kuweka pesa kwa wakala ni mpaka uende kwenye tawi ili wabadilishe pesa ndio uweke kwenye akaunti. Hii ni tofauti na akaunti za watoto za pesa ya Kitanzania ambazo unaweza kuweka pesa benki au kwa wakala.
 
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom