Msaada-Nairobi fly kaniharibu ngozi shingoni

Msaada-Nairobi fly kaniharibu ngozi shingoni

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,780
Reaction score
2,556
Jana asubuhi nimeamka na kukuta najisikia muwasho sehemu ya shingo. Nikajua ni kawaida ya matatizo madogomadogo ya mwili. Leo nimeangalia nimekuta kama michirizi shingoni inawasha kwa sababu ngozi yangu ni nyeupe inaonekana sana.

Nimewaonesha watu wenye experience wananambia ni mdudu anayeitwa nairobi fly kanipitia. Sasa wakuu naombeni msaada jamani dawa nayoweza kutumia kuzuia asiniharibu ngozi mwili mzima kwa sababu kwa mbali naona ishaanza kubabuka sehemu za shingoni.

Kama kunamtu ili tatizo lishawahi mkuta naomba anisaidie ushauri jamani sababu nimekosa raha kabisa.

Akhsanteni
 
nadhani anaitwa narrow bee fly, na sio Nairobi fly, watu walikua wanakosea matamshi.
 
Hiyo michubuko ikitoka wala hakuna madhara ya kutisha ...baada ya siku chache utakuwa kama ulivyokuwa wala huna sababu ya kutafuta dawa zaidi ufanye jitihada asikurudie huyo mdudu.
 
Hao wadudu ni nouma. Hawana tofauti na tindikali. Wanapatikana sana mikoa ya kilimanjaro, Arusha.

Paka dawa ya meno. Nakumbukia kipindi hicho o-level. Mtu akitembelewa na hao wadudu alikuwa anapaka dawa ya meno.

Ukiwahi inasaidia.
 
nadhani anaitwa narrow fly, na sio Nairobi fly, watu walikua wanakosea matamshi.....

yap mkuu,ni makosa ya kimatamshi tu.kama ushawahi kuexperience kitu kama hicho naomba ushauri wako namna ya kupungu michubuko yake
 
Hiyo michubuko ikitoka wala hakuna madhara ya kutisha ...baada ya siku chache utakuwa kama ulivyokuwa ...wala huna sababu ya kutafuta dawa .....zaidi ufanye jitihada asikurudie huyo mdudu.

kwani mkuu kunauwezekano akanirudia tena huyo mdudu,i mean anaweza akawa amejificha kwenye kitanda nacholalia??
 
kwani mkuu kunauwezekano akanirudia tena huyo mdudu,i mean anaweza akawa amejificha kwenye kitanda

ukiona yupo mmoja ujue wapo wengi hapo sehem,haijalishi kama wameshakutembelea wana uwezo wa kukuaribu tena sehem nyingine tofauti.siwapendi hao wadudu kabisa hawana adabu
 
Pole ndugu yangu,HILI NI JANGA JINGINE KWA HUKU KILIMANJARO MOSHI sehemu ya marangu Chuoni takriban kila siku wanachuo 10 huunguzwa na huyu mdudu kwa msimu huu wa mvua but dawa nackia dawa ya meno ila ni hatari sana watu sura zishaharibiwa vibaya wadada weupe khaaaa ndo hatari.hawana dawa zaid ya kumtafuta na kumuuaaa
 
nadhani anaitwa narrow fly, na sio Nairobi fly, watu walikua wanakosea matamshi.....

There is a difference between the bee fly (Bombyliidae) which is a 'fly' and the Nairobi fly (Paederus) which is actually a 'beetle'.
 
Mi aliwahi kunibabua sehem ya misuli wa mguu. Nlikua moshi kibosho. Sikupaka dawa niliwacha hadi pakasafika penyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom