Msaada: Nahisi nimepotea humu Dar es Salaam

Msaada: Nahisi nimepotea humu Dar es Salaam

Nipo Mikocheni karibu na kituo cha polisi, nataka nirudi Kimara lakini nahisi nimepotea.

Nifanyeje nirudi Kimara ndugu zangu, nilikuwa natokea Makumbusho nikajikuta nashukia Mikocheni.

Nifanyeje nirudi Kimara usiku unaingia, si ndo nitapotea zaidi?
Trap trap trap......
 
Tumia Google map
 
Mwai Kibaki Road ni hii Old Bagamoyo Road... Panda Magari ya Kawe - Buza au Kawe - Mbagala au Kawe - Temeke Ushukie Morocco (nauli 400) then Morocco unaweza kupanda Mwendokasi moja kwa moja hadi Kimara...

Au ukifika Morocco panda gari za Masaki - Simu2000 (nauli 400) mpaka Mawasiliano. Ukifika Mawasiliano panda gari za kwenda Kimara.

Option nyingine; hapo ulipo panda gari zinazoenda Kawe (nauli 400) ukifika Kawe panda gari zinazoenda Mbezi (nauli 500) ukifika Mbezi panda gari zinazoenda Kimara (nauli 400)

Option ya tatu; panda gari zinazoenda Kawe (Nauli 400), ukifika Kawe panda gari zinazoenda Mawasiliano (nauli 400),ukifika Mawasiliano panda gari zinazoenda Kimara (nauli 500).

Ushindwe wewe tu.
Ok vizuri umeeleza ila kwa mgeni gari ya kwenda kimara unamchanganya maana kuuliza kashindwa so hatakuwa anasoma hivyo kuona gari la kimara hakuna ni mbezi ndoo linapitia kimara kupitia moro road
 
Mwana mpotevu na leo tunaomba utoke upotee. Mungu asaidie upotelee mitaa yangu, nataka kukupa msaada wa Kimwili na akili
 
Uncle dereva kwako sijipotezi nipe lokeshen chap naibuka kama upepo 😂😂😂

Hivi mleta mada alifanikiwa kurudi kwao salama kweli

Leo ni sikukuu uncle dereva na sioni mwaliko ujue😎

☺️

Aunt abiria ubwabwa wa sikukuu tulikuwa tuufinye wote huko ungindoni, vile kuanzia jana nipo mji mdogo wa Muheza kusalimia ndugu na jamaa...
 
☺️

Aunt abiria ubwabwa wa sikukuu tulikuwa tuufinye wote huko ungindoni, vile kuanzia jana nipo mji mdogo wa Muheza kusalimia ndugu na jamaa...
Hakuna kilichoharibika uncle dereva..kama huko Muheza ni Kwema basi hilo ndilo la msingi zaidi..

Ukuje na maembe + machungwa 😉😉
 
Nipo Mikocheni karibu na kituo cha polisi, nataka nirudi Kimara lakini nahisi nimepotea.

Nifanyeje nirudi Kimara ndugu zangu, nilikuwa natokea Makumbusho nikajikuta nashukia Mikocheni.

Nifanyeje nirudi Kimara usiku unaingia, si ndo nitapotea zaidi?
Nguo ulizo vaa uzivue, halafu uzipindue ndani kuwe nje halafu uzivae! Mara utakumbuka njia
 
Hakuna kilichoharibika uncle dereva..kama huko Muheza ni Kwema basi hilo ndilo la msingi zaidi..

Ukuje na maembe + machungwa 😉😉

Huku kwema kabisa aunt abiria, mvua tu ndio kero...

Msimu wa 🥭 ni kama umeisha, naona kuna viembe vidogo sijui ndio waviitaje huku, machungwa 🍊 naona yapo yapo haya
 
Huku kwema kabisa aunt abiria, mvua tu ndio kero...

Msimu wa 🥭 ni kama umeisha, naona kuna viembe vidogo sijui ndio waviitaje huku, machungwa 🍊 naona yapo yapo haya
Jambo la kheri kama ni Kwema uncle dereva..
Usijali kuhusu mvua itakata tu😊

Hakuna shida chochote kitakachopatikana..hata usipopata chochote ila uzima na afya yako na wapendwa wako ni zawadi pia..ok!
 
Back
Top Bottom