Umewahi kutapeliwa?

Umewahi kutapeliwa?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
3,967
Reaction score
12,572
Ilikuwa 2022 tuko kijiweni mida ya saa tano asubuhi, muda huo tume paki Pikipiki tuna piga stori, mara ikaja gali ndogo ya abiria akawa ameshuka jamaa ana begi dogo Mgongoni.

Kama ilivyo kawaida bodaboda tukiona Abiria huwa tuna mkimbilia, Sasa tulivyo mkimbilia yule jamaa yeye akakataa akasema anataka kwanza aongee na simu akitaka kuondoka atakuja achukue boda mmoja aondoke, tukasema sawa tukarudi kupaki boda zetu tuka endelea na stori, muda huo jamaa yuko pembeni yetu Kwa mbali kidogo akiongea na simu.

Kumbe bwana, muda huo jamaa siyo kwamba alikuwa ana ongea na simu, bali alikuwa ana angalia ni Pikipiki ipi ambayo bado ni mpya.

Jamaa alivyo maliza kuongea na simu nikashangaa Moja Kwa Moja ananifuata Mimi, akaniuliza dogo vipi unazijua Mashine zote zinazo koboa na kuuza Mchele hapa? Nikasema zote nazijua kaka halafu Mimi ni kontawa hapa mjini, jamaa akasema sawa, akaniambia yeye ni mfanyabiashara wa Michele ametoka Dar hivyo anahitaji kilo 3000, akaniomba Kwa siku zote ambazo atakuwa ananunua mchele Mimi ndo niwe bodaboda wake, nikasema hizi si ndo Dili zenyewe Sasa.

Jamaa nilianza kumzungusha kwenye Mashine zote kuanzia muda huo huo, akawa anaenda kuongea na Wafanya Biashara huku Mimi nimemsubiri nje, wakawa wana kubaliana Bei.

Siku hiyo ya kwanza mida ya jioni nikampeleka gesti ambayo atakuwa analala, kitu Cha kushangaza akanilipa elfu 40 huku chakula Cha mchana kaninunulia yeye, na kizuri zaidi hata chakula Cha usiku akaniambia tule wote pale gesti, akalipia yeye, tulivyo maliza kula nikaondoka zangu Geto na elfu 40 yangu mfukoni,

Kesho yake tena kama kawaida, nikamfuata gesti tukaanza kuzunguka mashineni kama kawaida akawa anaongea na wamiliki wa Mashine wamuandalie mchele, Yani ikawa inakuwa hivyo Kila tukienda mashineni, ikifika Mchana tuna enda hotelini ananiambia agiza msosi unao utaka, nikiagiza analipia halafu tunakaa hapo tuna piga stori Kwa sana, Yani nikajikuta mshikaji namuona kama ndugu yangu.

Sasa bwana, siku ya tatu nikamfuata asubuhi pale gesti, nilivyo fika tu akaagiza supu ya samaki na chapati mbili mbili tukala, tulivyo maliza akanipa elfu 40 akaniambia Dogo chukua hii elfu 40 yako mapema mana Leo naweza kulipia mchele,

Sasa bwana tukaenda Mashine Moja hivi tuka Kuta tayari Kuna wauzaji watatu wamesha timiza kilo 3000, kweli jamaa akazicheki akaona ziko fresh, Sasa akawaambia inatakiwa mchele waupake mafuta ndo waupakie kwenye magunia.

Pale Mashineni pembeni Kuna wauzaji wa magunia akawaambia anahitaji gunia sikumbuki zilikuwa ngapi, wakampa gunia akawapa wale wapakiaji ambao ndo walikuwa Wana husika na kuupaka mchele mafuta, akawaambia anaenda benki kutoa pesa za kuwalipa wenye mchele, wapakiaji kwenye magunia ambao ndo pia walikuwa Wana upaka mafuta mchele.

Sasa jamaa akawaambia, bakini na huyu dogo Mimi naenda benki kutoa pesa Ili niwalipe wote, jamaa akaondoka na Pikipiki yangu bwana.

Mimi bwana nikabakia pale kama Bosi huku nime wasimamia wanao paka mchele mafuta na kupakia kwenye magunia.

Mara ikapita nusu saa nikaanza kuulizwa vipi dogo huyo ndugu yako mbona harudi, nikawaambia atarudi tu labda pale benki foleni halafu kingine ameenda kutoa pesa Ndefu, wakasema poa, mara ikafika dakika arobaini wakaniuliza tena, Dogo vipi Sasa hii kazi tuna elekea kumaliza ndugu yako mbona hatokei? Ikabidi nimpigie simu nimwambie Mimi nasumbuliwa hapa, hapo Mimi Sina wasiwasi Wala nini, Ile napiga simu naambiwa namba haipatikani, nikarudia tena, haipatikani, ikabidi nisimame nianze kuangaza huku na kule, hapo muda unazidi kwenda.

Ikafikia hatua watu wakamaliza kupakia mchele kwenye magunia yote na kufunga, Sasa wakaanza kuniuliza vipi ndugu yako mbona harudi Sasa, nikawaambia hapatikani, Sasa walivyoona kama Mimi mwenyewe nimeanza kuwa na hofu ndo wakaniuliza kwani ni nani yako? Ndo nika waeleza ukweli wote nilivyo kutana naye, ndo wakaniambia dogo Usha tapeliwa Pikipiki tayari, ndo hapo hapo nikaamini nime tapeliwa tayari.

Tukapiga simu polisi kutoa taarifa, wakaniuliza ni muda Gani umepita? Nikawaambia ni saa Moja hivi, polisi wakasema hiyo kuipata ni ngumu kama ni Mwizi tayari kashavuka mji tayari.

Sasa wale wauzaji wa mchele wakapatwa na hasira mchele wao umepakwa mafuta, na Kila mmoja alikuwa na kilo zake na zimesha chang'anywa tayari, bado aliye toa gunia, wakaanza kunishambulia Kwa maneno, wakanizonga sana, namshukuru mama mmoja hivi ndo aliye niokoa mana Mimi mwenyewe nilikuwa sijielewi muda huo, Pikipiki ndo ilikuwa na miezi minne tu, Pikipiki yangu ya Mkataba ikawa imepotea hivyo na sikuwahi kuipata mpaka Leo, nikaachana kabisa na kazi ya ubodaboda nikajifunza ufundi simu.

Watu wote walio kuwepo pale Mashineni siku hiyo walikubali kuwa , hata wao wange tapeliwa tu kivyovyote.

Mimi nilikuwa nasema siwezi kutapeliwa ila huwezi amini siku hiyo nilitapeliwa mpaka nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe, niliambulia laki na ishirini Kwa yule jamaa halafu yeye akaondoka na Pikipiki ya milioni tatu na laki tatu 😁.

Note: hii stori si yangu, nimeikuta mahali nikaona ni share.
 
Pole sana.

Nakumbuka kipindi Toyota Noah zinatrend kuna jamaa aliiba Kwa mtindo kama huo.kumbuka hiyo Noah ilikuwa moja tu kijiji kizima

Picha linaanza jamaa alifika kwenye kijiwe fulani akiwa anaonesha ana huzuni fulani (alijua watamuuliza)

Kweli kama kawaida ya waswahili wakamuuliza kulikoni,ndipo akasema yeye na ndugu yake ni wageni kwenye hicho kijiji ambapo walifikia mashambani kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Akaeleza kuwa huyo ndugu yake alishikwa na homa Kali wakamkimbiza katika kituo cha afya cha pale, hata hivyo amepoteza Maisha ,wakati huo anasimulia mwanaume analia huku wenyeji (wenyemji) wakimfariji wakimtaka ajikaze kiume.

Walivyohoji kwamba mwili uko wapi akadai upo mortuary,hata hivyo anaomba ikiwezekana Huyo ndugu yake azikwe tu,kwani Kwa mujibu wa Sheria za kiislamu zinamtaka mtu akifa asicheleweshwe (hapa alizipanga Beki vizuri 😂kwani wenyeji wa kijiji kile 99% ni waislamu.

Wazee Kwa vijana wakampongeza Kwa kuijua dini na uamuzi wake wa kuzika,ikabidi wamuoneshe makaburi yalipo ili taratibu za kuchimba zianze Jamaa akawaambia kuwa ndugu yake alikuwa ni mtu muhimu na ndiye aliyekuwa na pesa za mradi wao hivyo asingependa azikwe kama mbwa ,anachotaka lipatikane gari ambalo litabeba mwili wa ndugu yake from health centre to makaburini akidai gharama si Tatizo kwani hata hizo pesa zitazotumika ni za Huyo marehemu, akadai ni muhimu ndugu yake azikwe kifahari.

Kweli zikapendekezwa gari zote zikaonekana hazifai ndipo alipojitokeza mtu mmoja mwenye noah yaje huku akitamka pesa ndefu ambapo jamaa hakupinga ,akatoa kibunda kilichowashtua wanaume wenye tamaa ,huku akidai lazima ipatikane nyumba ambapo itakuwa kama sehemu rasmi ya msiba na kuomboleza.(Hapa alocheza kama kiungo kifupi alitawala Dimba😂)

Basi wakapelekwa vijana kadhaa kwenda kuchimba kaburi tena Kwa malipo jambo ambalo pale kijijini lilikuwa geni mno,watu wakaingia kwenye noah kwenda makaburini huku jamaa Kwa utanashati akikabidhiwa gari na kwani muonekano alionesha ni dereva,jamaa akawa anaendesha huku akifuta machozi kila saa kuonesha kaumizwa na msiba wa ndugu yake.

Wakati kazi ya kuchimba kaburi inaanza jamaa aliwasha gari na kurudi mtaani ,watu wakaingia na wadiwasi kidogo lakini kwakuwa alikuwa ni tapeli mzuri alirudi akiwa na katoni kadhaa za maji ya kunywa kwaajili ya wachimbani wa kaburi huku akiwa na mchele na Vitu vingine akadai anavipeleka kwenye nyumba ambayo walipanga kama ni sehemu maalumu ya kuomboleza.
Watu waliamini huku akiwaambia amaamini kaburi lipo tayari na akitoka kushusha vyakula atawachukua waende Hadi hospital kuchukua mwili wa ndugu yake.(Hapa alikuwa anacheza kama Striker kwani hakuwa na muda wa kupoteza alikuwa yeye na goli.

Unadhani arudi kufanya nini?

Vyakula akashushe ale nani?

Mjini akili,kama kijanja kaa kitaalamu.
 
Ilikuwa 2022 tuko kijiweni mida ya saa tano asubuhi, muda huo tume paki Pikipiki tuna piga stori, mara ikaja gali ndogo ya abiria akawa ameshuka jamaa ana begi dogo Mgongoni.

Kama ilivyo kawaida bodaboda tukiona Abiria huwa tuna mkimbilia, Sasa tulivyo mkimbilia yule jamaa yeye akakataa akasema anataka kwanza aongee na simu akitaka kuondoka atakuja achukue boda mmoja aondoke, tukasema sawa tukarudi kupaki boda zetu tuka endelea na stori, muda huo jamaa yuko pembeni yetu Kwa mbali kidogo akiongea na simu.

Kumbe bwana, muda huo jamaa siyo kwamba alikuwa ana ongea na simu, bali alikuwa ana angalia ni Pikipiki ipi ambayo bado ni mpya.

Jamaa alivyo maliza kuongea na simu nikashangaa Moja Kwa Moja ananifuata Mimi, akaniuliza dogo vipi unazijua Mashine zote zinazo koboa na kuuza Mchele hapa? Nikasema zote nazijua kaka halafu Mimi ni kontawa hapa mjini, jamaa akasema sawa, akaniambia yeye ni mfanyabiashara wa Michele ametoka Dar hivyo anahitaji kilo 3000, akaniomba Kwa siku zote ambazo atakuwa ananunua mchele Mimi ndo niwe bodaboda wake, nikasema hizi si ndo Dili zenyewe Sasa.

Jamaa nilianza kumzungusha kwenye Mashine zote kuanzia muda huo huo, akawa anaenda kuongea na Wafanya Biashara huku Mimi nimemsubiri nje, wakawa wana kubaliana Bei.

Siku hiyo ya kwanza mida ya jioni nikampeleka gesti ambayo atakuwa analala, kitu Cha kushangaza akanilipa elfu 40 huku chakula Cha mchana kaninunulia yeye, na kizuri zaidi hata chakula Cha usiku akaniambia tule wote pale gesti, akalipia yeye, tulivyo maliza kula nikaondoka zangu Geto na elfu 40 yangu mfukoni,

Kesho yake tena kama kawaida, nikamfuata gesti tukaanza kuzunguka mashineni kama kawaida akawa anaongea na wamiliki wa Mashine wamuandalie mchele, Yani ikawa inakuwa hivyo Kila tukienda mashineni, ikifika Mchana tuna enda hotelini ananiambia agiza msosi unao utaka, nikiagiza analipia halafu tunakaa hapo tuna piga stori Kwa sana, Yani nikajikuta mshikaji namuona kama ndugu yangu.

Sasa bwana, siku ya tatu nikamfuata asubuhi pale gesti, nilivyo fika tu akaagiza supu ya samaki na chapati mbili mbili tukala, tulivyo maliza akanipa elfu 40 akaniambia Dogo chukua hii elfu 40 yako mapema mana Leo naweza kulipia mchele,

Sasa bwana tukaenda Mashine Moja hivi tuka Kuta tayari Kuna wauzaji watatu wamesha timiza kilo 3000, kweli jamaa akazicheki akaona ziko fresh, Sasa akawaambia inatakiwa mchele waupake mafuta ndo waupakie kwenye magunia.

Pale Mashineni pembeni Kuna wauzaji wa magunia akawaambia anahitaji gunia sikumbuki zilikuwa ngapi, wakampa gunia akawapa wale wapakiaji ambao ndo walikuwa Wana husika na kuupaka mchele mafuta, akawaambia anaenda benki kutoa pesa za kuwalipa wenye mchele, wapakiaji kwenye magunia ambao ndo pia walikuwa Wana upaka mafuta mchele.

Sasa jamaa akawaambia, bakini na huyu dogo Mimi naenda benki kutoa pesa Ili niwalipe wote, jamaa akaondoka na Pikipiki yangu bwana.

Mimi bwana nikabakia pale kama Bosi huku nime wasimamia wanao paka mchele mafuta na kupakia kwenye magunia.

Mara ikapita nusu saa nikaanza kuulizwa vipi dogo huyo ndugu yako mbona harudi, nikawaambia atarudi tu labda pale benki foleni halafu kingine ameenda kutoa pesa Ndefu, wakasema poa, mara ikafika dakika arobaini wakaniuliza tena, Dogo vipi Sasa hii kazi tuna elekea kumaliza ndugu yako mbona hatokei? Ikabidi nimpigie simu nimwambie Mimi nasumbuliwa hapa, hapo Mimi Sina wasiwasi Wala nini, Ile napiga simu naambiwa namba haipatikani, nikarudia tena, haipatikani, ikabidi nisimame nianze kuangaza huku na kule, hapo muda unazidi kwenda.

Ikafikia hatua watu wakamaliza kupakia mchele kwenye magunia yote na kufunga, Sasa wakaanza kuniuliza vipi ndugu yako mbona harudi Sasa, nikawaambia hapatikani, Sasa walivyoona kama Mimi mwenyewe nimeanza kuwa na hofu ndo wakaniuliza kwani ni nani yako? Ndo nika waeleza ukweli wote nilivyo kutana naye, ndo wakaniambia dogo Usha tapeliwa Pikipiki tayari, ndo hapo hapo nikaamini nime tapeliwa tayari.

Tukapiga simu polisi kutoa taarifa, wakaniuliza ni muda Gani umepita? Nikawaambia ni saa Moja hivi, polisi wakasema hiyo kuipata ni ngumu kama ni Mwizi tayari kashavuka mji tayari.

Sasa wale wauzaji wa mchele wakapatwa na hasira mchele wao umepakwa mafuta, na Kila mmoja alikuwa na kilo zake na zimesha chang'anywa tayari, bado aliye toa gunia, wakaanza kunishambulia Kwa maneno, wakanizonga sana, namshukuru mama mmoja hivi ndo aliye niokoa mana Mimi mwenyewe nilikuwa sijielewi muda huo, Pikipiki ndo ilikuwa na miezi minne tu, Pikipiki yangu ya Mkataba ikawa imepotea hivyo na sikuwahi kuipata mpaka Leo, nikaachana kabisa na kazi ya ubodaboda nikajifunza ufundi simu.

Watu wote walio kuwepo pale Mashineni siku hiyo walikubali kuwa , hata wao wange tapeliwa tu kivyovyote.

Mimi nilikuwa nasema siwezi kutapeliwa ila huwezi amini siku hiyo nilitapeliwa mpaka nikikumbuka huwa nacheka mwenyewe, niliambulia laki na ishirini Kwa yule jamaa halafu yeye akaondoka na Pikipiki ya milioni tatu na laki tatu 😁.

Note: hii stori si yangu, nimeikuta mahali nikaona ni share.
Chai
 
Back
Top Bottom