Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Bei zinatofautiana sana kwa sababu zifuatazo. Ubora wa miche, location na muuzaji mwenyewe alivyoipata. Jana nimenunua Tabata Aroma pale, bei ni Tsh 1000/ kwa mche, nikaacha kununua Mbagala mwisho pale jamaa anauza 500/ kwa mche sababu ya ubora. Pia niliacha kununua Mkuranga mjini kwa sababu ya bei kuwa kubwa, ni Sh 3000/ kwa mche. Wastani wa bei ni Tsh 400/ mpaka 4000/ kwa mche.

Pia waweza tumia cuttings, kila cutting moja huuzwa Tsh 200/ na inasafirishwa toka Tanga. Hii njia ni nzuri kama una large scale na mvua zipo. Ila kwa mwaka huu mvua ni magumashi, usijaribu labda huko Tanga ambako mvua ziko.

Malila unaweza nijuza mbagala na aroma maeneo gani yenye miche ya mitiki, nataka ninunue kama mia mbili hivi.
 
Malila unaweza nijuza mbagala na aroma maeneo gani yenye miche ya mitiki,nataka ninunue kama mia mbili hivi.

Ukifika Tabata Aroma, iko pembeni kulia kwako kama umetoka mjini kwenda Segerea. Miche yao mingine ipo Kinyerezi mwisho wa lami.Bei ni Tsh 1000/ ni miche yenye ubora ukilinganisha na Mbagala.

Ukifika Mbagala inapoishia dabo ROAD mpya, unaanza mtelemko kwenda Kongowe, kabla hujavuka daraja, unaingia mkono wa kulia, mita kama mia hivi ndani, acha maua yaliyopo barabarani, fuata hicho kinjia.Bei ni Tsh 500/ ila ubora wake kama shamba halina unyevu wa kutosha ni mdogo.
 
Ok nitaenda huko! Thanx.
 
Vipi kuhusu soko la mbao dar? Nachotaka kujua ni kuhusu soko kama ni kubwa.
 
Mkuu malila nilikuwa naomba kujiunga na umoja wenu wakibihashara hasa wakupanda miti je nitafanyaje!
Tafadhali naomba unijibu!
 
Mkuu malila nilikuwa naomba kujiunga na umoja wenu wakibihashara hasa wakupanda miti je nitafanyaje!
Tafadhali naomba unijibu!

Karibu sana,
Hakuna kiingilio kabisa, cha umuhimu ni uaminifu wako tu, nipe mail yako kupitia pm ili tuanze mawasiliano ya moja kwa moja.
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.

Mkuu huu ushauri wako na ulichokifanya nimekipenda na ntatekeleza kwa kukuiga ili kudumisha ushauri wako
 
Vipi kuhusu soko la mbao dar ? Nachotaka kujua ni kuhusu soko kama ni kubwa

Kwa kweli soko la mbao ni kubwa sana hapa hapa nchini na nje ya nchi. Kwa sasa mbao za Tanzania zinauzwa Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Somalia hadi uarabuni. Ukitaka kujua ukubwa wa soko hili nenda Morogoro uhesabu malori yanayoleta mbao kutoka nyanda za juu kusini. Mbao nyingine zinatoka mpaka Malawi.

Kwa maoni yangu soko la mbao litazidi kupanuka ingawaje uzalishaji kwa miaka kadhaa ijayo utakuwa chini kutokana na kuisha kwa miti hasa huko vijijini. Hivyo bei itazidi kupanda na siyo kushuka. Mahitaji ya mbao yatazidi kwenda juu kwani wengi siku hizi wanajitahidi kujenga nyumba bora, mpaka huko vijijini. Mbao za asili kama mninga, mvule, n.k haziwezi tena kutumika kwenye kazi za kuezekea majumba kutokana na bei zake kuwa kubwa mno.
 
Mkuu mninga unachukua muda gani mpaka kuuvuna? Mimi huwa naiona vijijini lakini nikiuliza una umri gani huwa sipati majibu yenye uhakika. Mninga ni utajiri.

Pia niliona kwenye maonesho ya kilimo mwaka fulani. Kuna gereza moja huko kilimanjaro wanatengeneza furniture (nyeupe) nzuri sana kwa kutumia muarobaini.
 
Mninga/Mvule ili uvunwe unahitaji miaka isiyopungua sabini. Kwa hiyo ukipanda wewe atavuna mjukuu wako.
 
Jamani maeneo ya chalinze -- lugoba ni miti gani inastawi vizuri.

Maeneo yale ni makame sana, miarobaini inaweza kustawi ila jamii nyingine ni ngumu sana kukua kibiashara. Kama unaingia Chalinze ukitokea huku Dar, kuna mitiki upande wa kushoto, ipo na haiongezeki kimo wala unene. Sijui Msederela kama unaweza kumea na kukua kibiashara.
 
Maeneo yale ni makame sana,miarobaini inaweza kustawi ila jamii nyingine ni ngumu sana kukua kibiashara. kama unaingia Chalinze ukitokea huku Dar,kuna mitiki upande wa kushoto,ipo na haiongezeki kimo wala unene. Sijui Msederela kama unaweza kumea na kukua kibiashara.

Hivi miarobaini inafaa kwa mbao? Mbona kama vile huwa haikui sana kwenda juu?
 
KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!

Wenger...!!! Nadhani wewe tunaweza kwenda pamoja jamaa yangu, Ebana unaweza kunidokeza kidogo acre moja maeneo ya huko inauzwaje...???/

Mninga/Mvule ili uvunwe unahitaji miaka isiyopungua sabini.Kwa hiyo ukipanda wewe atavuna mjukuu wako.

miaka 70! sipo tayari kwa hili. Ngoja niendelee kufanya utaratibu wa kumiliki ardhi kisheria maana hizi projects za muda mrefu ni lazima uwashirikishe watu wa ardhi kikamilifu kabla ya kuanza kupanda miti. Tuliangalie kwa umakini hili swala, watu wengi wamepoteza ardhi kwa kutofuata taratibu za umiliki
 
Back
Top Bottom