Patandi
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 397
- 371
Wakuu heshima kwenu.
Naomba msaada wenu kuhusu matibabu sahihi ya ugonjwa wa akili na mahali yanapopatikana. Nina ndugu yangu alianza kusumbuliwa na ugonjwa huu tangu akiwa mdogo. Baada ya kutibiwa huku kijijini bila mafanikio alipelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Pale Muhimbili alifanyiwa kipimo cha EEG na report yake ilisemahivi:
"The EEG tracing shows an abnormal background predominantly theta activity mingled with delta sharp complexes. The frequency range from 4.3 to 9.9Hz. Amplitude range from 38.2 to 70.6 uV. Photo-stimulation and hyperventilation provoked no further abnormal activity.
Conclusion: - EEG shows an abnormal backgound. Hyperventilation and Photic stimulation provoked no further abnormal activity. This is in keeping with seizure disorder."
Baada ya hapo ameendelea kutibiwa katika Hospital mbalimbali ikiwemo Muhimbili, Hospital ya Mkoa Iringa, Hospital ya Rufaa Mbeya,Bagamoyo Mental Health Facility, Korogwe na Mirembe National Mental Health Hospital.
Dawa ambazo amepata kuzitumia na baadhi anaendelea kuzitumia ni kama ifuatavyo; Haloperidol tabs, Carbamazepine tabs, Lagactil inj, Diazepam tabs na inj, Modical, Halotex tabs Tagretal tabs, Promethazine tabs n.k
Dawa hizo ameanza kuzitumia tangu mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 10 lakini mpaka leo hakuna mafanikio. Hali inazidi kuwa mbaya. Amekuwa na hasira nyingi, mkali, anapiga watu, anahararibu majengo na magari ya watu ya watu. Kwa ujumla amekuwa tishio kwa watu na vitu.
Tumejaribu kuonana na viongozi wa serikali na vyombo vya usalama ili aweze kupelekwa mahali ambapo atakuwa salama zaidi ili jamii na mali zao waepukane na changamoto wanazopitia lakini hatujafanikiwa.
Kupitia uzi huu tunaomba yeyote mwenye msaada wa aina yoyote ya kutuwezesha kupata mahali ambapo anaweza kwenda kupata matibabu ambayo yamponya na kuweza kuishi na jamii inayo mzunguka kwa amani atusaidie.
Muda aliokaa Mirembe wanasema kufuatana na kanuni zao unatosha na hawawezi kumpokea tena . Tufanyaje ili kunusuru maisha yake na ya jamii huku tunakoishi.
Tunatanguliza shukurani zetu.