Ufahamu Ugonjwa wa Kifafa na namna bora ya Kuishi na Wagonjwa wa kifafa

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
JFSpaces 10FEB 2.jpg

Kifafa ni hali ya mshtuko wa ghafla au matokeo yasiyo ya kawaida katika Ubongo wa Binadamu ambayo inaweza kusababisha Mtu kuzimia, kukamaa kwa misuli na mabadiliko ya hisia au fahamu

Hali hii inaweza kuathiri Watu kwa njia tofauti kutegemea na eneo la Ubongo linaloathiriwa.

Kufahamu zaidi kuhusu Kifafa, ungana nasi katika Mjadala utakaoendeshwa na Wataalam kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Februari 10, 2024 saa 10:00 hadi 12:00 Jioni Kupitia X Space ya JamiiForums.

Link ya Mjadala https://jamii.app/MNHSession

Pia unaweza kuweka maswali au maoni yako katika uzi huu, yatasomwa siku ya mjadala.

Unaweza kusoma zaidi hapa kujua kuhusu KIFAFA

Wengi wanaamini ni ugonjwa unaoambukiza na pia unatokana na mapepo. Watu milioni moja wanaugua ugonjwa huo Tanzania

Si ugonjwa unaoambukiza, lakini uzoefu unaonyesha wagonjwa wake wamekuwa wakikosa ukaribu kutoka kwa wanajamii wengine.

Hawa ni wagonjwa wa kifafa, ugonjwa ambao wataalamu wanasema unatokana na hitilafu au jeraha katika ubongo linalosababisha mgonjwa kuanguka, kukakamaa, kuzimia na wakati mwingine kutoa povu mdomoni.

Hali huwa ngumu zaidi pale wagonjwa hao wanapoanguka; jamii inayowazunguka imekuwa ikishindwa kuwasaidia kwa wakati kwa kudhani ni mapepo.

“Jambo hili limefanya asilimia 75 ya wagonjwa wa kifafa Tanzania kupelekwa kutafuta tiba kwa waganga wa kienyeji na baadhi ya viongozi wa kidini wakiamini kuwa mgonjwa amevamiwa na mapepo mabaya au mashetani,” anasema Dk Edward Kija ambaye ni bingwa wa mfumo wa fahamu na ubongo kwa watoto wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Mbali na hilo pia asilimia 50 ya wanajamii bado wanaamini kuwa kifafa ni ugonjwa wa kuambukiza, hivyo huwanyanyapaa wagonjwa na kuwasababishia msongo wa mawazo.

“Hali hii hutokea pale mgonjwa anapopata degedege na kudondoka, wengi hufikiri kuwa ukigusa povu analotoa mdomoni au akitoa hewa chafu na ukanusa basi nawe utapata ugonjwa huo,” anasema na kuongeza: “Hali hii imekuwa ikifanya wananchi kushindwa kuwapeleka wagonjwa hospitali waweze kupatiwa tiba, kwa sababu ya imani kwamba wamerogwa au wameingiwa na mashetani.”

Huduma kwa mgonjwa wa kifafa

Anasema jamii inapaswa kutambua kuwa mtu anapokuwa katika hali hiyo anahitaji msaada wa haraka ikiwamo kwa kuangalia degedege hilo limetokea katika sehemu gani ili athari zaidi zisitokee.

“Watu wanaomzunguka mgonjwa huyu wanatakiwa kuangalia hali hiyo ikiwa imetokea katika sehemu ambayo huweza kumsababishia madhara zaidi kama kuangukia katika moto au maji, ni lazima aondolewe katika eneo hilo.

Wananchi wasiogope kumgusa mgonjwa aliyepata kifafa hawataambukizwa, wamtoe na wamuweke sehemu salama,” anasema.

Anasema pia kuna watu wenye hofu kuwa mgonjwa huyo anapodondoka atang’ata ulimi, hivyo humuwekea kijiko, kidole au kijiti, kitendo anachosema hakifai.

“Unapoweka kitu mdomoni, unaweza kusababisha njia ya hewa kuziba na hali ikiwa hivyo unaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa,” anasema Dk Kija

Anasema wakati huo pia mgonjwa hutakiwa kutolewa nguo au vitu vinavyombana mwilini mwake au kulegezwa na baada ya hapo anapaswa kulazwa kwa kutumia ubavu wa kushoto hadi pale atakapoamka.

“Hivyo kama unyanyapaa utaendelea kuwepo ni vigumu watu hawa kupata usaidizi wa haraka pale unapohitajika kutokana na watu kuona kama wataambukizwa,” anasema.

Tahadhari kwa wenye kifafa

Mwakilishi wa Chama cha wenye Kifafa Tanzania (Tea), Jane Mwenda anasema jamii inapaswa kutambua pia mtu aliye na ugonjwa wa kifafa hatakiwi kufanya kazi katika jua kali hata kama ni mwanafunzi.

“Tumeshafanya kampeni nyingi kwa sababu kuna walimu mtoto akikosa anamwambia apige magoti juani, lile ni kosa ndiyo maana siku hizi watoto walio na vifafa wana alama nyekundu katika bega ili kuwatambulisha wasifanyishwe kazi ngumu.”

“Lakini watu hawa pia hawaruhusiwi kuvuka barabara peke yao bila msaada wa mtu kwa sababu wanaweza kudondoka katikati ya barabara na watu wakamkimbia wakidhani kuwa ana mashetani,” anasema.

Anasema kwa wale wanaopatwa na kifafa usiku wanatakiwa kuwekewa magodoro yao chini ili wasidondoke.

Takwimu zinasemaje?

Wakati unyanyapaa ukitajwa kama moja ya kitu kinachofanya wagonjwa wa kifafa kukosa matibabu sahihi, takwimu zinaonyesha kuwa watu wanaoishi na kifafa ni zaidi ya milioni 60 duniani kote huku Afrika ikiwa ni bara ambalo limeathirika zaidi na tatizo hilo.

Kwa upande wa Afrika takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watu 1000 basi 20 hadi 50 kati yao wanaishi na tatizo hilo.

Lakini pia kati ya wagonjwa milioni 60 wanaopatikana duniani asilimia 80 kati yake hutokea katika nchi zinazoendelea.

Kwa upande wa Tanzania zaidi ya watu milioni moja ni wagonjwa wa kifafa huku hali ikionekana kuwa mbaya zaidi katika mkoa wa Morogoro kijiji cha Mahenge kutokana na aina ya wadudu wanaopatikana huko.

Wadudu hawa mithili ya nzi waitwao ‘Simulium fly’ wanapatikana katika mito iliyopo maeneo hayo.

Nzi hawa wanapowang’ata watu huwaachia virusi vya ‘Oncocerca volvus’ ambavyo husababisha ugonjwa wa ‘Onchocerciasis’ ambao baadaye huwafanya kupata kifafa

“Jambo hilo liliifanya Serikali kuanza kuwapatia dawa za kuzuia ugonjwa huo mara mbili kila mwaka tangu mwaka 2007,” anasema Dk Mnacho Mohammed ambaye ni daktari bingwa wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kutoka Muhimbili.

Imani potofu

Hapa nchini zaidi ya asilimia 36 ya watu bado wanaamini kuwa ugonjwa wa kifafa unatokana na nguvu za giza.

“Lakini asilimia 60 ya wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu hospitalini hufika mwaka mmoja baada ya kupata tatizo huku wengi wanoishi na kifafa Tanzania ni cha kiwango cha juu,” anasema Dk Mohammed.

Anaongeza: “Ni asilimia tano hadi 10 ya wagonjwa wa kifafa Tanzania ndiyo hupatiwa matibabu hospitalini.”

Dalili za mgonjwa wa kifafa

Wagonjwa wa kifafa huweza kuwa na dalili za aina mbili tofauti ikiwamo kutopoteza fahamu ila anakuwa hajui anachokifanya, kutetemeka kwa sehemu moja ya mwili kama kidole, mkono wote, upande mmoja wa mkono na mguu au upande mmoja wa uso.

Wakati mwingine kama hitilafu itatokea katika ubongo unaoendesha hisia kama harufu au usikivu dalili zake zinaweza kuwa ni kusikia harufu au kelele ambazo kiuhalisia hazipo.

Kama hitilafu itatokea katika ubongo unaoendesha kufikiri au kuongea, mgonjwa huyo ataanza kuongea ovyo, kucheka ovyo au kubadilika kwa hali na mapigo ya moyo.

Sehemu ya pili ya dalili za ugonjwa wa kifafa hutokea pale sehemu mbili za ubongo zinapopata hitilafu mgonjwa huweza kupoteza fahamu, kuanguka na kugeuza macho juu, kutetemeka mwili mzima na wengine hutoa povu mdomoni.

Pia kuanguka na kujigonga usoni hasa kwa watoto au kuzubaa na kuacha anachokifanya.
 
1628658894680.png

Kifafa ni nini?
Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva. Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.

Dalili na ishara za kifafa

Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?

Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya muda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa muda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa nyingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina nyingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je, kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?
La, Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.
  • Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu.
Je, kuna tiba ya kifafa?
Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali nyingine kama vile uvimbe kwenye ubongo, ugonjwa wa figo au ugonjwa wa Ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa muda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.


Namna nyingine za kudhibiti kifafa
Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji angalau masaa 9) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwanini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?
Kwa muda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu nyingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwanini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?
Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.

Matatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu

Je, kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?

Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya muda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.

Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.

Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?
Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa nyingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali nyingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii, dawa ya pili na wakati mwingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.

Ni kwa muda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?
Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote. Katika watoto, hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa ngehitajika kutumia madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi daktari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa kipindi fulani cha muda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.

Ni muda gani unaochukuliwa ili kudhibiti kifafa?
Wagonjwa tofauti wana aina tofauti za kifafa na aina tofauti za kifafa hudhibitiwa kwa njia tofauti.Baada ya kubainika kumehakikishwa, mgonjwa huwekwa kwenye kipimo kimoja cha dawa hapo mwanzoni. Hushauriwa kurudi baada ya mwezi ama zaidi dakitari atathmini ikiwa dawa inadhibiti kifafa kwa njia inayofaa.Ikiwa sivyo, basi kipimo cha dawa huongezwa pole pole. Na ikiwa hii haina mafanikio, basi dawa ya pili huongezwa na ikiwa inahitajika, dawa ya tatu itaongezwa.

Muda unaochukuliwa kwa ugonjwa wa kifafa kudhibitiwa hutofautiana kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mwingine.Ugonjwa wa kifafa wa mgonjwa mmoja unaweza kudhibitiwa kwa dawa moja tu.Katika visa vingine, mgonjwa anaweza kuwa akitumia madawa 3 na bado anaathirika na kifafa, ingawaje idadi ya kuzirai kunakosababishwa na kifafa kutapungua ukilinganisha na hapo awali. Wagonjwa wengine hutibika haraka kuliko wengine na aina nyingine za kifafa huwa rahisi kudhibiti kuliko nyingine.

Hakuna mbinu iliyobainika katika kudhibiti kifafa.Lengo la matibabu ni kupunguza idadi ya kuzirai kunakoathiri mgonjwa na ikiwa inawezekana kusimamisha kuzirai kabisa kwa muda mrefu.

Ni nani yuko kwenye hatari ya kupata kifafa?
Ugonjwa wa kifafa unaweza kuathiri mtu yeyote katika umri wowote. Madhara ya ubongo ndio hali ya kawaida ambayo inaweza kusababisha kifafa baadaye. Matatizo wakati wa kujifungua,homa ya nyonga ya manjano katika mwezi wa kwanza wa maisha, magonjwa ya utotoni kama homa ya uti wa mgongo ni sababu za kawaida za kifafa katika watoto. Homa kali pia husababisha kuzirai kwa watoto wadogo. Katika visa vingine kuzirai huku hufanyika kila wakati kuna homa. Mtoto ambaye amezirai mara tatu ama zaidi ambako kuna uhusiano na homa anafaa kuwekwa chini ya matibabu dhidi ya kifafa.

Watu wazima ambao huathiriwa na madhara ya ubongo kwa sababu ya jeraha, ambukizo ama kwa sababu ya ugonjwa mwingine kama maradhi ya ini, maradhi ya figo wanaweza pia kuathiriwa na ugonjwa wa kifafa.

Ni muhimu kukumbuka ya kwamba ugonjwa wa kifafa unaweza kuwaathiri watu ambao hawana madhara yoyote ya ubongo ama ugonjwa wa hapo awali. Katika visa vingine hutokea katika familia, lakini wakati mwingi hutokea bila ya sababu yoyote inayojulikana.

Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa mtu atashikwa na mshtuko wa kifafa?
Wakati mwingi, huduma ya kwanza ina maana ya kumfanya mtu awe salama wakati mshtuko wa kifafa unapotokea. Kwa bahati nzuri, mshtuko huwa mfupi na huisha baada ya dakika kadhaa.

Hatua ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya kifafa ni kufahamu kitu cha kufanya wakati ugonjwa huu unapotokea. Hii ni muhimu ikiwa unamchunga mgonjwa wa kifafa lakini pia kwa kila mtu. Ugonjwa wa kifafa unaweza kuanza katika umri wowote na kila mtu anahitaji kufahamu nini cha kufanya wakati mtu karibu nao anaathiriwa na kifafa.

Huduma ya Kwanza
  • Kuwa mtulivu na usiogope. Kifafa humuogopesha mtazamaji. Huchukua dakika chache na kwa kawaida huhitaji matibabu.Kumbuka ya kwamba mtu aliyeshikwa na kifafa huwa hafamu vitendo vyake na anaweza au asiweze kukusikia.
  • Walinde dhidi ya majeraha wakati wanaposhikwa na kifafa.Ikiwa inahitajika mweke chini kwa njia iliyo taratibu.
  • Sogeza vitu vigumu, vitu vyenye ncha kali na vilivyo moto na linda kichwa na mwili wa mgonjwa dhidi ya jeraha.
  • Usiweke chochote mdomoni ama ujaribu kubanua meno.
  • Mtu hayuko katika hatari ya kumeza ulimi wake
  • Usijaribu kuzuia mwendo wao kwa kutumia nguvu.Hili linaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia yule anayejaribu kuwasaidia.
  • Popote inapowezekana, jaribu kumlaza mtoto katika sehemu iliyo laini na wageuze upande mmoja.
  • Weka kitu tambarare na laini chini ya kichwa chake ili asijiumize.
  • Fungua nguo zilizombana haswa kwenye shingo kama tai, skafu na kadhalika
  • Usiweke chochote mdomoni.
  • Nakili muda ambao mshtuko umechukua.
  • Jaribu kutazama mwondoko ambao mtu hufanya wakati ameshikwa na kifafa.
  • Wakati mkutuo unaanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.
  • Baada ya kifafa, mvingirishe mtu ili alalie upande mmoja.Hili hufanya mate kutoka mdomoni na kuhakikisha ya kwamba hanyongwi. Ikiwa kuna matapishi, mweke mtu kwa upande mmoja na safisha mdomo wake kwa kidole.
  • Usijaribu kumpatia dawa ama uoevu hadi aamke
  • Waondolee hofu, zungumza nao kwa upole na wasaidie kupata nafuu pole pole.
  • Usimwache mtu pekee yake hadi apate nafuu.
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa nadhani nimeathiriwa na kifafa?
Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kifafa ni hali ambayo inaweza kudhibitiwa. Sio kitu cha kuona haya. Sio laana ama ulemavu. Ni hali inayohitaji matibabu na kufuatiliwa kama hali nyingine kama shinikizo la juu la damu, kisukari, pumu na kadhalika

Ikiwa unadhani ya kwamba umeathiriwa na ugonjwa wa kifafa ama ikiwa umewahi kuanguka chini na kuzimia ni muhimu kutafuta usaidizi wa dakitari aliye karibu. Ikiwa inawezekana andamana na mtu aliyekuwa nawe wakati ikifanyika ili waeleze kile walichokiona. Hili litasaidia dakitari kufanya

Ni sehemu gani ya ubongo huathiriwa na kifafa?
Ubongo ni ogani iliyo na sehemu nyingi (sehemu ya mwili) ambazo hudhibiti mwili wote. Sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili na kazi tofauti kwenye mwili. Kuna sehemu ya ubongo ambayo hudhibiti misuli ya mkono; sehemu tofauti itadhibiti kuhisi uchungu wa mkono huo huo na sehemu tofauti ya ubongo itaratibu sauti ya kupiga mayowe wakati mkono huo unahisi uchungiu ama uko kwenye hatari. Hizi sehemu zimeunganishwa na seli za ubongo (nyuroni). Muungano huu ndio ule unaoturuhusu kufanya kazi kama mtu mmoja kwa njia ya kupatana kwa misuli.

Kifafa ni shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo. Sehemu yoyote ya ubongo inaweza kupatwa na jambo hili lisilo la kawaida. Kwa sababu sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili, hii ndiiyo sababu mtukutiko wa maungo katika kifafa ni tofauti kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ama pia kutoka kwa kuzirai huku na kule. Ikiwa kuna shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo katika sehemu ya ubongo inayoathiri misuli ya mikono na miguu, kutakuweko msukumano mwingi katika hizo sehemu za mwili.

Shughuli hii isiyo ya kawaida kwenye ubongo inaweza kufanyika tu katika sehemu moja ya ubongo ama inaweza kusambaa katika muungano ili kuhusisha ubongo wote.Kuzimia ambako husababishwa na shughuli ya sehemu moja ya ubongo ndio kule tunakokuita kuzirai kusio kamili. Kuzirai kunakosababishwa na shughuli ya ubongo wote ndio kule tunakokuita ugonjwa wa kifafa ulio mbaya ama kuzimia kamili.

Kwa jumla tunaweza kusema ya kwamba ikiwa sehemu ndogo ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mdogo. Ikiwa sehemu kubwa ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mkubwa. Kuzirahi kusio kamili kutaathiri sehemu ndogo ya ubongo kuliko kuzimia kuliko kamili.

Ni vipi naweza kujilinda mimi mwenyewe na familia yangu dhidi ya kifafa?
Njia moja muhimu ya kuwalinda watoto dhidi ya hatari ya kifafa ni kuhakikisha ya kwamba wanapata chanjo zao kwa wakati unaofaa. BCG kwa mfano humlinda dhidi ya kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwa ugonjwa wa kawaida hivi leo na unapoathiri mtoto mdogo ambaye hajapata chanjo, hatari ya kupata ugonjwa homa ya uti wa mgongo (meningitis) huongezeka. Homa ya uti wa mgongo itamweka mtoto kwenye hatari kubwa ya kupata kifafa. Chanjo nyingine maalumu kwa aina tofauti za homa ya uti wa mgongo zinapatikana hospitalini lakini kwa ada.

Homa ni kitu kinachoongezea hatari ya kupatwa na mshtuko ilhali inaweza kudhibitiwa vyema. Mtoto ambaye homa yake inaruhusiwa kupanda juu yuko katika hatari ya kupatwa na mshtuko. Ni muhimu kwa homa kudhibitiwa vizuri pindi tu inapoanza. Udhibiiti wa homa unajumuisha; kutumia dawa kama Panado (paracetamol) ama Brufen (Ibuprofen), mtoe mtoto nguo kisha umpanguze na kitambaa kilicholoweshwa ndani ya maji yenye joto la kadri na la muhimu zaidi ni kutafuta msaada wa matibabu.

Ulinzi dhidi ya jeraha, haswa jeraha kwenye kichwa ambayo ndiyo sababu nyingine ya kifafa. Ulinzi hutokana na kuhakikisha ya kwamba watoto hawezi kuanguka kwa urahisi kutoka katika sehemu iliyo juu, usimamizi unaofaa wanapocheza na kuweka mbali vitu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara wanapocheza. Unaposafiri kwenye gari, ni muhimu kutumia mishipi ya usalama ili kupunguza hatari ya kujeruhiwa ikiwa kutatokea ajali. Jeraha la kichwa ndilo jeraha ambalo hutokea mara kwa mara kukitokea ajali.

Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?
Kuzirai ambako hakuwezi kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba). Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.

Pili, ugonjwa wa kifafa unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu ambayo inaweza kusababisha kifo katika muda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa.

Nitapata usaidizi wapi?
Hospitali iliyo karibu nawe itakutolea usaidizi. Watakuwa na dakitari ambaye atakuchunguza na atakushauri kuhusu uchunguzi wowote ama matibabu ambayo unaweza kuhitaji kutumia.

Uongo unaozungumziwa kuhusu Kifafa

"Kifafa ni aina ya ulemavu kwani huathiri utenda kazi wa ubongo"

Ulemavu ulielezewa vizuri na Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1976. Unatofautisha dhana tatu ambazo hutumiwa sana na unadhihirisha baina ya kudhoofika, ulemavu na upungufu.

Kudhoofika
ni upungufu wowote ama hali ya akili isiyo ya kawaida (saikolojia), utenda kazi wa mwili (fiziolojia) ama muundo wa mwili wa binadamu (anatomia) ama utenda kazi; Ulemavu ni kikwazo ama kukosa uwezo (unaotokana na upungufu) wa kufanya shughuli kwa njia inayochukuliwa kuwa ya kawaida kwa binadamu; Upungufu ni kasoro inayotokea kwa mtu kwa sababu ya kudhoofika ama ulemavu ambao huzuia kutimilika kwa wajibu unaochukuliwa kuwa wa kawaida (kwa kutegemea umri, jinsia na mambo ya ushirikiano wa jamii na utamaduni) kwa mtu huyo.

Kifafa ni matokeo ya utenda kazi wa ubongo usio wa kawaida ama kudhoofika kwa utenda kazi wa ubongo.Huathiri utenda kazi wa ubongo kwa kuendelea na kuwacha. Kuna hali nyingine ambazo huwa na athari inayoendelea na ya muda mrefu. Hizi hali hutokea kama kutoona vizuri, kutowiiana vizuri,kuongea pole pole,kutoweza kumakinika na kusahausahau. Hali hizi huitwa ulemavu ama taahira ya akili.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kumshika mtu mwenye hali/ulemavu mwingine. Unaweza pia kutokea tu wenyewe. Mgonjwa wa kifafa ambaye yuko chini ya matibabu na anafuatiliwa mara kwa mara anaweza kutimiza majukumu yake kama mtu yeyote mwingine. Katika hali hii hadhaniwi kuwa na ulemavu wowote. Ikiwa kuzirai kunakosababishwa na kifafa kumeongezeka na kunamzuia mtu kufanya kazi yake ya kawaida, basi hili huchukuliwa kuwa ulemavu.

"Kifafa hutokea kwa sababu ya kupagawa na mapepo"
Ugonjwa wa Kifafa unatibika kwa dawa za asili hakuna dawa ya hospitali itakayoweza kutibu maradhi ya kifafa.
chanzo. Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu
 
Back
Top Bottom