MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

aisee hizi dini zingine kwa kweli.Mama yako atakuwa hajitambui,yaani ni kama vile mtu akianza kutumia madawa ya kulevya kuacha ni ngumu,ila mama anatakiwa ajitambue,anza kumwambia the bad side of that dini,mengine hata ujitungie ila uiponde sana hiyo dini aloingia huko.Katekwa ufahamu wake,naomba nikuulize ni dhehebu gani hilo?maana siku hizi kuna utitiri wa madhehebu ni ya kiongo ongo tu watu wanadanganywa tena ni ya kishetani ila yanajidai yanamtaja Yesu
 
Mungu yupo na makanisa ya kweli yapo na wokovu pia upo. Tatizo kubwa la RC na makanisa ya wokovu lililopo ni kwamba wanaona RC ni sehem tu ambayo watu ukutana jumapili pia haliwakuzi kiimani waumini wake zaid za kufwata shajala tu na hii ni kweli wa RC wengi hawasomi biblia ila sara zao wamezishika( katekisimu) Pia RC wanaomba sana kupitia watakatifu ambao we are nt sure kama kweli ni saint . Walokole wao wanaomba straight kwa Yesu hakuna kupitia kwa bikira maria, joseph mt agustino hakuna cha rozali wala nin wao ni Yesu. So mtu akiokoka na akiambiwa miaka yote uliyokuwa RC ni bure na ukaamin ni lazima ubadilike. Ndo mana nao Rc wakaanzisha kalismatic kwa ajili ya Wa Rc wenye iman kali ambao ni sawa na walokole. Mama yako yupo sawa tena sana ukimwi wengine wanasema ni pepo ndo mana ukiombewa linatoka ila pia hospital kuna dawa so ugonjwa kutibika hospital haina mana kuwa sio pepo. Kuna mapepo mengine kazi yake ni kukutia umaskin kila mwisho wa mwez lazima uumwe tena ulazwe usidhan ni ugonjwa wa kawaida.
 
Pole sana.

Kitu anachofundishwa mtu na mtu anayemwamini huwa kina athari kubwa sana kijamii kwa mfundishwaji. Suala linalomuathiri mama yako si imani yake kwa Mungu, bali ni imani yake kwa Mchungaji wake. Mchungaji akipotoka, huwapotosha wote walio nyuma yake. Weka akilini kuwa, akili ya mama yako na ufahamu wake umeshikwa na tafsiri mbaya ya maandiko anayoipata kutoka huko anakoabudu. Mama atakuwa ameambiwa kwamba Yesu hakuja kuleta amani bali upanga kwa tafsiri ya kidunia.

Ungekuwa karibu, mtu wa awali wa kuzungumza naye alikuwa Pastor wake. Mimi binafsi, kwa kumsikiliza Pastor maneno yake na mahubiri yake, naweza tu kumbaini mapema ikiwa anaongozwa na 'Roho Mtakatifu' au 'Roho Mtakavitu'. Wachungaji wengi wamekuwa sumu ya imani za watu kwa upotoshaji kwa lengo la kuhamasisha ushabiki na mafarakano kwa manufaa yao.

Labda utajiuliza kwa nini nimekwambia yote haya: nimesema hivi kuyarejelea maelezo yako kuwa baba yako ni mtu mwenye nafasi kiuchumi. Anachokifanya huyo *Roho Mtakavitu* ni kuwakosanisha na kumshikilia mama yako. Once wameachana na kugawana mali, mama yako atapewa cheo kanisani na maelekezo ya pastor yatabadilika. Believe me, shetani hajagi na uongo peke yake, huchanganya uongo na ukweli, ili kwa ile punje ya ukweli upate kumuamini. Hata kama baba yako ni mchawi, Wakristo hatukuambiwa tumnunie shetani, bali tumuondoe. Hakika una wakati mgumu. Omba!
 
Ishu ya uchawi ni ya ndani sana ila napata wasiwasi unaposema babako ni mfanyabiashara mkubwa.
Mimi sikuzote naamini ili uwe mfanyabiashara mkubwa lazima kuikinga biashara yako( zindiko) kufanya biashara ya mkono mweupe dunia hii ni kazi sana either uwe mcha mungu au mshirikina la sivyo wenzio watakuibia kamazingara. Mie nina rafiki yangu babake mchawi ila yeye hajui mana tukiwa kijiweni tunamsema sana mzee wake jamaa akiwa anakuja tunachange mada tunaanza habari za mpira,mziki. So yeye ataweza kujua tu siku akigombana na mtu au mlevi ambwatukie hilo.
 
Kuna uzi fulani kwenye jukwaa la hoja mbali mbali kuhusu Martha agent wa SCOAN hapa Tanzania, inahitaji uvumilivu kupitia njia yake lakini ndio yenye uhakika wa mtu kupata fully attention kwa men of God there, lakini baadhi ya watu wamekuwa wakienda wenyewe na kama ni mpango wa Mungu wanafanikiwa; kama uliona live service ya last Sunday Emmanuel TV kuna mdada mmoja wa Kitanzania alijilipua (ukiwa na shida kweli huwezi kuona aibu kujilipua) na kumlilia T.B Joshua kanisani kuhusu hali ya mama yake ambaye hakupata nafasi ya kuingia kanisani (kipaumbele ni wenye appointment) na T.B Joshua alimuattend na Mungu alimponya.

Website ni kichomi, na nafikiri waweza subiri lifetime kufanikisha kwa njia hiyo. Ukitumia njia yako jiandae kukaa hata majuma 3 Lagos lkn kama ni zamu yako then Mungu atakugusa tu. Advantage ya appointment, unapata full attention, yaani masomo, ushauri, maombi kabla ya ibada ambayo wise men wanawapitia wote (ndio maana visitors huwaoni wakianguka sana kanisani, kwani wanakuwa weshafanyia maombi ya kina kabla ya misa). Ushauri wangu, jipendekezeni tu kwa Martha.
MKIIJUA KWELI ITAWAWEKA HURU; tatizo hapa mama hajui kweli za mungu zinasemaje wala hakuna hata mmoja katika hiyo familia anayezijua hizo kweli vinginevyo mngekaa naye chini tu na kudiscuss kweli za neno la mungu kwa amani naye angeelewa. Kule aliko nako ni upotevuni kwa maana kweli ya mungu haipo katikati yao; ni mungu gani huyo atakaetambulisha kuwa tatizo ni uchawi lakini uwezo wa kulitatua hana? ni mungu yupi huyo wanayemuabudu katika hilo kanisa ambaye uchawi unatesa waumini zake lakini hatatui? au sadaka iliyotolewa haijatimia mpaka yaletwe mamilioni? kweli za mungu ni silaha yako binafsi ya kuishi nazo na si za kukutia utumwani mwa SCOAN au T.B NANI SIJUI; Hakuna mwanadamu yoyote ambaye yuko juu ya neno la mungu wala ambaye ana hati miliki nalo kwa kuwa linatenda kazi lenyewe kama lilivyo; kondoo wa Yesu ni wa Yesu na si wa mchungaji huyu au mchungaji yule au askofu yule, tena nyumba iliyofarakana haiwezi kusimama kwa maana Yesu alisema mkiwa na umoja mtajulikana kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu kwelikweli. Madhehebu dhehebu hizi zilizoibuka na kauli mbiu za kilokole ni upotevu mtupu na ni za maajenti wa freemasons; kama mti hujulikana kwa matunda yake mbona familia zote za hao walioitwa walokole zina faraka za kila aina? uponyaji sio ishu hata shetani mwenyewe huitisha moto nao ukashuka kutoka mbinguni na tena je imani zetu zitajikita juu ya miujiza na mazingaombwe? HOJA IMEJIBIWA tafuta fundi wa kweli wa neno la mungu ambaye hana mamlaka yoyote kanisani aendeshe vipindi virefu vya neno la mungu ndani ya familia yenu.
 
Mungu yupo na makanisa ya kweli yapo na wokovu pia upo. Tatizo kubwa la RC na makanisa ya wokovu lililopo ni kwamba wanaona RC ni sehem tu ambayo watu ukutana jumapili pia haliwakuzi kiimani waumini wake zaid za kufwata shajala tu na hii ni kweli wa RC wengi hawasomi biblia ila sara zao wamezishika( katekisimu) Pia RC wanaomba sana kupitia watakatifu ambao we are nt sure kama kweli ni saint . Walokole wao wanaomba straight kwa Yesu hakuna kupitia kwa bikira maria, joseph mt agustino hakuna cha rozali wala nin wao ni Yesu. So mtu akiokoka na akiambiwa miaka yote uliyokuwa RC ni bure na ukaamin ni lazima ubadilike. Ndo mana nao Rc wakaanzisha kalismatic kwa ajili ya Wa Rc wenye iman kali ambao ni sawa na walokole. Mama yako yupo sawa tena sana ukimwi wengine wanasema ni pepo ndo mana ukiombewa linatoka ila pia hospital kuna dawa so ugonjwa kutibika hospital haina mana kuwa sio pepo. Kuna mapepo mengine kazi yake ni kukutia umaskin kila mwisho wa mwez lazima uumwe tena ulazwe usidhan ni ugonjwa wa kawaida.

Falsafa mbaya kabisa!

Kama unaamini huyo mama yetu yupo sawa, unaweza kuniambia kwa imani hiyo aliyonayo anamsaidiaje mumewe (ambaye yeye anaamini ni mchawi) ili aachane na uchawi wake kwa kutumia chuki na kujitenga?

Maelezo yako ndio hasa chachu ya mafarakano katika jamii. Mchungaji mwenye ufahamu na maarifa hawezi kumwambia muumini wake aache kutumia dawa na yeye awe anamuombea tu. Nafikiri muanzisha mada ameeleza jinsi rafiki wa mama yake alivyofariki kwa kansa ya ziwa sababu ya imani kama yako.

Yooote ulioandika yanakosa maana kwa jambo moja tu: NDOA YA WATU IKO HATARINI. Mchungaji asiyeweza kumuita mume kanisani na kuliweka mezani suala lao, hana nafasi katika Kristo (upatanishi). Mimi nikiwa mchawi, ndugu zangu hawatanisaidia kwa kunitenga bali kwa kunipenda na kuniombea ili nami nibadilike na kumfuata Mungu kama wao.

Kama mama na mchungaji wake hawana uthubutu wa kumkabili mchawi mmoja kwa maombi na kumshinda, basi nina mashaka na Yesu wao. Baba hakupaswa kuchukiwa (kama inavyodhaniwa mchawi) bali alipaswa kuhuishwa.

Mchungaji HAPASWI kumwambia mama kuwa mumeo ni mchawi. Alichopaswa kufanya ni kumuombea rehema ili kwamba, matatizo ya nyumbani kwake yakome. Katika hali ya Kimungu, baba angeanza kupata shida na yeye mwenyewe angejikiri na kubadilika.
 
Ishu ya uchawi ni ya ndani sana ila napata wasiwasi unaposema babako ni mfanyabiashara mkubwa.
Mimi sikuzote naamini ili uwe mfanyabiashara mkubwa lazima kuikinga biashara yako( zindiko) kufanya biashara ya mkono mweupe dunia hii ni kazi sana either uwe mcha mungu au mshirikina la sivyo wenzio watakuibia kamazingara. Mie nina rafiki yangu babake mchawi ila yeye hajui mana tukiwa kijiweni tunamsema sana mzee wake jamaa akiwa anakuja tunachange mada tunaanza habari za mpira,mziki. So yeye ataweza kujua tu siku akigombana na mtu au mlevi ambwatukie hilo.

Unahitaji kutuliza ufahamu wako.
 
Mie kinachinijia ni 'kwa nini mama kaamua kuwa mlokole now?'

Mtu atakayeweza kung'amua hicho unachofikiria Konnie, nadhani ndio namna nyepesi ya kutoa msaada kwa hiyo familia.
Wapo wamama wanaamua kuokoka kwa kuwa waume zao ni walevi, wazinzi na mambo mengineyo mabaya hivyo wanaona Mungu ndio tumaini la mwisho.
 
Tena hao wanaojiita walokole ni wabishi jamani
hata penye ukweli atakusomea misitari yote ya bibilia hadi aone unashindwa.

Dada yangu na mumewe wanaishi kila mtu kivyake kisa ulokole wa dada
hawaambiliki.

Ila kwa kuwa ni la kifamilia zaidi inabidi mkae chini mliangalie kwa undani zaidi.
Pole sana.
 
Wapendwa wanajf naombeni
ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa
familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha
yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa
mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani
tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake
yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa
kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka
nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba
kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu
nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote
ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna
kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye
maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga
bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende
hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni
dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana
na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya
matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na
msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia
ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na
kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na
Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart
attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye
makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani
alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda
akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post
yangu ndefu, naombeni michango yenu.

nawaza kwa sauti hivi ukristu kama si wazungu kuja africa tungeujulia wapi?uislam kama si waarabu kuja africa kufanya biashara tungeujulia wapi?jaman naomba tuelewe kuwa huu udini uliletwa tuu kwa nia ya kuja kutufarakanisha na si kingine...heri yangu ninae mtumainia Mungu ila sina dini kabisaaaaaa...sitaki kichefuchefu
 
Ukiona mchungaji, askofu, padre, nabii etc anakwambia flani ndiye mchawi kwenye familia au ukoo, anza kutilia mashaka mtu huyo, hizo ni kauli za waganga wa kienyeji maana vita vyetu si vya damu na nyama. Hizo kauli hazitoki kwa Mungu maana lengo lake ni kuleta mafarakano baina ya watu.
 
Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.

Ina maana dada Kaunga, kweli mtu pekee anayeweza kutazama suala la hiyo ndoa rationaly ni T.B Joshua?! huyo pekee?!

Sidhani kama ni kweli! Inakua kama Mungu amebinafsishwa ujue!

Na Sidhani kama Mungu ninayemuamini ni wa aina hiyo!!

Hapa hapa kwetu kuna watu wachamungu!
Kumbuka ni Mungu ndiye anayeokoa watu sio mtu!
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.
Inawezekana kumbadilisha mama!
  1. Muelezeni ukweli kuwa mdogo wenu alikuwa na bacteria tumboni.
  2. Jaribuni mmoja wenu aende huko anakosali (hata wewe ukirudi) then mjue wanamahubiri gani yanayoleta chuki, then muone kama mama anaamini ktk biblia au ktk maneno ya mchungaji? au waumini wenzake (anaweza kuwa muunimi specific)
  3. Kama anaamini ktk biblia, basi kumfanya awe na upendo ni rahisi ni kumuomba Mungu na kumuonesha vifungu vya biblia vinavyoonesha hatupaswi kuhukumiana hapa duniani mwenye mamlaka ni Mungu peke yake, na Mume wake wa ndoa anahitaji kumuheshimu
  4. Ila kama anasikiliza sana watu hiyo inabidi muwe na ukaribu au ufahamu wa hao watu walivyo mbrain wash
  5. All in all, muombeeni awe na wokovu wakuwapenda wengine kwani hata Yesu Kristu hakumchukia mtu.
 
cheza na dhehebu linaitwa jitengeni wewe!
Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.
 
Tena hao wanaojiita walokole ni wabishi jamani
hata penye ukweli atakusomea misitari yote ya bibilia hadi aone unashindwa.

Dada yangu na mumewe wanaishi kila mtu kivyake kisa ulokole wa dada
hawaambiliki.

Ila kwa kuwa ni la kifamilia zaidi inabidi mkae chini mliangalie kwa undani zaidi.
Pole sana.
Mara nyingi ubishi huendana na kutokujiamini, kuna kitu kingine huwa nashindwa kuwaelewa hawa watu hasa pale wanapoanza kung'ang'ania hoja na mwisho kusema kuwa huwezi kuelewa kwa akili ya kibinadamu, wakati wananishawishi kwa akili ya kibinadamu.
mimi napendekeza ni wakati muafaka sasa kufundisha elimu ya falsafa, kwa shule zetu za upili. Hata matatizo ya kiimani yaliyopo sasa yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uwezo mdogo wa kufikiri.
Dini zimekuwa biashara kubwa afrika hasa sehemu ambazo watu wanaelimu ndogo na umaskini uliokolea, matokeo yake zimezidi kujenga mifarakano katika jamii kuliko mapatano, sasa hizi sio sifa za wanayedai kumuamini ila ni kinyume chake
 
Falsafa mbaya kabisa!

Mie sijasema kama ni mchawi babake yaliyosema ni mapepo kuwa yametumwa na babake kama nimeelewa vzuri. Mama ndo mana hajamwambia baba direct mpaka saiz kuhusu ilo ila kunavita ya kiroho hapo inaendelea kat ya hao wanandoa.
 
Ina maana dada Kaunga, kweli mtu pekee anayeweza kutazama suala la hiyo ndoa rationaly ni T.B Joshua?! huyo pekee?!

Sidhani kama ni kweli! Inakua kama Mungu amebinafsishwa ujue!

Na Sidhani kama Mungu ninayemuamini ni wa aina hiyo!!

Hapa hapa kwetu kuna watu wachamungu!
Kumbuka ni Mungu ndiye anayeokoa watu sio mtu!

Mlokole ninayemjua mimi, ni yeye pekee. Labda kwakuwa sijaamua kuwafahamu wengine, mimi nimetoa mfano tu na ndio maana nikasema sijui sana.
 
Kabla sijasoma post za wengine, naomba nichangie kabla kichwa hakijachakachuliwa.

Hapa naona tatizo zaidi ya ulokole.
Wazazi wako wanaweza kuwa wamekuwa na matatizo katoika ndoa yao kwa muda mrefu ambayo hajakupatiwa ufumbuzi.
Labda, kutokana na baba yako kuwa bize, attention ilipungua kwa mama, hii ikamfanya mama kuwa mpweke kwa kipindi kirefu. Lakini alivumilia for the sake ya ndoa.(Mama yako alikuwa na kazi?)

Baada ya mama yako kukutana na rafikiye mwenye matatizo ya kansa (wote wana frustration zao za maisha), wakaungana na kutafuta faraja kwenye ulokole. Na kama ulokole umeweza kujaza gap iliyotengenezwa na baa yako, hakuna jambo mama anaweza kuwaelewa eti aachane na ulokole wake.

Walokole wanachofanya ni kujaza gap iliyosababishwa na matatizo yako, kama huna imani nzuri unaweza kuwa 'brain washed'.

Suluhu ya maumivu ya muda mrefu katika ndoa sio rahisi kuyatibu kijuu juu, imagine tangu miaka ya 80 wameoana it's 30+ years. Kwanza inategemea na uelewa, utayari wa wenza wote wawili. Huwezi mlazimisha mama aelewe, hujui amekuwa akiumia kiasi gani kimya kimya, huwezi mlaumu baba, huwezi jua ni kiasi gani anaamini alikuwa najitoa kwa familia.

Hapa inabidi wewe kijana ukae nao, mtafute chanzo cha mama kujikuta kwenye ulokole mkali kiasi hicho, ndio muanze kufatuta suluhisho. Kumlaumu mama peke yake itaongeza ukubwa wa tatizo. Usiegemee upande wowote, kuwa neutral ili uweze kuona mambo kwa upana wake.

Mungu akutie nguvu usuluhishe wazazi wako.

Nimeupenda mchanganuo wako, na ndio maana counseling nzuri inatakiwa. Changamoto ni kumfanya huyo mama kwenda au hata kukubali hiyo counseling na ndio maana nikashauri aende kupatiwa hiyo counseling kwa mlokole ambaye kwa maoni yangu huwa ana dig kutafuta root causes ya matatizo mbali mbali.
 
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.

Kwenye red ya kwanza ni wajibu wa mzee wako kutafuta wazee wenye hekima na kuzungumza na mama yenu ili afafanue ni kwa vipi baada ya miaka mingi tu ya ndoa, sasa anamwona mkuu si msafi tena kwake.

Red ya pili kwamba mama anatoka saa 11 asubuhi na kurudi usiku hiyo ni ishara kwamba labda amepoteza imani ya upendo na mzee kiasi cha kukubaliana na ushauri wa nje kwamba kuna sehemu za kuondoa wimbi la mawazo na kuburudisha roho kwa pambio na maombi ambazo si rasmi bali madarasa ya shule au majumbani mwa watu.

Red ya tatu umeema mzee ni "businessman" wa nguvu na bila shaka amevuta umri hivyo kumfanya kuwa mzee wa busara. Hapa tena inabidi mzee nae aangalie utaratibu wake wa shughuli za biashara anazozifanya kwani huenda zimeonoa kabia mawazo kwamba ana mke na familia. Nafikiri inabidi afikirie kusafiri pamoja na mama angalau mara mbili kwa wiki inatosha.

Red ya nne huyo mama ambae amemuitroduce mama yenu kwa walokole ndie tatizo na pengine amekuwa akimlia timing mzee wenu kwa muda mrefu sana. Alipoona amempata mama yetu nae mama yenu akatoa malalamiko yake kwa huyo mama na ndipo alipochukua advantage ya kuvuruga kila kitu.

Kuna kitu kinazungumzwa sana kwamba kinaharibu sana ndoa nyingi nacho ni "maneno ya watu", maneno ya watu ni sumu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom