MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

Hebu tueleze huwa unatumia kigezo gani au kipimo gani kujua kuwa imani fulani haipo sawa na nyingine ipo sawa....

NB:
IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Kila imani hutenda kazi.Inategemea msingi imani hiyo ni upi. Hata lucifer anauwezo na wapo wafanikiwayo kupitia yeye.Ni akili yako kuamua unahitaji imani ya mlengo gani. MUNGU wa Kweli au miunga(ushetani)
 
Kuna jamaa alimfukuza mkewe kwa kesi kama hiyo...Mke aliambiwa afanye maombi ya mvua yani siku tatu mfululizo bila kupumzika usiku ni mchana.....Basi jamaa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa kusafiri masafa marefu, siku anarudi kutoka safari amechoka atleast apumzike ale chakula cha nyumbani na mkewe;,,, ile kuingia tu ndani kakuta mke ana roroma kwa maombi wala ajigusi...

Basi pale pale jamaa alimpiga kipigo kitakatifu na takalaka juu....Mke yupo mtaani kama amechanganyikiwa anazunguka tuu...

Kwa kweli wanawake ndo wanaidanganyika na haya makanisa kwani asilimia 80% ya waumini wao ni wanawake...

Point of correction:
Usifikirie wanawake ndio hudanganyika ni kua wanawake ndio hua mstari wa mbele kubeba mzigo wa kuombea nyumba zao, na ukae ukijua familia nyingi zina matatizo kadha wa kadha kwa hiyo option ni either mpumbavu akimbilie kwenye ushirikina au mwerevu akimbilie kwenye maombi

Na suala la kuomba mvua unahisi ni tatizo??au kuomba 3days ni tatizo?au wewe ni mgeni wa maandiko

Mwanamke aplay party yake nyumban as a woman mda wake mwingine akiutumia kumtukia Mungu sioni tatizo maana kama kasi ya maovu inaongezeka kwa nini kasi ya kusali isiongezeke?BTW UFALME WA MBINGU UNATAFUTWA KWA BIDII

Pili kwa mleta mada:
Sikuoffend lakini baba yako kua msomi au tajiri haimaanishi kua hawezi kua mshirikina maana ushirikina nao umegawanyika kwani wapo matajiri wengi utajiri wao umeambatana na utoaji wa kafara mbalimbali ili mambo yao yazidi kufanikiwa,hilo hulijui???

Mbali na hilo inawezekana kutokana na uwezo wake wa kifedha yy ndio tatizo mfano kama ana mahusiano nje ya ndoa,hamweshimu mama yako,hana mda na mambo ya kiimani n.k yote haya yamempelekea mama yako kua frustrated kiasi cha kua na mzigo wa kuinusuru ndoa yake lkn kwako wewe unaweza usimwelewe what she is going through

Nachokushauri kaa nae kwa upendo atleast ujue chanzo cha yeye kuwa hivyo ukishajua tatizo lipo kwake au kwa baba utajua wapi uanzie kusolve tofauti zilizopo
 
Hivi hiyo appointment SCOAN nyinyi mnaipataje kirahisi...

Maana mama yangu ameomba hiyo chance ya ku visit muda mrefu lakini mpaka leo haieleweki,, kwanza alienda kwa agent wao pale karibu na Mariedo akakuta hapaeleweki utaratibu unakwendaje maana watu kibao wanalalamika,,, then tulijaza fomu kwenye website ya SCOAN na baada ya kumaliza tukapewa namba za simu za kupiga ku confirm kama inakuaje.. Hizo namba hatujawai kuzipata kila ukipiga ni busy au not rechable

Kuna njia yoyote ya kumsaidia Mama apate visiting appointment there maana amekwama kabisa japokuwa ameshajiandaa kwenda hata kesho akipata chance..

Kuna uzi fulani kwenye jukwaa la hoja mbali mbali kuhusu Martha agent wa SCOAN hapa Tanzania, inahitaji uvumilivu kupitia njia yake lakini ndio yenye uhakika wa mtu kupata fully attention kwa men of God there, lakini baadhi ya watu wamekuwa wakienda wenyewe na kama ni mpango wa Mungu wanafanikiwa; kama uliona live service ya last Sunday Emmanuel TV kuna mdada mmoja wa Kitanzania alijilipua (ukiwa na shida kweli huwezi kuona aibu kujilipua) na kumlilia T.B Joshua kanisani kuhusu hali ya mama yake ambaye hakupata nafasi ya kuingia kanisani (kipaumbele ni wenye appointment) na T.B Joshua alimuattend na Mungu alimponya.

Website ni kichomi, na nafikiri waweza subiri lifetime kufanikisha kwa njia hiyo. Ukitumia njia yako jiandae kukaa hata majuma 3 Lagos lkn kama ni zamu yako then Mungu atakugusa tu. Advantage ya appointment, unapata full attention, yaani masomo, ushauri, maombi kabla ya ibada ambayo wise men wanawapitia wote (ndio maana visitors huwaoni wakianguka sana kanisani, kwani wanakuwa weshafanyia maombi ya kina kabla ya misa). Ushauri wangu, jipendekezeni tu kwa Martha.
 
^^
Simameni kama familia kamili,,mwacheni aende siku akikutana na ukweli atarudi.
..
Nani kasema kila mhubiri hupata wafuasi kwa njia za kawaida bila madawa? You never know huko amekutana na mzizi upi.
^^
 
Makanisa ya kilokole ni janga kwani mengi hasa yanayoanzishwa na watu binafsi ni mradi wa kuchuma fedha kwa watu baada ya kuwazubaisha kisaikolojia. Kuna huyu fernandes hua anawaambia waomini wake wakiumwa wasali tu wasiende hospitalini. Wiki mbili zilizopita alifumwa na muamini wake wa zamani mwanamke mmoja hospitali IMTU. Yule mwanamke akaninong'oneza 'muone anaangalia chini ili tusimtambue kama amekuja hospitali'
 
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.

Yani huyo mama yako atakuwa hajui maana yakuokoka.maana kama angekuwa anafahamu ilo asingejitenga na wenzio.kwanini yy asiwe ndo mfano wa familia?angeu2mia vizuri huo ulokole wake angeweza hata kumshawishi mumewe kuokoa.huyo nimbaguzi anawezaje kuujua uchafu wa kiroho wa m2?hata maandiko yanasema usimhukumu mwenzio.ss yy kama kaamua kum2mikia mungu sio kwa style hiyo.anatakiwa akaechini aishauri vizuri familia kuhusu kuoka kwake nakwaambae anaamini ataweza kuokoka.sio kwakumlazimisha m2 na kuwatenga.mshauri akaisome vizuri bible.
 
Kwa sisi walokole tunamuhesabu huyo mama kuwa ni MCHANGA KIROHO yani bado hajujua maana halisi ya WOKOVU, lakini akizidi kudumu ktk imani na kusoma neno la Mungu na kupata mafundisho mbalimbali atakuwa KIROHO, na hayo malalamiko yote yatakwisha.

BELIEVE ME.
 
sokwe, Ablessed na Kaunga, Biblia inasema palipo na Roho wa Bwana hapo pana amani.Mtu anayesema ameokoka basi
1. Anapaswa kuwa na upendo wa kweli (Maana Mungu ni Pendo)
2. Anapaswa kuwapenda watu wa nyumbani mwake (Maana asiyewajali watu wa nyumbani mwake ameikana imani tena ni mbaya kuliko asiyeamini)
3. Ata mpenda na kumtii mwenzi wake zaidi (Maana ndivyo Biblia inavyotaka)
4.Atashiriki ibada na watu wa nyumbani mwake maani ndiyo impasayo Mkrosto.

Kwa maelezo aliyoyatoa ndugu sokwe, ni kweli bila shaka huyo mama hajaamia katika kanisa la walokole in the strict sense. Pengine anasali kwa makanisa yanayomtaja Kriso lakini ni watu wenye imani iliyopotoka na wapo wengi sana hapa Dar. Nashauri kama wewe ni mtu wa imani hebu mwombe Mungu na mama yako atafunguliwa. Amehamia kanisa gani? (you ve a discretion to answer)
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa wanajf naombeni ushauri, mama yangu ameingia kwenye makanisa ya kilokole japokuwa familia nzima ni wakatoliki, tangu ameingia kwenye makanisa hayo maisha yake yamebadilika sana, hana ukaribu na mumewe yaani baba yetu! Kwa mfano walikuwa wanasali pamoja asubuhi na jioni pamoja sasa haiwezekani tena kwani Ana amini baba yangu ni mchafu! ashirikiani na ndugu zake yaani wajomba na shangazi zetu japokuwa wamefanya jitihada kubwa kujaribu kutafuta muda kuzungumza nae imeshindikana! Kwani anatoka nyumbani saa 11 alfajiri na kurudi usiku.

Baba yetu amekuwa kwenye kipindi kigumu sana kiasi cha kuniomba kuzungumza nae kwani Mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia yetu nimeshindwa kuzungumza nae kwa sasa kwani naishi Japan na familia yote ipo tanzania, natarajia kurudi nyumba kwa likizo fupi mwezi wa 12, kuna kipindi Mdogo wangu alikuwa anasumbuliwa na tumbo akampeleka kwenye maombi akaonekana Ana mapepo yaliyokuwa anadai baba yetu ndie anamloga bwana Mdogo!

Nilipopata taarifa hizo nilishtuka sana nikamuomba Mdogo wangu aende hospital kwa uchunguzi bahati nzuri Nina rafiki yangu tulisoma pamoja ni dr wa matumbo pale muhimbili, baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana na bacteria h. Pylori ambao walisababisha apate ulcers pia, baada ya matibabu amepona kabisa! Baba yangu ni mfanya biashara mkubwa sana na msomi Sio Kwamba najisifia ila ndio ukweli, alifanya kazi kwenye jumuia ya Africa mashariki miaka ya 80, akaamua kuacha kwa hiyari yake na kijiingiza kwenye biashara tangu miaka hiyo, anafanya biashara ulaya na Middle East na marekani, baba yangu anaweza kuwa mchawi?

Japokuwa habari hizi hazijamfikia Kama zikimfikia anaweza akapata heart attack Kama Sio stroke, kuna mama aliyemuintroduce mama yangu kwenye makanisa haya ya kilokole alikwisha fariki na cancer ya ziwa kwani alikataa matibabu ya hospital! Napata Shaka ikitokea mama kuumwa huenda akakataa Kwenda hospital pia au kuficha maradhi yake, poleni kwa post yangu ndefu, naombeni michango yenu.

Pole sana kaka, mama yako amekuwa HYPNOTIZED..Amekuwa na HISIA KALI KWA MUNGU ( STRONG FEELINGS ABOUT GOD ) badala ya kuwa na IMANI KALI KWA MUNGU ( STRONG FAITH TO GOD ). Kabla sijatoa ushauri ningepnda kujua umri wa mama yako na baba yako na mtoto wake wa mwisho ana umri gani.
 
Hebu tueleze huwa unatumia kigezo gani au kipimo gani kujua kuwa imani fulani haipo sawa na nyingine ipo sawa....

NB:
IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Imani huja kwa kusikia, na kwa kusikia kutoka katika neno la Mungu. Imani zote, zote uzijuazo, huja kwa kusikia. Ila imani ya Kikriso huja kwa kusikia maneno ya Kristo. Kwa hiyo imani ya kikristo huja kwa kusikia maneno ya Kristo. Imani isiyoendana na neno la Kristo sio imani ya kweli as far as Christianity is concerned. Tatizo leo watu wameweka imani kwa watu badala ya Mungu. Utasikia mtu anasema mimi nasali kwa flani, mimi nasali kwa apostle flani, na anfanya yote ayasemayo postle huyo hata kama ni kinyume na mapenzi na neno la Mungu. Kama tusipokuwa na maarifa, tutaangamia
 
Haya maswala ni magumu kuliko unavyoweza kufikiria. Mtu wa hivyo ukimforce ndo unazidi kumpoteza. Kuna ndugu yangu aliingia huko kwa kweli ilikuwa kasheshe kwenye familia. Alitafutiwa na mke hukohuko kanisani akafungishwa ndoa bila wazazi wala sisi ndugu kujua mpaka wazazi wakamwachia laana fulani. Alikuwa haambiliki kamwe na wanafamilia wote alituona tuna mapepo. Baada ya juhudi zote kushindikana tuliamua kumwacha. Miaka 12 baadae ndipo alipogundua kuwa alikuwa amepotea na kuamua kurudi ktk familia na kutoka kwenye hilo kanisa.
Nakushauri mwacheni tu ipo siku atarudi ingawa anaweza asirudi kamwe. HIYO SUMU NI KALI SANA. ZIDISHENI MAOMBI
 
Pole. Yalinikuta kwa mke wangu alivyohamia kwa makanisa hayo na kutaka kuwahamishia huko watoto. Mimi nimetumia udikteta kidogo na tunakaribia mwaka wa kumi. NiPM tuongee. Pole.
We ulitumia udikteta kidogo?? mimi mke wangu alihamishia nguo kule redio safina nikanyamaza ..kesho yake natoka zangu kwenye mishe zangu saa 4 usiku nikakuta wamejaa wanampigia maombi kidi yangu joto limempanda ghafla ...nilichokifanya hadi leo sijaona hata sura moja pale kwangu ikabidi na wife aachane na ile dhehebu
 
Wengi wao ni FANATIC tu hawajui mbele wala nyuma kwa imani zisizo na mwelekeo kwa kutumia msemo usemao " IMANI NI KUAMINI YALE USIYYAONA....." na wengi wao wanjifanya kuwa wao ni "MOVING ENCYCLOPEDIA" na huwezi wakosoa au washihisha pale wanapokosea. Na kuishia kutaja tu namba za m-pesa, tigo pesa, airtel money na kufungua benki na saccoss kibao na kulazimisha waamini wawachangie pesa kibao.
Ushauri wangu, mkalishe chini mama yako mweleze kinagaubaga namna sahihi ya kuabudu na kupata maana sahihi ya yale ahubiliwayo ili asije akapotoka, kwani naamini mama siku zote ni msikivu, mwerewa na mtendaji wa yale ashauliwayo , naamini atakuelewa : Never give in bro, always strive for an execcelence", as there is nothing imposible under the sun.
 
Kabla sijasoma post za wengine, naomba nichangie kabla kichwa hakijachakachuliwa.

Hapa naona tatizo zaidi ya ulokole.
Wazazi wako wanaweza kuwa wamekuwa na matatizo katoika ndoa yao kwa muda mrefu ambayo hajakupatiwa ufumbuzi.
Labda, kutokana na baba yako kuwa bize, attention ilipungua kwa mama, hii ikamfanya mama kuwa mpweke kwa kipindi kirefu. Lakini alivumilia for the sake ya ndoa.(Mama yako alikuwa na kazi?)

Baada ya mama yako kukutana na rafikiye mwenye matatizo ya kansa (wote wana frustration zao za maisha), wakaungana na kutafuta faraja kwenye ulokole. Na kama ulokole umeweza kujaza gap iliyotengenezwa na baa yako, hakuna jambo mama anaweza kuwaelewa eti aachane na ulokole wake.

Walokole wanachofanya ni kujaza gap iliyosababishwa na matatizo yako, kama huna imani nzuri unaweza kuwa 'brain washed'.

Suluhu ya maumivu ya muda mrefu katika ndoa sio rahisi kuyatibu kijuu juu, imagine tangu miaka ya 80 wameoana it's 30+ years. Kwanza inategemea na uelewa, utayari wa wenza wote wawili. Huwezi mlazimisha mama aelewe, hujui amekuwa akiumia kiasi gani kimya kimya, huwezi mlaumu baba, huwezi jua ni kiasi gani anaamini alikuwa najitoa kwa familia.

Hapa inabidi wewe kijana ukae nao, mtafute chanzo cha mama kujikuta kwenye ulokole mkali kiasi hicho, ndio muanze kufatuta suluhisho. Kumlaumu mama peke yake itaongeza ukubwa wa tatizo. Usiegemee upande wowote, kuwa neutral ili uweze kuona mambo kwa upana wake.

Mungu akutie nguvu usuluhishe wazazi wako.
 
Hebu tueleze huwa unatumia kigezo gani au kipimo gani kujua kuwa imani fulani haipo sawa na nyingine ipo sawa....

NB:
IMANI ni hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Vipo vigezo vingi lkn siwezi kuvitaja hapa maana kila mtu ana uhuru wa kuamini anachoamini. Pia naheshimu imani zote, hata ambazo sikubaliani nazo. Nisingependa kuchakachua uzi wa watu , turudi kwenye mada ili mwenzetu apate msaaada
 
Mie kinachinijia ni 'kwa nini mama kaamua kuwa mlokole now?'

Mdogo wangu Ablessed put it well.
Alitakiwa achange to the better na sio to the worse. Siamini uwepo wa Mungu kwenye hilo dhehebu lake jipya ambalo badala ya kuimarisha familia linaleta mtafaruku.
Nini cha kufanya, kwakweli sijui sana maana hao watu wanakuwa kama fanatic fulani. Kama mnaweza, book appointment SCOAN pale si tu mtapata derivelence lkn pia counciling yenye lengo ya kuwapatanisha. Nafikiri njia hiyo mama yako anaweza ielewa. Be smart when presenting that issue; mama mwambie tunsmpeleka baba ili kama kuna mavitu ya ukoo au biashara yakavunjwe na familia yote iwe derivered, baba, mwambie mnampeleka mama kwa councilling kwa kuwa anaoweza kuwasikiliza ni walokole wenzake na wewe unaamini the only smart mlokole anayeweza kutazama swala lao kwa rationally ni T.B.Joshua na ministry yake ya reconciliation.
 
Karismatik ya kikatoliki inatofautiana na walokole wengine?

Mi nawaona sawa tu

Unajua Kaunga uliyosema ni kweli sister lkn kuna baadhi ya imani haziko sawa na nadhani waamini wengine walishazistukia japo si rahisi kuzijua. Ni vizuri akaihandle hii issue vizuri. Nimeona jamaa zangu kadhaa wakitekwa na hii mitego ya imani na hasa wanapoonekana wana matatizo. Roho yoyote inayopingana na mafundisho ya kristo haitokani na Mungu . Maana hata Bwana alikua mnyenyekevu , sasa hii inayoleta mtafaruku ktk familia inatia shaka kidogo. Kama ni wakatoliki basi wajaribu pia kwenda pale ubungo EMAUS kuna catholic charismatic renewal ambapo every Saturday na sunday huwa wanakuwepo . Hata hivyo pole Mungu akusaidie tu kuliokoa hilo jahazi bro.
 
Hii asilimia umeipataje?

Back
Top Bottom