Jembemtaji
JF-Expert Member
- Aug 21, 2014
- 1,193
- 926
- Thread starter
- #61
Nimekuelewa vizuri sana nitafanya ivyo.
Waongee nao ili iweje? Wanalipwaje pesa kwa kutimiza wajibu wao?
Ndo tatizo la wananchi wengi kutokujua sheria wala taratibu japo kidogo. Watumishi wengi kwenye idara za serikali wakishakuona ww ni kiazi watakusumbua sana.
Mtoa mada,mimi nipo idara ya mahakama ushauri wangu kwako usitoe rushwa wala usiahidi chochote kwa hao watumishi. Kuhudumiwa ni haki yako ya msingi.
Fanya utafiti ulijue jina la hakimu anayesimamia kesi ya mirathi,jina la karani wa mahakama,na jina la muhasibu.
Andika barua ya malalamiko,barua ieleze tatizo lilivyo orodhesha majina ya wahusika namba ya kesi ni muhimu. Apa pia itategemea je,hukumu ya mirathi ilishatoka? Kama imetoka na mnayo mkononi shida itakuwa kwa muhasibu wa mahakama.
Kuna dawati la malalamiko la mahakama wasilisha barua hapo au laah mtafute afisa utumishi wa mahakama ya wilaya ya temeke umkabidhi malalamiko yako, nakala nyingine itume kwa hakimu mkazi mfawidhwi wa mahakama ya mkoa pale kisutu.
Kuna mdau amekupa namba apo juu hiyo namba pia inapatikana kwenye mabango yaliyobandikwa mahakaman ni kwa msaada zaidi. Tatizo wananchi wengi ni waoga na sio wadadisi.
Tatizo lako ni simple tu na linatatulika na kwa kukusaidia watumishi wa mahakama tuna vitambulisho ambavyo tunavivaa kifuani ili iwe rahisi kunote majina ya watumishi wasumbufu.
Achana na wadau hapo juu wanakushauri utoe rushwa. Mtu anayetoa rushwa hana tofauti na asiyejielewa huwezi kutoa rushwa kama unajua haki zako,kuhudumiwa ni haki yako ya kikatiba. Kutoa rushwa kwa kisingizio cha kuepuka usumbufu hakina mantiki. Unaweza kupata haki yako bila usumbufu ikiwa :
1.Unajiamini
2.Unafata maelekezo na taratibu unazopewa
3.Unajua haki zako kama mteja.
Zingatia: Malalamiko yawe kwa maandishi. Mfumo wa mawasiliano mkuu wa kimahakama na serikalini kwa ujumla ni maandishi usiende kulalamika kwa mdomo.
Jitahidi kujieleza vizuri wakati mwingine sababu ya uoga unashindwa kujieleza vizuri ukaeleweka.