Msaada: Mafao yameingia kwenye account ya mahakama ya wilaya Temeke, tumezungushwa mpaka tumechoka

Habari ndugu,
Tulikuwa na ndugu yetu alistaafu mwaka 2019 alikua nurse Muhimbili hospital.

Baada kustaafu alifuatilia mafao yake hakufanikiwa kupata. Baadae akaugua akafa 2020, baada ya kufa tunafungua na tukafanikiwa kuingiziwa mafao kwenye hiyo account ya mahakama.

Cha kusikitisha ni kwamba wanatoa hoja tofauti kila tukitaka kuchukua hiyo hela mpaka msimamizi wa mirathi amekata tamaa.

File wanadai halionekani, mara karani amefiwa, mara mhasibu yuko likizo, mara hakimu hayupo.

Naomba msaada kwa mwenye ufahamu kwenye jambo hili tunaweza kwenda wapi kupata msaada.
Tafuta wakili MSOMI,atakusaidieni
 
😂😂😂

Mkuu mimi sio mtaalam wa sheria kabisa.

Ila nashauri awaone mahakama ya wilaya ama ya mkoa watamsaidia.

Ikishindikana afanye mtego na TAKUKURU wamshikishe hakimu mlungula.

Hoja zao eti mhasibu amesafiri, mhasibu akisafiri hasafiri na ofisi, karani haendi likizo na ofisi.

Hapo njia ni moja tu, wawashikishe moto wa takukuru.
Kumbe Hakimu mfawidhi ni mkwara tuu!🙄🙄🙄
 
Kwa ninavyofahamu fedha zikishaingia kwenye account ya mahakama,msimamizi wa mirathi atapewa fomu ya kugawa hizo fedha kwa kila mrithi ,na kila mrithi atasaini kwenye hio fomu,baada ya hapo kila mrithi atapewa vendor form kwa aijili ya kujazwa na bank ambayo muhusika anapendelea fedha zake ziwekwe huko,alafu zitarudishwa mahakamani kwa ajili ya kuprocess malipo,je haya yalikwishafanyika kwenu?

Kama tayari ,ni suala la ufatiliaji tu na hapa inabaki kua ni kazi ya muhasibu ili muweze kulipwa ,hivyo msimamizi wa mirathi anawajibu wa kufatilia kwa huyo muhasibu ajue kua amefikia hatua gani ,nadhani hua wanapeleka mahakama kuu kwa ajili ya kuprocess malipo
Samahani faili likishafika mahakama kuu inachukua muda gani pesa kuingizwa kwenye account za warithi? Nina watoto wa ndugu yangu washamaliza process wameambiwa faili lishapelekwa mahakama kuu, inakaribia mwezi pesa hazijaingizwa kwenye account zao.
 
Back
Top Bottom