Msaada: Kwa sifa hizi naweza kuwa Assistant Lecturer?

Msaada: Kwa sifa hizi naweza kuwa Assistant Lecturer?

Nimeishia hapa. Haitowezekana kuwa Assistant lecturer. Pia kozi ni kachumbari inakua ngumu kuona somo gani utafundisha.

Ingekua walau umesoma kitu hiko hiko bachelors na masters basi ushauri ungekua usome PhD walau unaweza pewa kozi za diploma huko
Ni kweli mkuu, ila niliona kusoma tena HR masters ni kama naongeza kazi kwenda sehemu nisiyopenda.
 
Another guy scored 4.2 from sokoine (bachelor), went to work manually in the US.....3.2 to be a lecture!!! Too low
Thank you, based on the contributions of other members,the only option at hand, is to go back and get a new degree.
 
Mpaka hapa sina namna aisee, wacha nione mwakani naweza rudi undergraduate tena nikiwa na
Criteria za upimaji muhitim wa chuo kikuu Tanzania ni za kijima sana!!

Uwezo wa kuwa lecture ni uwezo wa ku uwasilishaji mzuri wa madam na sio ufaulu pekee!!

Sasa hapa bongo unaweza ukawa na GPA Kali halafu uwasilishaji wako zero na ukawa lecture!

Tuna safari ndefu kama taifa huko tuendako!
 
Anza digrii nyingine ya kwanza, na usirudi nyuma. Ukimaliza, unga ya pili.
 
Habari wakuu, naombeni msaada wa haraka kwa ufafanuzi au ushauri.

Nimekua na passion ya kuja kufundisha vyuo vikuu kwa muda sasa, lakini kuna jambo linanitatiza hapa.

Undergraduate nilisoma Human Resources Management (GPA 3.2) Naomba izingatie hii GPA. Kozi hii haikuwa passion yangu, nilisoma tu kutokuwa na muongozo mzuri kipindi hicho.

Baada ya miaka zaidi ya 7 nikipiga mishe zangu, nikaamua nikasome kitu napenda, nikasoma Post Graduate Diploma ya Mass communication (GPA 4.8)

Je nikisoma masters na nikafaulu vizuri, naweza kuwa assistant lecturer kwenye vyuo vikuu nchini?

Je PGD itafunika udhaifu wa undergraduate? Au yanipasa nianze bachelor degree upya?

Naombeni ushauri wenye uelewa na uzoefu.

NB: usianze Ushauri wa achana kusoma na kuajiriwa katafute pesa, nisiwe muongo, nina vibiashara vinaendesha maisha vizuri, hapa naongelea kufukuzia passion, ile kitu roho inapenda.

Asante
HUWEZI KUWA.
HAUNA SIFA HATA MOJA.
 
Haiwezekani. Hata postgraduate na masters na PhD upate gpa za 5. Kama undergraduate ulizingua hukufikisha walau 3.8 ndio basi tena.

Mimi nikipambana udsm hapo nikaishia 3.5 ndoto zikafa. Ungekuwa walau na 3.5 and above ungepambana kwenye hivi vyuo vya kati mfano ifm cbe tia etc ungeweza kupata .
Lakini wewe una lower second class nikitu ambacho hakiwezekani kabisa
Sifa za lecturers wa vyuo vya kati kama IFM, TIA, CBE, si sawa na za lecturers wanaofundisha vyuo vikuu mfano SUA, UDOM, UDSM? jooohs
 
Nimeishia hapa. Haitowezekana kuwa Assistant lecturer. Pia kozi ni kachumbari inakua ngumu kuona somo gani utafundisha.

Ingekua walau umesoma kitu hiko hiko bachelors na masters basi ushauri ungekua usome PhD walau unaweza pewa kozi za diploma huko
Yaani mwenye PhD anapewa course ya "Angalu" diploma..!!
PhD ni kupewa angalau..!!!

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Na ikatokea bachelor una GPA YA 3.8na Masters ukawa na 3.2 je apa utakuwa na sifa ya kufundisha chuo kikuu?
 
Yaani mwenye PhD anapewa course ya "Angalu" diploma..!!
PhD ni kupewa angalau..!!!

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Eeeh maana tutorial assistant au assistant lecturer wanaangalia sana matokeo ya bachelors. So kwa PhD unaweza ibia ibia walau ukapewa kozi za diploma tena ni kwa "mlango wa nyuma" maana TCU wanaweza kukuletea query.
 
Na ikatokea bachelor una GPA YA 3.8na Masters ukawa na 3.2 je apa utakuwa na sifa ya kufundisha chuo kikuu?
Yes unaweza kuomba kama tutorial assistant ila hauwezi kuomba assistant lecturer maana masters haijafika GPA 4.0
 
Criteria za upimaji muhitim wa chuo kikuu Tanzania ni za kijima sana!!

Uwezo wa kuwa lecture ni uwezo wa ku uwasilishaji mzuri wa madam na sio ufaulu pekee!!

Sasa hapa bongo unaweza ukawa na GPA Kali halafu uwasilishaji wako zero na ukawa lecture!

Tuna safari ndefu kama taifa huko tuendako!
Ni kweli mkuu, nilikua naongea na mtu fulani nae alishangaa sana kwanini wanafanya hivyo, lakini ndo hivyo huwezi bishana, ni kurudi kusoma tu.
 
Back
Top Bottom